Mkeo akifungwa jela utamsubiri au?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkeo akifungwa jela utamsubiri au??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Jul 25, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu ninakiona na sikielewi kabisa.Mwanaume akifungwa jela, mke anapaswa naye kuwa kifungoni angalau cha nje.Jamii inamtegemea amsubiri mumewe arudi nyumbani hata kama anatumikia kifungo cha miaka 50! Sheria hata hivyo inamruhusu mke kudai talaka kama mume atafungwa kifungo cha muda mrefu.

  Lakini mke akiwa na kesi tu..(hapo hajafungwa)...mume ataanza kujitafutia liwazo kwa kisingizio ati mke hayupo nyumbani anahangaika na kesi.Akifungwa ndiyo kabisaaa asahau kumkuta mumewe akimsubiri.

  1.Hivi ni kwanini jamani?

  2.Kwa wanaume tu...mkeo akifungwa utamsubiri amalize kifungo?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Inategemea ni kifungo cha muda gani na kosa alilolifanya. Lakini kwa ujumla my first instict ni kumsubiri na kumpa suport.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Akifungwa kwa makosa kama wizi/ufisadi, kupigana/kutukanana, rushwa ( makosa ambayo hata wanaume hushtakiwa na kufungwa)

  Kifungo cha miaka 1-10, ukiongezea na muda wa kukaa rumande ( kwa kosa ambalo dhamana yake inakuwa ngumu kama makosa ya akina Liyumba)
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapo dada yangu umenipata. Miaka 10 ni mingi. Lakini kama mwenyezi Mungu atatupa uzima I will still hold a torch for her.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ntamsubiri huku nikiburudika na vidumu
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mambo hayo!
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  inategemea kifungo cha mda gani na hii kwa pande zote za jinsia sio mwanamke mtu.na kama kifungo sio cha mda mrefu inawezekana kumsubiri.na pia tuangalieni kumsubiri kivipi? ni msubiri kwenye swala la tendo la ndoa au nimsubiri tuendeleze ndoa yetu? kama ni kuendeleza ndoa inawezekana kwa mda mrefu zaidi kuliko kwenye swala la tendo la ndoa.naweza nikatimiza mahitaji yangu ya ndoa huku namsubiri kwa kujikinga na magonjwa.sisi binadamu vitu vingine vigumu kujizuia.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Habari hii, inaweza kujadiliwa kwa kina kule kwenye kona ya Mapenzi na Mahusiano
   
 11. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  IT would be so nice,if you forward this question to Winnie Mandela cause i believe yeye ni authority tosha na a living example of what not to do when thy husband a public figure is holed up in jail
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sheria inamruhusu kudai talaka? Inategemea ni ndoa ya aina gani. Kama ni ndoa ya kikristo sidhani kama anaruhusiwa kutoa talaka.

  Kuhusu kusubiriana inatagemeana na tabia ya mtu. Hatuwezi ku-generalise. Kuna wanawake wanaweza kumsubiri mume hata kwa miaka 50. Lakini wapo wanaoshindwa. Na mara kadhaa wanaume waliotoka vifungoni wamewakuta wake zao wakiwa na watoto waliozaa na wanaume wengine wakati wao wakiwa kifungoni.

  Vivyo hivyo wapo wanaume waaminifu wenye kuweza kusubiri. Na wapo wasioweza kusubiri mke aliyefungwa au aliye nje tu kwa muda fulani hata kama si kifungoni. Kwa ujumla wote wanatakiwa kusubiriana kama mwingine yupo kifungoni.
   
 13. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sheria inamruhusu kudai talaka? Inategemea ni ndoa ya aina gani. Kama ni ndoa ya kikristo sidhani kama anaruhusiwa kutoa talaka.

  Kuhusu kusubiriana inatagemeana na tabia ya mtu. Hatuwezi ku-generalise. Kuna wanawake wanaweza kumsubiri mume hata kwa miaka 50. Lakini wapo wanaoshindwa. Na mara kadhaa wanaume waliotoka vifungoni wamewakuta wake zao wakiwa na watoto waliozaa na wanaume wengine wakati wao wakiwa kifungoni.

  Vivyo hivyo wapo wanaume waaminifu wenye kuweza kusubiri. Na wapo wasioweza kusubiri mke aliyefungwa au aliye nje tu kwa muda fulani hata kama si kifungoni. Kwa ujumla wote wanatakiwa kusubiriana kama mwingine yupo kifungoni.
   
 14. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  WoS,
  Mtu yeyote ambaye hawezi kuvumilia shida ya mkewe basi anaweza kufanya lolote lile hata kama huyo mke hajafungwa.
  Agano la ndoa ni kwamba tutatenganishwa na kifo, na tuko tayari kuvumiliana katika shida na raha. Shida ya mke wangu au mume wangu ni shida yangu pia. Kama mke wangu yuko kifungoni basi nami ninaingia katika kifungo hicho kwa mujibu wa agano la ndoa yetu. Kipimo cha viapo vya ndoa hupimwa katika masuala makubwa yeyote na si ugonjwa pekee. Kama kweli unampenda mkeo basi hutamsaliti kwa hizo dakika tatu za kujiliwaza.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  I would have been surprised if Winnie's case wouldnt have been mentioned here.
  Coming to her case, she waited for close to 30 years....
  = was it bcoz Mandela was a public figure?
  = ni wanaume wangapi wangesubiri ujana wao uwapitie machoni hadi uishie kisa wanamsubiri mke atoke jela? Hapo juu tu wachangiaji waliokuwa wakweli wamesema kuwa itawawia vigumu.
  = Ni nini kinafanya watu kuona mwanamke tu ndio anapaswa kumsubiri mwanamume?,,,
   
 16. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  it would have done her no harm asking for a divorce,instead of selling her wares in full public view-in fact huyu mwanamke amampunguzia Nelson miaka kumi ya uhai
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  1. Ndiyo... kifungo kinaweza kuwa sababu ya mtu kudai talaka mahakamani kufuatana na sheria ya ndoa ya 1971 ( LMA 1971/aCT.NO.5)..

  In order for the Court to pass a decree for divorce, it should be satisfied that the following grounds, which show that the marriage has broken down irreparably, exist. Some of these grounds are adultery, sexual perversion, cruelty, willful neglect, imprisonment for life or for a period of not less than five years, mental illness certified by at least two doctors or change of religion by either party.
  2.Tabia ya mtu - kweli kabisa..kuna mtu ukimpa mgongo tu..keshavuta kimada ndani! zipo kesi za wanawake walioenda kujifungulia makwao na huku nyuma waume wakahamia/hamishia nyumba ndogo zao.

  Ila ninachoshindwa kuelewa ni kwanini wanawake tu ndio waonekane wanapaswa kumsubiri mume mfungwa...nimeona kwa wenzetu wazungu wako wawazi zaidi..iwe mwanamke au mwanaume - hudai talaka mara moja pale mwenza anapofungwa.Hii inaepusha matarajio yasiyopatikana kwa jamii na kuwa wakweli zaidi kuwa kusubiriana ni kugumu.
   
 18. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sababu ya kufanya wanawake waonekane kama ndio wenye jukumu la kumsubri mume aliyefungwa ni Mfumo-dume wa jamii zetu. Mwanamke anaonekana ni mali ya mume. Yeye ndiye akamtoa kwao na kumleta ndani ya nyumba "yake". Na ni kutokana na mantinki hiyo mwanaume ndiye anayetoa mahari kwa wazazi wa mwanamke, na kumchukua. Kumbe inaonekana mume ana haki fulani ya umiliki juu ya mkewe. Mke kwa mantiki hii hana umiliki juu ya mumewe. Kumbe mume akiwa kifungoni "mali yake" lazima imsubiri mpaka arudi mwenye mali. Wos huo ni mfumo dume wa kiafrika ambao taratibu utaisha tu.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  sawasawa ndugu yangu....
  mfumo huu unaishia taratibu.
  Kwanza siku hizi watu wanakutana mjini wanapanga maisha yao... kwamba mmoja anammiliki mwingine ni kitu kinapigwa vita sana.
  Kusubiri hata kwa mwanamke kunategemea wawili hao walivyokuwa wanaheshimiana, wanapendana, na kujaliana.Hutegemei kuwa mwanaume mnyanyasaji akifungwa basi mkewe atajifungia ndani miaka 30 akimsubiri!
   
 20. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Thread hii ipelekwe katika forum ya mahusiano.
   
Loading...