Mkenya mwenye diploma anaajiri mtanzania mwenye degree au masters...hii imekaaje

Cha ajabu ni nini? Mbona Joshua Nassari anaongoza watu wenye elimu kubwa Jimboni kwake?
Acha mawazo mgando.
 
tuache tabia ya kuwaona wakenya kama ndio wanaakili kuliko sisi. Mjasiliamali Tajiri kuliko wote EA ni BAHRESA kwani yeye ni mkenya. Kuna Vijana wengi wa tanzania wamefanikiwa sana hata shule hawajaenda hao wote huwaoni mkuu hadi ukatoe reference kwa tapeli wa kikenya.

kuna graduates wengi watanzania walianzisha organizations, companies na biashara mbalimbali wamefanikiwa kwa nini tusitumie hawa kam mfano tuwaamasishe watanzania wenzetu ili wafanikiwe?

Ahsante kwa changamoto lakini tunapaswa kuangalia tulichonacho na kikithamini badala ya kuchukua mfano mmoja na kuutegemea.
 
hii ni changamoto kubwa sana niliyokutana nayo,imenisikitisha sana mkenya anakuja bongo af anaanzisha instution ya kutoa elimu ya ujasiriamali hana mtaji wala nini anapewa kachumba kamoja af zile application fees anakuja kulipia hako kachumba af ada za wanafunzi anatumia kulipia mishahara watz wenye vidigrii na masters,,,,huu si ni ujinga kabisa inamaanisha watz wanasubiri kuajiriwa tu? hata kwa vitu ambavyo wanaweza kuajiajiri...............HII NI HATARI CHUKUA HATUA

We hamnazo !
 
wachangiaje wengi hawaja muelewa mtoa mada! anacho jaribu kueleza ni kuhusu ubunifu na kutumia elimu yako kuongeza ajira kwa vijana. kimsingi mtu aliye soma anategemewa kuwa mbunifu zaidi kuliko ambaye hajasoma. elimu yetu lazima ituelekeze kuwa wabunifu na kujiajiri kuliko kuajiriwa.changamoto iliyo mbele yetu ni kuwa na elimu inayo tuelekeza huko na ndio kuchukua hatua.
 
Apple ( Steve Job college drop out ameajiri wasomi wangapi kibao ) Facebook founders ( college drop out ) Bill Gates ( college drop out ,Oprah ( college degree kamaliza baada yakuwa billionaire)so usiwe so insecure .kuwa na degree sio guarantee ya kuwa successful .Peter Jennings ( high school drop out na alikuwa evening anchor na editor ABC .wengi tuuu,
Safi sana Natalia, tatizo la wabongo wanaangalia vyeti kuliko kuangalia uwezo wa mtu. Leo wapo wabongo ambao wameishia darasa la saba lakini wamefanya makubwa sana na wameajiri watu wenye digree zao.
Hili ni tatizo la kimtazamo tu.
 
Bill Gate ameajiri maprofesa,wakati yeye ni college dropout,Steve Job pia,Bakheresa,Hood Morogoro,...yaaani ni wengi ile mbaya.wewe ni mbaguzi wa rangi umeona mkenya tu? How about wahindi ?mtoa mada acha UBAGUZI na Majungu piga kazi huu sio Muda wa majungu
 
Katika kuchangia pia napata picha nyingine ya mawazo mengi ya watanzania. Mwenye mada alichokua anatoa ni changamoto kwamba alilofanya huyo mkenya lingeweza pia fanywa na mtanzania mwenye diploma. Hapo hakijaeleweka nini au ndio hayo anayojaribu kutuonyesha mtoa mada kwamba ninyi ni wavivu hata wa kufikiri? Hatukatai hata darasa la saba angeweza kufanya hilo alilofanya huyo mkenya lakini ni kweli hatuna watanzania wanaoweza kuona hizo opportunity na kuzifanyia kazi? Hebu tuichukulie hii mada kama changamoto kwetu. Wala siwalaumu waliompa kibali sababu hakuna aliethubutu!!!! Hii nchi sijui lini tutakua serious, kuanzia juu mpaka chini sioni. Rwanda juzi tu imetoka katika matatizo lakini watu wako serious, mipango inatekelezwa, uchumi unakua sisi tumekalia siasa tu utendaji zero afu wachina wakija wanalima mchicha bonde la mto msimbazi tunaanza kuoa macho.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kwannini tuzungumzie wakenya??? mimim namifono iliyo wazi, watu walioishia darasa la 7,wameajii degree holder, na niwatanzania, na nivijana wadogo. nadhani hapa si kuangalia vyeti kikubwa ni jinsi ya kutumia utashi , akili na elimu tulio nayo,sio sisi maprofessa kufungua bar tu.
 
Bill Gate ameajiri maprofesa,wakati yeye ni college dropout,Steve Job pia,Bakheresa,Hood Morogoro,...yaaani ni wengi ile mbaya.wewe ni mbaguzi wa rangi umeona mkenya tu? How about wahindi ?mtoa mada acha UBAGUZI na Majungu piga kazi huu sio Muda wa majungu

Baasiiiii,punguza hasira yaheeee,jamaaa kapitiwa tu kimtazamo
 
Sasa kama shida yako ni kazi,elimu ya anayekuajiri inakuusu nini? Wengne wanata kazi wewe unaulizia elimu ya mwenye kazi kwa kujidanganya na degree zako! Wenzako wanachapa kazi bila kujali aliyewaajiri ni nani!
 
ni bora umpe job mwenye hiyo diploma ya kenya kuliko masters ya bongo, waTz wenzangu uozo haupo tu form IV ya 2012 bali pia vyuo vikuu vyetu!!
 
Baasiiiii,punguza hasira yaheeee,jamaaa kapitiwa tu kimtazamo

Jaman 2msamehe mtoa mada inawezekana katika zunguka yake kamuona huyo mkenya pekee akang'oa matairi na kuanza kumuangalia ka role model wake na hata kumtolea mifano kama alivyoeleza. 2mshauri azame zaid na kuona watz wangapi wamefanya hayo na katika mazingira yepi, pia 2silazimishe kila m2 akawa hivyo kwan apart from kuji2ma, kufanya kazi kwa bidii na kufikiria sana angalieni upande wa pili natural gift frm god.
 
Usiwe na mawazo ya kijinga fuatilia Elimu ya Bakhresa au Mengi na waliowaajiri utapata majibu sio unakurupuka na mada za kiji..a

Reginald Mengi,FCCA,FCPA(T).Kwenye uhasibu ukifikia level ya Fellow kama Mengi wewe ni Mtaalam uliyebobea.

Wengine hata Associate bado,wengine ndo kwanza wanajiandaa na Module E.
 
mvumbuzi wa nadhalia ya Genetics afilefi na kuondoka chuoni ndo ukawa mwanzo wa kufanya utafiti wa genetics and hereditary. Sir Isac Newton alifukuzwa shule ndo akaenda kugundua nadhalia ya calculus. tusitishwe wala tusibeze taaluma za watu hata kama ni diploma
 
Hapa tatizo mkenya, degree,n.k Tatizo ni mfumo wa elimu unaomfanya mtu kuamini kuwa 1 + 1 ni mbili bila kufikiri kidogo. Hii dhana ya jibu moja sahihi ndio inaleta jamii ya watu wasio wabunifu,watu wanaoogopa kujaribu jibu lingine au watu wenye woga wa kufeli . Wale waliooneka kufeli darasani na hawana kwa sababu hawakumpa mwalimu jibu analotaka kwani walifikiria zaidi ya jibu moja wanafanya vizuri katika maisha kwa sababu wanazidi ku create vitu vipya na kuwaajiri wenzao waliobaki katika mfumo one correct answer na kupata hizo degree ambazo hawawezi kuzitumia kwa manufaa yao wenyewe zaidi ya kuingia na bahasha ya kaki ikiwa cv kwenye ofisi za so called failures kuwa wahasibu,marketers, walimu nk
 
Mtoa maada hajadharau Diploma,bali alitaka kufikisha Ujumbe kwamba ni lazima Wabongo tufikilie nje ya Box, Tunaamini sana maisha yako kwenye kuajiliwa tu, Leo hii mtu anakuuliza kama kozi fulani inalipa au la, haya ndo maisha yetu, Watu wanaenda Kuongeza elimu ili tu wpate mshahara mkubwa,

Tuna kansa ya kupendasana kuajiliwa bila kujalisha kama hiyo pesa tunayo lipwa inatutosha au la,tunaamini kwamba tunasoma ili tuajiliwe na si vinginevyo, na tukujalibu kuulizana kuhusu kujiajili watu huja na visingizo elfu moja,
 
Back
Top Bottom