Mkenya Kutoa Ng'ombe 20 na Mbuzi 40 kumuoa Mtoto wa Clinton | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkenya Kutoa Ng'ombe 20 na Mbuzi 40 kumuoa Mtoto wa Clinton

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Chelsea Clinton, Mkenya yuko tayari kutoa ng'ombe 20 na mbuzi 40 kumuoa Saturday, August 08, 2009 8:00 PM
  Raia mmoja wa Kenya ambaye alituma posa ya kumuoa binti wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, miaka tisa iliyopita amesisitiza nia yake ya kutaka kumuoa binti huyo wakati alipokutana na Hillary Clinton nchini Kenya na amesema yuko tayari kutoa ng'ombe 20 na mbuzi 40.
  Awali Mkenya huyo Godwin Kipkemoi Chepkurgor mwenye umri wa miaka 40 alituma posa ya kumuoa Chelsea Clinton, binti wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton mwaka 2000 na aliahidi kutoa ng'ombe 20 na mbuzi 40 kama mahari.

  Mkenya huyo amekumbushia nia yake ya kumuoa Chelsea, wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, alipofanya ziara yake nchini Kenya hivi karibuni.

  Hillary alimjibu mkenya huyo kuwa Chelsea ni mtu mzima sasa ana maamuzi yake lakini atamfikishia ujumbe huo.

  Chepkurgor alisema kuwa anampenda Chelsea kwakuwa ni mwanamke mrembo na mwenye nidhamu.

  "Bado sijafanikiwa kukutana naye, nimesubiria kwa muda mrefu na bado nitaendelea kusubiri mpaka siku nitakayokutana naye nimuelezee hisia zangu kwake" alisema Chepkurgor.

  Chepkurgor anaendesha duka lake la vifaa vya kompyuta na electronics katika mji wa Nakuru. Kama posa yake itakubaliwa basi Chelsea atakuwa mke wake wa pili.

  Baada ya kutuma posa yake kwa Clinton mwaka 2000, Chepkurgor alivuta subira kidogo na baadae kumuoa Grace mwaka 2006. Chepkurgor na Grace walisoma wote shule moja.

  "Mke wangu hana tatizo na mimi kuoa mke wa pili" alisema Chepkurgor na kuongeza "Alisikiliza majibu aliyotoa Hillary na wala hakulalamika".

  Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mwanaume anaruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja, kwa hiyo kama posa yake itakubaliwa Chelsea atakuwa mke wa pili Chepkurgor.
   
Loading...