Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Raia wa Kenya asiyekuwa na sifa za ualimu ameajiriwa kuwa Mkuu wa Shule za Kimataifa za St. Columba's jijini Dar es salaam Jamhuri limebaini
Shule hizo zinazomilikiwa na Kanisa la Presbyterian Church of East Africa, lenye Makao Makuu nchini kenya, ziko Upanga na Makongo jijini humu
Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine, imevalia njuga uboreshaji wa Elimu, ikiwa pamoja na kufanya uhakiki wa walimu, jambo ambalo, ama halijatelekezwa, au linafunikwa katika shule za St. Columba's
Uchunguzi uliofanywa na Jamhuri umebaini Mkuu wa Shule hizo zinazotoa elimu ya msingi kwa lugha ya Kingereza, David Wathiga, hana elimu wala sifa za kushika wadhifa huo
Ni kwasababu hiyo, imebainika kuwa alishawahi kufukuzwa asifanye kazi hiyo, lakini akarudi kinyemela kwa msaada wa maafisa wa Idara ya Uhamiaji na wenzao wa Idara ya Kazi wanaohusika na ajira nchini.
"Huyu alikuwa Mwalimu wa kawaida katika Kampasi ya Makongo mwaka 2011, kabla ya kufukuzwa kutokana na uwezo mdogo wa kufundisha masomo ya Sayansi na Hisabati, kila mmoja anashangaa ni vigezo gani vilitumika kumrudisha na kumpa wadhifa wa juu kabisa" kimesema chanzo cha habari
Wakati anatimuliwa, Meneja wa Shule katika Kampasi ya Makongo alikuwa Steven Kabumba, na Katibu wa Bodi ya Shule akiwa ni Vida Mwasalla
Kabla ya kuachishwa, uongozi wa shule ulimtaarifu kwa maandishi kuwa usingeweza kumtafutia kibali kingine cha kuendelea kufanya kazi nchini baada ya kubaini hana uwezo wa kufundisha
Mbali na kuwa na kiwango cha chini katika utendaji, imebainika kuwa Wathiga alisoma katika Chuo cha City & Guilds nchini Kenya ambacho mitihani yake haitambuliwi na Baraza la Mitihani nchini humo (KNEC) chuo hicho kimekuwa hakitambuliwi kitaaluma mahala popote.
Kwa mujibu wa vyeti ambavyo navyo vinavyodaiwa kuwa ni vya kughushi, Wathiga ana Diploma ya Elimu ya Kiroho (Theological Education by Extension)
Chanzo: Gazeti Jamhuri