Mkenya auawa katika maandamano ya CHADEMA Arusha

Jaribu kutumia hata robo ya akili yako hawa waliletwa na CDM

01.jpg
 
Hao ndio chadema, wako tayari kuleta mamluki ili wahahakishe kuwa fujo zinafanyika.


Mamluki unazungumzia akina Mbowe, Slaa, Ndesa..... you name them; waliotoka Dar na kwingine kwenda Arusha kuandamana au huyo Marehemu?

Mwenye akili zake timamu anajua maandamano yalifanywa na watu gani?



 
Hao ndio chadema, wako tayari kuleta mamluki ili wahahakishe kuwa fujo zinafanyika.

On the contrary, hilo ndilo jeshi letu la polisi la kifisadi lisilotumia akili!!! They always unleash their misery to people indiscriminately. Arusha ni mji wa kitalii, presence of people of other nationalities is very common in AR! Unataka kusema hilo nalo hulijui???!! Yaani kufa mkenya mmoja tu ndo una-conclude kwamba CDM wameleta mamluki???? Kama uko hivyo... Basi utakua na akili kama za hao polisi wako!!!!
 
Makamba anahusika na Wakenya!

Tukumbuke wanausalama wev walikuwa wanapiga watu oyo . yawezekana alikuwa anatembea na shughuli zake tu. polisi walikuwa wamepata nafasi ya kubofya traiga siku hiyo na wengine wanaimiss mianja mingi so hawakuwa wanaangalia mtu. just firing bila kujua inampata nani. nguvu hii inatakiwa ilaaniwe vibaya kwani ni kubwa mno na wakey wadai mtu wao.
 
Hivi ndo tunaanza kujua kuwa kumbe polisi hawakuwapiga waandamanaji hata raia wema walipigwa. Mbwaaaa mbwaa
 
Fanya uchunguzi usiropoke tu, ni aibu kwa mwana jamiii kuwa hivyo "think before" kwani risasi zilikuwa na senser ya kuwatambua waandamanaji tu?
thank you very much... cha kuongeza ni kwamba, inawezekana wote waliouwawa hawakuwa kwenye maandamano, waweza kuta ndio ile tabia ya polisi wetu kuua watu tu
 
fanya uchunguzi usiropoke tu, ni aibu kwa mwana jamiii kuwa hivyo "think before" kwani risasi zilikuwa na senser ya kuwatambua waandamanaji tu?

mleta mada yupo sahihi kabisa kuleta hii mada, wala hakuna haja ya ku "think before", kwa hiyo wewe unalionaje hilo la polisi kufyatua fyatua ovyo risasi, kwa mtu yoyote hata kama sio muandamanaji?? Wanaoandamana utawatambua kwa mabango, nyimbo, hamasa, ushawishi na nyuso zao, leo hii mtu yupo pembeni, apigwe risasi, then umwambie great thinker asiropoke?? Bila shaka wewe ndio unayeropoka.
 
Mkenya aliyeuwawa alikuwa anaishi maeneo ya Sakina. Polisi walimpa jina la George Waitara ili kuficha uraia wake mpaka pale viongozi wa chadema walipoenda kuonyeshwa alipokuwa anaishi wakakuta kitambulisho chake chumbani. Hatujui hilo jina RPC alilotangaza la George Waitara alilitoa wapi. Ubalozi wa Kenya umeshajulishwa.

Majeruhi wengi walipigwa risasi za moto uwanjani na maeneo mengine ya mjini. Mtoto wa miaka 14 amepigwa risasi ya paja akiwa maeneo ya stand kuu jogoo house akiuza mtumba. Kuna kijana amepigwa risasi mbili za mguu akiwa karibu na st thomas hospital na kuporwa hela na polisi! Mama Mkwe wa RPC wa zamani wa Arusha ambaye sasa yupo makao makuu anaitwa Hemed na yeye inasemekana amejeruhiwa na bomu au risasi sasa sijui kama alikuwa anaandamana. Ukweli ni kwamba polisi hawakuwa na nia ya kutawanya waandamanaji bali kuwaua waandamanaji. Na je kulikuwa na haja gani ya kupiga mabomu zaidi ya 30 uwanjani kabla ya mkutano?

Inasikitisha pale ambapo wachache wetu tunageuza jamiiforum kijiwe cha kupiga story kutokana na majibu ya mzaha na utani. Nafasi ambayo zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanaikosa kwa kutokuwa na internet au umeme au vocha za kubrowse kwenye simu sisi wengine tunaichezea kwa kutoa majibu ya kitoto.

Watu wamekufa na kuumizwa vibaya hata kama unalaumu CDM basi laumu kwa hoja na siyo kejeli.

Kilichotokea arusha ni ishara ya wapi tunaweza kuishia siku za usoni. Serikali iliyopo madarakani isipoliona hilo na sisi tusipoliongelea itakuja kuwa taabu na sijui kama damu zetu zitakuwa juu yetu pia au vipi.

Tutafute ukweli kwa nguvu zetu zote na tusimamie ukweli na haki daima.
 
Hao ndio chadema, wako tayari kuleta mamluki ili wahahakishe kuwa fujo zinafanyika.
Si vema kuwa na mawazo ya kishabiki pale ambapo tunaona kabisa maisha ya watu yamepotea na yanaweza kupotea.
Ni muhimu kwa watu wote kupinga mauaji kwa vyovyote vile.
Raia yeyote mwema anatakiwa aache ushabiki wa kipuuzi katika jambo kama hili.
Watanzania ni wamoja na siasa hazitakiwi kutugawa kiasi cha kuua wengine.
Watu wenye mawazo ya kushabikia kwa kuwaumiza au kuua wengine hawatakiwi kwenye jamii!
 
Tulikuwa tunasikia tangu zamani kwamba kabla ya kwenda kufanya kazi iwe ya kutuliza ghasia au kupiga wapinzani wa CCM,FFU wanaruhusiwa kuvuta bangi,marijuana,cannabis,ganja! hii ni uthibitisho tosha,they did not act like proffessional law enforcers at all but enraged hooligans! intoxicated with the illegal herb!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom