MKEMIA kutoka ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali, Faustin Malamula atoa Ushahidi kesi ya Madawa(Bangi) inayomkabiri Paul Ikumbi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
MKEMIA kutoka ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali, Faustin Malamula, amedai baada ya kufanya uchunguzi wa kete 43, zizaniwazo kuwa ni bhangi alibaini kwamba ni bhangi ambazo zilikuwa na kemikali ya Tetrahydrocannabinol(THC), ambayo husababisha ulevi usiopoonyeka kirahisi.

Malamula ambaye ni wakala wa maabara ya Serikali, alidai hayo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke, mbele ya Hakimu Mkazi Anna Mpessa, wakati akitoa ushahidi wa kesi ya kukutwa na bhangi, inayomkabili Poul Ikumbi.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Cecilia Mkonongo, shahidi huyo alidai Agosti 20, mwaka jana akiwa maeneo yake ya kazi alifika askari polisi kutoka kituo cha polisi Kilwaroad Jackson akiwa na bahasha angavu ambayo ilikuwa na kete 43 zizaniwazo ni dawa za kulevya.

" Afande Jackson alikuja maeneo yangu ya kazi akiwa na bahasha angavu ikiwa na kete 43 zizaniwayo dawa za kulevya pamoja na bahasha ambayo ilikuwa na barua kutoka kwa Mkuu wa upelelezi Kilwaroad.

Barua hiyo ilikuwa inahitaji uchunguzi kama ni dawa za kulevya na iko na madhara gani kwa mtumiaji," alidai.

Mkemia huyo alidai baada ya kupokea vitu hivyo alisajili kielelezo hicho na kupewa namba kisha alianza kupima sampuli iliyokuwa na uzito wa gramu 22.25 ambapo alichukuwa sampuli ya kila kete moja kwa ajili ya uchunguzi.

Shahidi Malamula, alidai baada ya uchunguzi wa awali na uchunguzi wa kina alibaini ni kwamba ni bhangi ambazo zina kemikali ya THC ambavyo madhara yake ni kuharibikiwa na akiri.

Alidai baada ya kukamilisha uchunguzi wa kina alifunga na kuweka ndani ya bahasha na kuandaa taarifa ya uchunguzi kisha kumpatia polisi taarifa hiyo.

Shahidi huyo baada ya kumaliza kutoa ushahidi huo aliomba mahakama kupokea kielelezo cha dawa hizo za kulevya pamoja na barua ya uchunguzi vipokelewe mahakamani hapo kama kielelezo ambapo vilipokelewa bila pingamizi.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka mshitakiwa inadaiwa alitenda kosa hilo Agosti 15, mwaka jana eneo la Keko Machungwa Dar es Salaam, ambapo alikutwa na majani ya mazao yaliyozuiliwa kisheria ambayo ni bhangi yenye uzito wa gramu 22.25.

Hakimu Anna aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 11, mwaka huu na mshitakiwa yuko nje kwa dhamana.
 
Kwa hiyo mshtakiwa hakupewa nafasi kuuliza maswali
 
Back
Top Bottom