Mkeka unakuja wa kuwaondoa Mawaziri nonsense kwenye Serikali ya Samia

Hii Nonsense nahisi kuna jambo sijaelewa mimi tofauti na hotuba ya waziri.

Kama nilimuelewa waziri ni kwamba tunatakiwa kuagiza sukari kutoka nje ku cover gap la uzalishaji otherwise mwekezaji anaweza kufanya expansion badala ya kuagiza.(Expansion inaweza ku cover shortage ya sasa?)

Pia wazalishaji pekee ndio wenye sifa za kupewa vibali vya kuagiza.
 
Hii nchi Ina viongizi wa ajabu kweli, waziri anaweza toa tamko Hadi unajiuliza kiwango chake cha elimu,naona siku hizi mama gwajima amebadilika Ila nadhani huyu anapaswa kuwa wakwanza kuondolewa, ana matamko Fulani ya kipuuuzi huku akipenda kutumia. Lugha ya isiyo staha.

Huyu mama hafai kuwa katika wizara ya afya, aondoke, labda kama kuna mpango wa kuanzisha wizara ya mizaha na uigizaji hiyo utamfaa.
 
Jamani Prof Mwandosya ni mzee ameshatumikia nchi hii muda mrefu, katika utumishi wake pia kafundisha vijana wengi sana engineers. Sasa kwa nini

Mwandosya alitaka kuuza ATCL na TTCL!

Halima James Mdee aingie kwenye Baraza la mawaziri!
Wala kuuza kampuni siyo dhambi. Kampuni inaweza kuuzwa hata kama bado inatengeneza faida. Duniani kote makampuni huuzwa na kununuliwa. Kama kampuni yako inauzika ina maana ina potentials za kufanya biashara na ndiyo maana inavutia wawekezaji..... Tangaza leo unauza Shirika la Masoko Kariakoo uone ni wawekezaji wangapi makini watajitokeza. Halafu Tangaza unauza Vodacom uone aina ya wawekezaji watakaoonesha nia. Kuuzika kwa kampuni is a sign of confidence
 
Amtoe
*bibi Teko
*Janaury febuary
*aweweso
*Yule bibi wa Afya

samia kama hutojali njoo Umtumbue DC wa ilala na DC wa morogoro hawajui kazi...

ila Yule chocolate mwinyigelo DC wa wilaya ya Tmk wanaume , hafai pia kuna uzi ntautoa nkiwa free juu ya shutuma moja hv
 
Wizara ya kilimo tukiacha unafiki wameshindwa kazi wote wawili,Viwanda na uwekezaji pia kazi wameshindwa .Maana Bei za vitu zimepanda lakini hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa,mfano vifaa vya ujenzi ni msiba mzito kwa Wananchi,pia TAMISEMI Umy anaelemewa na wizara bora amuhamishe hiyo wazara ni ngumu kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata akibadili mawaziri bado watateuliwa wale wale waliowahi kuwa mawaziri yaan kiufupi hakuna jipya.

Kama kuna waziri aliwahi kusema kipindi cha mkapa kuwa ndege ya Rais lazima inunuliwe mtakula hata majani. Cha ajabu ndege yenyewe kumbe mbovu aibu sana.

Mkeka wa mawaziri awamu iliyofuata na yeye akawepo tena yaan tukasahau kabsa huyu alitia hasara taifa kwa upumbavu wake.

Kwahyo hakuna jipya nchi hii, kama kweli tunataka maendeleo ya kweli ni lazima kwanza wananchi tuondoe uoga na kuishia kulalamika mitandaoni.

Pili ni lazima tuache kuchagua viongozi kwa mazoea na ushabiki wa vyama.

tatu tunapaswa tuchague rais mzalendo wa kweli mwenye misimamo na asiyeyumbishwa hovyo hovyo ktk kile anachokiamini.
Nne ni lazima tubadili katiba ili kuruhusu wagombea binafsi ili tuache kuchagua wanasiasa maana ndo wanaotuchelesha kufika tunapopataka.
 
Wa kwanza awe Simbachawene.

Sababu:
Kuruhusu Polisi kufanya kazi kama genge la majambazi kiasi cha wananchi kuona wapo salama zaidi bila ya kuwa na polisi.

Kila mara Rais amekuwa akiwalalamikia Polisi kwa matendo yao hovyo.

Wa pili ni Dotto Biteko

Sababu
Kuendekeza rushwa, kuvuruga mfumo wa ulinzi wa leseni, na kutumia nafasi yake ya uwaziri kuwanufaisha ndugu zake wenye asili ya Rwanda.

Wa tatu ni Kabudi

Sababu
Kushindwa kusimamia uhuru wa mahakama na kuhakikisha mahakama inaendeshwa na watu wenye weledi wa kutosha. Kuiacha mahakama iendelee kuingiliwa na Serikali.
 
Back
Top Bottom