Mke wangu rudi nyumbani hali yangu mbaya

Mr Bean

JF-Expert Member
Mar 17, 2018
206
177
Habari zenu wadau,

Kwa kweli maisha yangu yanapitia katika kipindi kigumu sana sasa hivi. Mke wangu ameondoka nyumbani na hataki mawasiliano na mimi kisa tu mpenzi wangu wa zamani na fitna zake.

Kwa kweli mke wangu, popote pale ulipo naomba ujue tu kuwa mimi najutia sana kwa yote mabaya niliyotenda juu yako. Hakika baada ya wewe kuondoka nyumbani, umeacha pengo kubwa sana na nimepata kujua umuhimu wako.

Hakuna wa kunichemshia chai asubuhi, wa kunipikia chakula mchana, wa kunipokea mizigo pindi nirudipo kutoka kazini jioni, hakuna wa kuniambia pole na kazi, hakuna wa kuongea na mimi nyumbani, nyumba imekua kama gofu.

Naomba urudi nyumbani mke wangu, nimejifunza kutokana na makosa. Nitakupenda na kukuheshimu mpaka mwisho wa maisha yako au yangu.

Siku zote nilikua nakwambia kuwa naogopa kufa, ila leo kwa mara ya kwanza naogopa kukupoteza wewe zaidi kuliko hata ninavyoogopa kufa rudi home waridi langu.

Ni mimi kipenzi chako Mr Bean

MREJESHO:

habari zenu wadau.

kama mjuavyo nyinyi wadau wa JF ni familia yangu, hivyo nimekuja kuwapa mrejesho wa kilichojiri.

Ama kweli usilolijua ni usiku wa giza. leo nimekuja kugundua kumbe huyu mke wangu aliniacha sio kwa sababu alizozisema yeye. alikua tu anatafuta sababu na wiki ilopita aliipata. kumbe kuna jamaa alikua anamdoea mke wangu. yaani sasa hivi jamaa ndo anaishi na mke wangu, nimemfata jamaa kumpa biti na kumtisha aachane na mke wangu.

Kilichotokea ni kwamba jamaa akaenda kunisema kwa aliekua mke wangu, na mke wangu akanifata hewani na kunipa matusi ya nguoni, na kuniambia nisimfatilie.

Kwa kweli imeniuma sana, ila ndio hivyo sina la kufanya.
 
Kama wewe ni mwanaume kweli.. mfate mke wako kwao ukamweleze haya maneno... Kuyaleta huku ambapo inawezekana hayupo kunathibitisha kwamba inawezekana wewe una maisha fulani ya tamthilia hivi za kivenezuela ndo mana akakukimbia
mkuu, mke wangu kakata mawasiliano na mimi. nimeona nijaribu huenda akapita humu JF akaona. sina njia nyingine ya kuwasiliana nae.
 
mpenzi wa zamani uyu ulie lalamika kuwa naweka picha zako status ama

alafu wewe naona unataka kuwa kama gudume mzee wa chai sana
 
Back
Top Bottom