Mke wangu nisamehe, nitadumu nawe mpaka utakaponichoka

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
315
740
Salam Kaka na dada zangu. Leo napenda kushea nanyi ka historia kangu kwa ufupi.

Mimi ni kijana wa miaka 30 sasa. Mwaka 2012 nilipokuwa kijijini kwetu, nilimtongoza binti mmoja hivi wa makamo. Yule binti alikubali, kunipa sex, ila binafsi sikufurahia Sana shoo yake ilikuwa ya kawaida sana. Na lengo langu halikuwa awe wa kudumu, nilitaka anipunguze ashiki tu nilizokuwa nazo kwa wakati huo.

Kadiri siku zilivozidi kwenda binti wawatu alizidi kunipenda zaidi na zaidi. Alitaman sana siku moja tuoane. Nilionesha furaha ya kinafiki katika hili. Wakati huo sikua na kazi wala pesa, lakini binti alinipenda kama nilivokuwa.

Baada ya miezi kama 8 hivi ya mapenzi yetu, binti alinambia kuwa ana ujauzito wangu, niliumia sana lakini hatimaye nikakubaliana na matokeo na niliamua kulea ile mimba.

Mimba ilipokuwa na miezi sita niliondoka kijijini kwasababu nilipata kazi jijini Tanga, ilaa nilikuwa bado namhudumia mama kijacho wangu. Roho ilikuwa inaniuma sana hasa pale ambapo ninapomuona mpenzi wangu huyu akiwa na furaha kutokana na kuwa nami roho ilikuwa inanisuta sana sana.

Nilikuja kurudi kijijin nikamkuta mtoto amezaliwa na ana mwaka mmoja. Namshukuru Mungu mtoto alikuwa ni kopi yangu kila kitu.

KIUKWELI
Roho iliniuma Sana kumkuta mama mtoto wangu akiwa amekonda Sana kutokana na kuniwaza mimi mara kwa mara, KIUKWELI hapo ndo niliyaona mapenzi yake kwangu. Nililia Sana moyoni. Nilitamani kumuacha lakini roho ya kibinaadamu ilinisuta sana, kiukweli nilishindwa kwani hakuwahi kunikosea wala kusikia habari mbaya toka kwake tangu nilipokuwa naye.

Niliamua kupiga moyo konde na kuamua kumuoa ili tule wote maisha kiasi ambacho MUNGU alinijaalia, kwasababu mpaka wakati huo kidogo matunda ya kazi yalianza kuonekana. Alilia Kwa furaha baada ya kuona nimemchumbia rasmi kwa wazazi wake.

KINACHONISIKITISHA
Imefika kipindi sasa limenifika kooni, nilimuonea huruma nikamuoa lakini dhamira inanisuta jamani. Najikuta simpendi kutoka moyoni haswaaa, najikaza lakini wapi, kila nikijikaza lakini wapi.

Suala hili sijawahi kumwambia mtu yeyote hata rafiki zangu hawajui. Moyo ukashindwa kuvumilia siku moja nikaamua kuandika sehemu ili machungu kidogo yapungue moyoni. Daaah, bila kuamini macho yangu, yule mke akaifuma ile nukuu mahali. Daaah niliumia sana ingawa naye aliumia zaidi. Alilia sana nilimuonea huruma lakini kwa sasa amepitezea maisha yanaendelea.

ANANIPENDA SANA LAKINI NAUMIA

NIMEFIKA PABAYA SANA.

1. Siwezi kupiga zaidi ya bao moja (hisia nae sina)
2. Ana wivu nami kupita kiasi. Kiasi cha kufikia kunichubnguza simu zangu na mitandao baadhi ya kijamii. (NAUMIA Sana)
3. Mdomo mrefu (anaongea Sana)

ANANIPENDA SANA LAKINI NAUMIA.

MUNGU ANISAMEHE KWA MAKALA HII MBOVU.


USHAURI TAFADHALI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachokuponza ni huruma zako mkuu. Kati yenu wawili, kwa situation mliyonayo ni lazima mmoja aumie. Either aumie mke kwa kuachwa na kujua hapendwi, au uumie wewe kwa kujifanya unampenda ili asiumie na wakati huohuo unaungua ndani. Hapo pima tu, kati ya ubinafsi na huruma ni kipi kitazidi kingine katika kukupa Faraja na amani ya muda mrefu
 
Huko ndo kunaitwa kupambana na hali yako! Maji umeshayavulia nguo sharti yaoge!!
 
Kinachokuponza ni huruma zako mkuu. Kati yenu wawili, kwa situation mliyonayo ni lazima mmoja aumie. Either aumie mke kwa kuachwa na kujua hapendwi, au uumie wewe kwa kujifanya unampenda ili asiumie na wakati huohuo unaungua ndani. Hapo pima tu, kati ya ubinafsi na huruma ni kipi kitazidi kingine katika kukupa Faraja na amani ya muda mrefu
Mkuu kwani jamaa anasemaje,mana kila nikisoma najikuta narudia mstari ule ule.

Naomba nifupishie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kamama furani kuniumiza sana. Nilitafuta grl mwingine. Huyu alikua bikra, maisha yaliendelea. Baada ya kama miezi miwili nikipata kazi nje kidogo ya mji.

Mala nyingi alinipgia simu alitaka kuja huku..Ila nilisoma (Ni kwasababu niligundua kua mim SIWEZI kupenda tena, nikawa naogopa kapoteza muda wake) najua angekuja na tunge-sex ndio but simpendi kutoka moyoni. Juzi nkampigia simu nikamwambia ukweli tu atafute mtu mwingine apendane naye na ampe zawadi hiyo!

Kashakuzalia mkuu jifunze kumpenda, ukimwacha utakuja kulia

kelphin kepph
 
Kukosa ubinadamu na kutothamini hisia za mwenzio ndio kunakufanya uishi maisha unayoishi sasa. Kama ulijua humpendi tangu mwanzo why umphuck?tena ukamphuck kavu kavu huku ukijua huna malengo nae!!!

Inatakiwa ifike mahali wanaume muache kutupia lawama zote nyege! Kama huna malengo na mtu why usitumie condom ili kuepusha machungu kwa viumbe vitakavyokuja kwa sababu ya nyege zako.

Namuonea huruma huyo dada anayeishi maisha ya uchungu sababu ya upumbavu wa mtu mwingine

#PayThePrice
#Povu
 
Vumilia tu maana ulimpenda mwenyewe.

Ila inabidi umwambie ukweli hasa kwa tabia zake za kukuchunguza.

Pia japokuwa umepoteza hisia kwake but anakupenda kweli kweli aisee!
tapatalk_1579771193470.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom