Mke wangu ni mwalimu, nataka nimtumie kuagiza gari

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,250
1,467
Jamani wadau tunakumbuka kuna makundi maalumu yaliondolewa au kupunguziwa ushuru wa forodha wakiagiza bidhaa nje ya nchi.

Je ule msamaha bado upo kwa waalimu na ni utaratibu gani wa kufuata upate kibali? Msaada jamani nataka kuagiza Escudo(Suzuki).
 
Kama ni MKE wako hautakuwa unamtumia Bali mtakuwa mnanunua gari la familia. Kichwa chako cha habari kinaashiria Kama unataka kuhujumu UCHUMI kwa kukwepa Kodi.
 
Kumbuka nyaraka zote zitaandikwa jina lake ramsmi la kazini kwake,
sasa chonde chonde siku msije mkamwagana tukaonana wabaya.
 
Umiliki utakuwa chini ya mkeo.akitaka "kukuuzia" utalazimika kulipa kodi yote iliyosamehewa,haah haah
 
Hivi huu msamaha wa kodi pale unapoagiza gari kutoka nje,unawahusu wafanyakazi wote wa serikalini? au ni baadhi tu ya makundi wadau.tupeane taarifa rasmi.
 
Wanatoa punguzo la % ngapi la kodi husika?...Au hawalipi kabisaa ushuru wa forodha?
 
Wanatoa punguzo la % ngapi la kodi husika?...Au hawalipi kabisaa ushuru wa forodha?
Wanasamehe import duty pekee, vingine kama VAT na registration na mengineyo unalipa. Ingia kwenye web ya TRA kwa taarifa zaidi. Pia gari husika lisizidi umri wa miaka 8.
 
Wanasamehe import duty pekee, vingine kama VAT na registration na mengineyo unalipa. Ingia kwenye web ya TRA kwa taarifa zaidi. Pia gari husika lisizidi umri wa miaka 8.
Ahsante mkuu
 
Nisaidie ushuru wa forodha kwa gari la 9ml ni km kiasi gani mkuu?
Kwa sasa wana bei elekezi hawajali umenunua kiasi gani nenda kwenye web site ya tra utaona calculator unaingiza aina ya gari na mwaka inakupa kodi halisi utakayolipa.
 
Back
Top Bottom