AbuuMaryam
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 2,536
- 4,513
Mke wangu ni mjamzito wa miezi 10 hivi sasaa...Yaani amepita tarehe yake ya makadirio jana tarehe 29.
Cha ajabu ni yeye kutohisi chochote.Ni juzi tar 27 kama sikosei ndio alianza kutokwa na maji maji meupe ukeni...Kidogo kidogo yakawa yanazidi.Nikamkimbiza hospital. Wakapima njia.Wakaona bado haijafunguka.
Wakamwambia afanye fanye mazoezi...Lakini wapi mpaka leo yupo bado hospital...Maji yanaendelea kutoka..Hakuna chochote kinachomuuma zaidi ya kichwa mara moja moja kinaacha.
Hasikii kichomi wala tumbo kukata wala mgongo wala kiuno...Ni ukeni tu ndio panavuta na maumivu kidogo ...
Ndio amesema yaani panavovuta ukeni ndio kunauma.
Na chooni ndio anaenda mara kwa mara kukojoa.
Manesi walivyopita jana wakampima pima kwa kugusa tumbo lake wakawa wamegusa vitu kama n vichwa viwili pembeni wakadhani ni mapacha...Lakini doctor akaja akagusa vizuri akawaambia sio mapacha mmegusa mbavu labda...Kichwa kipo chini mbona tayari...Bado kutoka tu.
Na mtoto bado mapigo yake ya moyo yanapiga kawaida tu na anacheza kawaida tu sanaaa.
Tatizo langu ni hilo mke wangu haeleweki...Maana yupo sawa tu...Hakuna mengine yanamsumbua kama mjamzito zaidi ya hizo dalili nilizozieleza hapo juu.
Naombeni utaalam wenu ndugu zangu kama kuna madaktar na wataalam wa haya mambo wanitulize akili yangu kwa kunipa nini cha kufanya.
Maana nasikia sijui kuna wanawake wengine wana nyonga ya kiume...Haziwezi zaa kawaida...Sijui wengine nyonga ya mnyama sijui nijuzini nitulize nafsi yangu.
Maana anazidi kukaa hospital tu na mnavyojua hospital chakula ni cha kununua na wanauza gharama utasema kule ni sehemu ya starehe.
Yaani mtu chai ya rangi anauza kikombe 500 kweli na half cake 500 ni upumbavu sana kuruhusu biashara kama hizi mahospital ni dhulma na unyonyaji mkubwa sanaa..