Mke wangu na mama mzazi

akenajo

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
1,634
611
Kuna wakati wanakuwa hawaelewani na kuna wakati wanaelewana ,sasa mimi naumia sana hiki kipindi wasichoelewana,nifanye nini?kama kuna mke asiyeelewana na mama mkwe wake umefanya nini kuiondoa hali hio ili nimpe ushauri mke wangu,tuishi wote kwa amani na upendo?Inaniuma sana,tafadhali nipeni ushauri?
 
mwambie mama you are not her boyfriend anymore...
 
Kuna wakati wanakuwa hawaelewani na kuna wakati wanaelewana ,sasa mimi naumia sana hiki kipindi wasichoelewana,nifanye nini?kama kuna mke asiyeelewana na mama mkwe wake umefanya nini kuiondoa hali hio ili nimpe ushauri mke wangu,tuishi wote kwa amani na upendo?Inaniuma sana,tafadhali nipeni ushauri?
mjengee au mpangishie mama pembeni, kukaa nae hapo .ni shida, wataanza kushindana nani zaidi.
 
mke anakuzidi ubavu na akili
bado hujawa baba wa familia

mama naye anakuzidi akili, bado hujawa baba wa familia.

Fanyia kazi uanamme wako kwanza hasa katika maamuzi ya familia, mitazamo ya kiume na upeo kwa ujumla.
 
kwa uandishi wako napata picha kwamba wote wako chini ya dari moja. sikulaumu manake inawezekana that is the only choice you have keeping them under one roof.

iko hivi wakati wowote ukiona watu wawili hawaelewani jua kuna conflict of interest some where. usiumie kwa maneno yangu makali ila ukweli ni hivi.

mama yako mzazi anakuhitaji wewe kama mwanae mpendwa kwahiyo anataka apewe nafasi ya kusikilizwa, kupendwa, kuheshimiwa, kuthaminiwa na hata kuongea na mwanae. like wise mkeo mpendwa anakuhitaji kwahiyo anataka kupewa muda wa kusikilizwa, kuheshimiwa, kupendwa, kuthaminiwa na hata kuongea na wewe.

ugomvi kati yao husababishwa na nini??? ukichunguza utaona kwamba mke ataoana mama anamsema vibaya ama kumtenda vibaya na upande wa pili ni vivyo hivyo. ila kiukweli ugomvi husababishwa na wivu ambao kila mmoja anao juu ya mwenzie juu yako wewe. haya mengine ya sijui mke hajapika vizuri ama mama kamwambia h/gel apike kitu tofauti ni kiini macho tu, ugomvi ni wewe.

ni ngmu sana kwa mwanadamu kuweza kujigawa kuwatumikia watu wawili kiasi hiki kwani ili uweze kuwaweka sawa lazima uwe na watu wenye utashi wa kuvumiliana. na kwasababu kila mmoja ana kichwa chake na akili yake ni ngumu kujua wanawaza nini.

kwangu mm busara ni hii sema na mkeo kwa lugha ya upendo sana ili ajifunze tu kumvumilia mama, na wewe ue upande wa mkeo ili umtie moyo. mama mweleze juu ya msimamoa wako kwa mkeo in a polite way ila usimwambie maneno magumu. kisha mtie moyo mkeo katika neno lolote gumu analokutana nalo toka kwa mama. najua wamama tulivyo na wake tulivyo, tunapenda hata kama ni kwenye party mimi kama make ndo niseme kama tunaenda sote ama ni mimi na mume tu so lazima uvijue vitu kama hivi.

kama kuna uwezo basi mfanye mkeo mtu muhimu sana kwako ili awe stable na mfanye mama mtu wa heshima sana ili ajue naheshimiwa nijiheshimu.
 
Ongea na mkeo ajaribu kumuheshimu mama mkwe wake, kwangu mimi mamamkwe ni mama. amstahi anapomkera. yawezekana mama akawa mgomvi lakini yeye ajaribu kutoshindana nae as long as haatarishi uhai wake. mkeo akijishusha na kumuona huyo kama mama yake mzazi , huyo mama hata kama ni mgomvi atona aibu ataacha. nawewe mwanaume uonyeshe kabisa hupendi hiyo tabia niabu bana mama mzazi kugombana na mkeo. na mbaya zaidi jamii ishajengeka mamamkwe,mawifi ni matatizo basi mtu hata hajaingia ndani anaanza kujipanga atapambana nao vipi. mbaya sana
 
Tuna tofauti ya mtazamo: Kuna wengine watamlaumu sana mama kwa nini anaingilia/kugombana na mkwewe na kuna wengine wataona ni kumkosea adabu sana Mama kama anagombana na mkwe wake.

Lakini bottom line kinachosaidia ni hekima........hekima namna ya kupunguza misuguano (ni ngumu kumaliza kabisa).

Mama amekulea, pamoja na kwamba umeoa lakini anahisi wewe ni sehemu ya maisha yake na pengine inakuwa ngumu sana kwake kukubali kwamba sasa wewe una kwako na umekua (hili linahitaji maombi kuliondoa) na ni kinamama wachache hustukia hili.

Kwa hiyo huwezi kumdharau kwa sababu ukipata tatizo anaumia......(ni rafiki mwema). Lakini kumbuka kwa sasa wewe upo kwako na ni kiongozi wa nyumba...............tumia busara......Kama ugomvi wao haufiki kwenye kutoana ngeu au kutiliana sumu waache usiwaingilie ila neno lako moja "sitaki umtu amwonee mwenzake na mama nakupenda lakini sipendi ugomvi huu, wewe ni mama yangu na nahitaji busra zako kuliko ugomvi naouona"

Akishindwa kukuelewa kaa kimya. Nimemzungumzia mama pengine ndiye anakuwa mgumu ku-deal naye ila mke yupo chini yako unamjua nje ndani!
 
Kweli sipendi kukaa na mama mkwe kabisa,as long as sipendi ugomvi .kwangu nawakaribisha ila usije a sheria zako nitakufukuza kwa kweli,mimi nakaa na watoto wengi uje uwabague wakati siwabagui nakufukuza, mama mkwe na mwifi sitaki kuwasikia ,sababu lol sitaki ugomvi mie
 
......relax, wanaelewana wakitaka na wanagombana wakitaka, it's none of ur business wala hujaombwa kuingilia "hobby" yao.
 
Kaa nao uwaeleze jinsi unavyoumia pale wanapokuwa hawaelewani. Wape nafasi wote waeleze matatizo yao yanayosababisha kutoelewana. Angalia matatizo hayo yanasababishwa na nini na kama unaweza kuyarekebisha yarekebishe haraka sana la huwezi kufanya hivyo basi waambie kiungwana kwa sauti ya upole kwamba hupendi hali ya kutoelewana kati yao itokee tena.

Usionyeshe upendeleo wa aina yoyote kwa mke au mama hata kama baada ya maelezo yao utaona ni nani mkosaji. Kama kuna mkosaji mwite pembeni mkiwa wawili umueleze anayoyafanya si mazuri na aachane nayo kabisa. Usijaribu kumkemea mkiwa wote watatu unaweza kuharibu ndoa au kumpoteza mama. Kila la heri.

Kuna wakati wanakuwa hawaelewani na kuna wakati wanaelewana ,sasa mimi naumia sana hiki kipindi wasichoelewana,nifanye nini?kama kuna mke asiyeelewana na mama mkwe wake umefanya nini kuiondoa hali hio ili nimpe ushauri mke wangu,tuishi wote kwa amani na upendo?Inaniuma sana,tafadhali nipeni ushauri?
 
gfsonwin naungana na maelezo yako hapo juu. Kwa kuongezea tenga muda kaa na mmoja mmoja na kumuelekeza nafasi yake ndani ya familia ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima. Kitu kizuri ni kuwa kuna muda fulani hao mtu na mkwewe huwa marafiki kitu kinachoonyesha kuwa huenda ni tatizo dogo sana linalowatibua. Nyumba nzingine huwa ugomvi mwanzo mwisho. Jaribu pia kuchimba kiini cha tatizo kwa lengo la kutatua.

The best solution ya hilo tatizo ni kuwatenganisha kama uwezekano huo upo. Ila kama haupo waweza kufuata ushauri hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Kweli sipendi kukaa na mama mkwe kabisa,as long as sipendi ugomvi .kwangu nawakaribisha ila usije a sheria zako nitakufukuza kwa kweli,mimi nakaa na watoto wengi uje uwabague wakati siwabagui nakufukuza, mama mkwe na mwifi sitaki kuwasikia ,sababu lol sitaki ugomvi mie

we utakua mtata sana...mbona mama wa mwanamke akija nyumbani wanaume huwa hatuna shida nao?
 
Thread kama hii ilishawahi kuwapo hapa jamvini, na narudia ushauri nilioutoa wakati huo.
Binafsi ningetafuta zangu safari kama ya mwezi hivi, ningewaacha mke na mkwewe hapo nyumbani kwa muda wote huo, halafu simu zangu zote walizozizoea ningezima.
Sasa kama wao wote ni mafahali basi na wakae zizi moja.
 
Simple.

Chochote kizuri unachomfanyia mama yako usifanye wewe, kipitishie kwa mkeo afanya. Awe busy naye kumfanyia vitu vidogo vidogo apendavyo, vizawadi, kumsifu nk. Atalainika na atashift upendo toka kwako kuja kwake. Kila wakati mweleze mama yako Jinsi Mke wako anavyomjali yaani anavyomjali mama na kupenda.

Mama akikuomba chochote mwelezea hamana tabu mama nitamwomba wife atakupa.

nafahami mbinu hii imefanya kazi kwa several couples including wale ambao initially wazazi wa mume hawakumtaka mke na walisusia hata harusi lakini sasa ni mabest kuliko mtoto wao wa kiume.
 
we utakua mtata sana...mbona mama wa mwanamke akija nyumbani wanaume huwa hatuna shida nao?
watu8 mimi sio mtata ila hata biblia inasema jicho lako likikukosesha bora ulikate sipendi mazingira ya mtu kunifnya nigombane nae as long as niliadithiwa alimtesa sana mke wa mtoto wake wakwanza lol sitamani kabisa aje kukaa kwangu maana kma ni mgomvi atanikwaza na kugombana n binadamu mie siwezi huwa inanicost sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
Simple.

Chochote kizuri unachomfanyia mama yako usifanye wewe, kipitishie kwa mkeo afanya. Awe busy naye kumfanyia vitu vidogo vidogo apendavyo, vizawadi, kumsifu nk. Atalainika na atashift upendo toka kwako kuja kwake. Kila wakati mweleze mama yako Jinsi Mke wako anavyomjali yaani anavyomjali mama na kupenda.

Mama akikuomba chochote mwelezea hamana tabu mama nitamwomba wife atakupa.

nafahami mbinu hii imefanya kazi kwa several couples including wale ambao initially wazazi wa mume hawakumtaka mke na walisusia hata harusi lakini sasa ni mabest kuliko mtoto wao wa kiume.

fuata huu ushauri ni mzuri..ikishindikana watenganishe mpeleke mama yako akaishi kwa watoto wake wa kike kama anao na wewe utume matumizi huko, sio lazima kuishi nae..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom