Mke wangu kuitwa Demu mbele yangu, nimejiuliza mengi

SOCIETY'S FOCUS

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
424
490
Ilikuwa jana mida ya saa tisa Alasiri kwenye mishemishe za kutafuta mahitaji ya wiki, nikiwa na mama wa watoto wangu baada ya kutoka Kanisani tukaona tupitie mjini kutafuta mawili matatu kwa ajili ya matumizi ya familia yetu. Ghafla walitokea vijana watatu waliokuwa wakipiga story huku wakicheka sana, baada ya kutuona walinyamza wote ghafla kama sekunde kadhaa kisha mmoja wao alitamka maneno haya "JAMAA ANA DEMU MKALI".

Binafsi hiyo kauli sikuipenda, sijui kwa upande wa mke maana hakuna aliyezungumzia hilo swala mpaka sasa, japo wote tulisikia. Sasa ndugu zangu Wanababa kwa Wanamama wote wa jukwaa hili, unajisikiaje Mke wako kuitwa demu mbele yako? au we Mwanamama kuitwa demu mbele ya mume wako?

Karibuni sana wandugu
 
Nawaunga mkono hao machalii, ulitakiwa kuita na kuwapatia mwekundu kwa kusifia my wife wako, na hiyo inauonyesha kuwa unamke mzuri kwa sura ingawa tabia yake walikuwa haijui. Binfsi napenda nikipita na mke wangu watu waugue shingo, miye sikuoa mwanamke asiyetizamika. Hata kuomba watu waombe tu, lakini wasipewe, maana wakipewa halafu nikafahamu, bado sijafikiria hatua nitakayochukua.
 
mi sioni shida iko wapi...kama kajaaliwa kajaaliwa tu acha watu waseme...elewa tu kuwa kila watu na aina zao za lugha wanazotumia so take it easy wala usimaind shukuru tu kuwa mkeo ni "mkali"
 
Sasa neno demu maana yake si ni jinsia ya kike hizo ni lugha za mitaani,huwezi kuwalazimisha watu waongee unavyotaka wewe ni kiasi cha kupotezea tu mimi sijaona tatizo hapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom