SOCIETY'S FOCUS
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 424
- 490
Ilikuwa jana mida ya saa tisa Alasiri kwenye mishemishe za kutafuta mahitaji ya wiki, nikiwa na mama wa watoto wangu baada ya kutoka Kanisani tukaona tupitie mjini kutafuta mawili matatu kwa ajili ya matumizi ya familia yetu. Ghafla walitokea vijana watatu waliokuwa wakipiga story huku wakicheka sana, baada ya kutuona walinyamza wote ghafla kama sekunde kadhaa kisha mmoja wao alitamka maneno haya "JAMAA ANA DEMU MKALI".
Binafsi hiyo kauli sikuipenda, sijui kwa upande wa mke maana hakuna aliyezungumzia hilo swala mpaka sasa, japo wote tulisikia. Sasa ndugu zangu Wanababa kwa Wanamama wote wa jukwaa hili, unajisikiaje Mke wako kuitwa demu mbele yako? au we Mwanamama kuitwa demu mbele ya mume wako?
Karibuni sana wandugu