Mke wangu kanunua kiwanja bila kunishirikisha na anataka kuanza kujenga

mmakondehuru

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
385
149
Habari wanajamvi,

Maneno yafuatayo nimetamkiwa na Mke wangu usiku wa Leo,

"Nimenunua Kiwanja na nataka kuanza ujenzi, ukiona inafaa waweza kunishauri"

Haya yanasemwa ikumbukwe sisi wenyewe hatuna nyumba ya kuishi.

Maswali:
Ni vizuri yeye aanze ujenzi wa kwake wakati hatuna pa kuishi na tuna watoto 2? Kwanini anunue kiwanja bila kunishirikisha?

Naomba ushauri wenu tafadhari
 
Ni sawa tu
Nawe act kama haufahamu ikiwa hamjliongelea.

Wanaume nyie ndio mmefanya wanawake wengi wacheze huu mchezo.. unabahati umejua mapema. Siri zetu za maendeleo tamu kweli kweli.. mpende zaidi mkeo ni yenu pamoja ila yeye ni bosi.. mmmh % fulani pia ipo ni roho mbaya tho esp ikiwa na ya uke wenza ndani

Wanawake oyeeeeee
 
Ni sawa tu
Nawe act kama haufahamu ikiwa hamjliongelea.

Wanaume nyie ndio mmefanya wanawake wengi wacheze huu mchezo.. unabahati umejua mapema. Siri zetu za maendeleo tamu kweli kweli.. mpende zaidi mkeo ni yenu pamoja ila yeye ni bosi.. mmmh % fulani pia ipo ni roho mbaya tho esp ikiwa na ya uke wenza ndani

Wanawake oyeeeeee


Hebu funguka zaidi .
 
Au inawezekana kanunuliwa na mchepuko kwa hiyo kaona hakikuhusu kinamuhusu yeye na mume mwenzio ndio maana hujashirikishwa mkuu...
 
Habar
Wanajamvi, maneno yafuatayo nimetamkiwa na Mke wangu usiku wa Leo,

"Nimenunua Kiwanja,na nataka kuanza ujenzi,ukiona inafaa waweza kunishauri"
Haya yananasemwa ikumbukwe sisi wenyewe hatuna nyumba ya kuishi ,

swali : ni vzur yeye aanze ujenzi wa kwake wakati hatuna pa kuishi na tuna watoto 2? Kwann anunue Kiwanja bila kunishirikisha? Naomba ushauri wenu tafadhari
Alishakuona wewe Poyoyo na ndiyo maana kakwambia Ukiona inafaa unaweza kumshauri au ukaka kimya kwa kuwa hautabadilisha chochote kwake......

Yaani wewe ni poyopoyo toka mumekuwa naye hajawahi kusikia neno lolote la maana kutoka kwako la kimaendelea kwa hiyo akikuendekeza utarudisha nyuma..Pia tambua kuwa kila mtu na kipaumbele chake kama wewe kipaumbele ni Magari yeye anaweza ona kipaumbele niNyumba kwa hiyo alishakuona wewe
 
hahahah pole ila unajua sometimes wanawake ndo wanaumiaga zaidi kwenye maswala Ayo alafu akikuangalia huna hata plan unaondoka asubuh unarud jioni huwazi chochote acha ajiongeze msaport 100%
 
Nimependa hapa "ukiona inafaa, waweza kunishauri".

Kuna tatizo kubwa ndani. Angalia ulipojikwaa dude, sio ulipoangukia.
 
Back
Top Bottom