Mke wangu kajikuta FBI kwa bahati mbaya

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,466
8,281
Ilikua ni siku tulivu tu Kama siku nyingine, basi shetani nae alikua kazini Kama kawaida yake.

Kifupi mke wangu huyu hana tabia kabisa ya kushika simu yangu hadi majuzi alipo ingiwa na tamaa za kutaka kujua Kama yaliyomo yamo.

Basi ni siku moja nyuma yake nilikua nimefanya muamala wa pesa kwa mwanadada Beatrice kulipia bidhaa alio niuzia. Baada ya kulipia nikamtumia text kumuuliza Kama kapata? Akanijibu ndio nimepata Asante. Nami nikamjibu Asante pia kwa kunivumilia Basi maongezi yakawa yameishia hapo na huyu Beatrice.

Basi hiyo siku nipo zangu bafuni naoga nasikia wife anabamiza bamiza milango mala atoke mala aingie ile kumaliza kuoga natoka namkuta mtu amefura hatari Mara ashike hichi aache, ashike hichi aache akaenda kushukua dekio kalileta ndani akaacha akachukua mswaki akatoka nje , akarudi kumbe kasau kuweka dawa akarudi akaweka dawa akaanza kupangalua mabegi Kama Kuna kitu anakitafuta hivi aah mimi kuoana hivyo nikamuuliza kulikoni mbona hivyo nikajibiwa kamuulize Beatrice. Nikaanza kujiuliza kwani Beatrice kafanya Nini? Mtoto wa watu akaangua kilio hatari huku akisema yaani tunafuta hela kwa shida hivi halafu wewe unahonga kirahisi hivyo. Na kwa unaomba na samahani kabisa kwa kumcheleweshea .

Kufikia hapo nikakosa sababu ya kuendelea kuongea nae na kubaki tu nacheka maana hata sijui pa kuanzia kumuelewesha kwa sababu hata simu yangu nilisha kataza kuushika , anacho nifikiria kufanya sijafanya. Na kiukweli Mimi Bwana kujieleza sipendi hasa kwa kiumbe wa kike. Na Mambo hayapo sawa Hadi leo Moto umewaka mtu Hana amani kabisa, yaani nisifanye chochote naambiwa Beatrice kwa hiyo humu ndani wimbo ni Beatrice. Aman huyu Dada angejua jina lake limeleta balaa kwenye familia yangu sijui angejisikiaje Dada wa watu. Sijui angeacha hii kazi yake ya kuuza bidhaa zake kwa mkopo na kutumiwa hela kwa simu sijui.

Sijui nimfokee huyu wife kwa Nini alishika simu? Sijui nikae chini nianze kumueleza Hali ilivyo hapa naona uvivu na akili inachoka kabisa.Yaani ni lawama tu kuwa aliniamini Sana na hakujua Kama Kuna siku nitamfanyia hayaa. Na hata nikimuelezea ataona Kama nampanga tu cos majibu tayari anayo.

Nimesha amua bana liwalo na liwe. Wacha Moto uwake ukimaliza utazima wenyewe.

NB
......... wanawake achaneni na simu za wanaume wenu .......
 
Samahani mkuu....
Hivi kwanini haukuja kwenye kule kikao cha wanaume hapa ndani..??
Ila minashangaa sana aiseee...🤨
278693446_1015367842747258_1580398510776258097_n.jpg
 
Ilikua ni siku tulivu tu Kama siku nyingine.basi shetani nae alikua kazini Kama kawaida yake.

Kifupi mke wangu huyu hana tabia kabisa ya kushika simu yangu hadi majuzi alipo ingiwa na tamaa za kutaka kujua Kama yaliyomo yamo.
We mweleze mapema aelewe kabla hajaenda kupooza 'machungu' kwa baharia aliyewahi kumuomba akamkatalia🙄
 
Huyo sio mwanamke wa kuowa mpige na mwichi kichwani ili azimie ...akizinduka mmwagie maji ya baridi...halafu andika taraka tatu mpatie aende kwao..na usijaribu kabisa kumpa nauri,
Ni mwanamke ambaye tayari nipo nae kwenye ndoa mkuu. Hapa nimekaa pembeni kwanza kuona shetani anachezaje hii ngoma
 
Kaa naye, ongea naye. Mweleweshe hali halisi. Huyo mwanamke anaonekana anakupenda mkuu. Angalia usije ukapuuzia hili, maana wanawake wengi wana asili ya vinyongo na kulipa kisasi, hasa akikupenda kwa dhati. Utakuja kupigwa matukio wewe endelea kumpuuzia tu na kumuacha na maumivu.
Na pia ishu kama hii bora ungeiua kibingwa mwenyewe kuliko kuileta hapa mkuu ni minor case.
 
We fanya sehemu yako sio kujijibu et ana majibu tayar, we mweleweshe na ushahidi wote mpe, asipo elewa sasa hyo n case nyingine, Ila wewe unakua umeshafanya unacho paswa kufanya

Ila kukaa kimya means unamuonyesha ubabe yaan you don't care liwalo na liwe, sasa hayo sio mapenzi.

Chukua jukumu Mzee mpe amani, n mkeo.
 
Mbona nongwa!???
Kwani kumueleza kilichotokea kuna shida gani? Mbona mnapenda kesi na ugomvi? Wewe ichukulie kama fursa ya kujifunza kwamba mkeo sometimes (wanawake wengi) huwa anakuchunguza, kuwa mwangalifu na weka masuala yako sawa na maisha yaendelee.
 
Mueleweshe tu ataelewa ila unavyoendelea kukaa kimya na kumuignore ndo unazidi kumzidishia kinyongo, na kama ni mtu wa visasi ataanza kuwafikiria watu wengne wanaomtaka! Just be humble mueleweshe m bembeleze vizuri atakaa sawa.
 
Kaa naye, ongea naye. Mweleweshe hali halisi. Huyo mwanamke anaonekana anakupenda mkuu. Angalia usije ukapuuzia hili, maana wanawake wengi wana asili ya vinyongo na kulipa kisasi, hasa akikupenda kwa dhati. Utakuja kupigwa matukio wewe endelea kumpuuzia tu na kumuacha na maumivu.
Na pia ishu kama hii bora ungeiua kibingwa mwenyewe kuliko kuileta hapa mkuu ni minor case.
Ngoja nione Kama yaliyopo yapo
 
We fanya sehemu yako sio kujijibu et ana majibu tayar, we mweleweshe na ushahidi wote mpe, asipo elewa sasa hyo n case nyingine, Ila wewe unakua umeshafanya unacho paswa kufanya

Ila kukaa kimya means unamuonyesha ubabe yaan you don't care liwalo na liwe, sasa hayo sio mapenzi.

Chukua jukumu Mzee mpe amani, n mkeo.
Sawa ngoja nijaribu
 
Mbona nongwa!???
Kwani kumueleza kilichotokea kuna shida gani? Mbona mnapenda kesi na ugomvi? Wewe ichukulie kama fursa ya kujifunza kwamba mkeo sometimes (wanawake wengi) huwa anakuchunguza, kuwa mwangalifu na weka masuala yako sawa na maisha yaendelee.
Mimi hapa najiuliza tu alikua anatafuta Nini kwenye simu yangu....? Mbona ndoa ilikua na Aman tele na sijawahi muonesha hata kumrharau hata siku moja .

Hivi kama mtu anakupenda na ameshakuoa unaendelea kuchunguza Nini...? Yaani alisahau Nini kunichunguza wakati wa uchumba Hadi aje anichunguze ndoani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom