NajuaKusoma
Member
- May 8, 2017
- 81
- 60
Ndugu wadau,
Hasa nyie mliopo katika ndoa naombeni mniambie hili huwa mnalitibu/mnalisovu vipi?
Mimi ni mjasiriamali na nina ndoa huu mwaka wa pili na nusu, mke wangu yeye ni mwalimu S/m na kwao ni Moshi ila mimi wa mkoani huku ziwani (nilimkuta keshazaa watoto wawili na kwa sasa kazaa 1na mimi). Nilikutana nae miaka kadhaa huko nyuma tukaishi kama wapenzi takribani miezi 8 na nilijiridhisha anafaa kuwa mke bora haswaa! Hatimaye tulifunga ndoa ya kidini.
Sasa katika familia ya wazazi wangu kukatokea mtafaruku wao na mama yangu mzazi akaachia ngazi na mji ukabakia mikononi mwa mke wa pili wa baba yangu. Mimi katika pita pita zangu nikapewa Hiace kama mtaji wangu na nikachukua mkopo katika Benk flani na skuweza kuurejesha ila mke wangu akaomba mkopo wa kazini kwake (5m) akanisevu na maisha yakasonga.
Hatimaye Mungu akanibariki riziki kubwa kubwa mwaka wa kwanza ndoani nikanunua kigari cha familia nikawa nampeleka na shuleni kwake, nikajenga katikati ya nchi na huku mkoani kwetu japo bado nmepanga. Nikaona mama yangu aje aishi nami ili aanze kuona matunda ya mwanae ale mboga saba na hapo ndio kasheshe limeanza.
Visa na vitimbi vimekuwa vingi na nina dada yangu kamaliza 6 na mke anaonesha kabisa wasifike kwangu na hata mama yangu hasalimiwi vizuri. Kiufupi anataka nifanye maamuzi magumu niclash ndugu wasiwepo ili tuishi kwa amani nae na huyo mke hana miaka hata 4 kazini na kwao maskini wa kutupa.
Leo anajitangaza mali (duka nyumba gari) ni vyake nikimuacha au akitaka tuachane bas tugawe kwa kua aliniokoa katika deni la benk. Naombeni ushauri wenu; je nimuongezee mke wa pili; nifukuze ndugu hasa mama; au bora niachane nae?
Karibuni kwa mawazo tofauti wadau; lolote sema.