Mke wangu hasapoti juhudi zangu. Ananikatisha tamaa sana

Hawa ndo wanawake wetu aisee
Screenshot_20200809-214334.jpeg
 
Sikuwa najua,

Kumbe kuwa na mwenza ambaye hasapoti juhudi zako za maendeleo INABOA SANA WAUNGWANA. Kitu ambacho sikua najua kumbe mke wako pia anaweza kukuonea wivu na kukudhuri kwa husda /kijicho /roho mbaya. Nimejiskia vibaya leo baada ya kumueleza kwa bashasha mke wangu WAZO langu zuuri hatimae kunilaumu na kuninunia.

Aisee! Nikamuuliza 'Sasa we unaona tufanyeje hapa?' hakuwa na jibu m badala wala suluhu yoyote. Wosia wake ni kuachana na ishu yangu na kujikalia tuuu.

Wito.
Mke/mume wako anaweza akawa kikwazo cha maisha na mafanikio yako. Najua mtapenda kujua ishu yenyewe, lakini naomba mniwie radhi kwa kutoiweka wazi.

Sasa kwa staili hii tutafikia uchumi mkubwa kweli?
Mpuuze, pambana kivyako
 
Back
Top Bottom