Mke wangu hasapoti juhudi zangu. Ananikatisha tamaa sana

Behind the camera

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
315
740
Sikuwa najua,

Kumbe kuwa na mwenza ambaye hasapoti juhudi zako za maendeleo INABOA SANA WAUNGWANA. Kitu ambacho sikua najua kumbe mke wako pia anaweza kukuonea wivu na kukudhuri kwa husda /kijicho /roho mbaya. Nimejiskia vibaya leo baada ya kumueleza kwa bashasha mke wangu WAZO langu zuuri hatimae kunilaumu na kuninunia.

Aisee! Nikamuuliza 'Sasa we unaona tufanyeje hapa?' hakuwa na jibu m badala wala suluhu yoyote. Wosia wake ni kuachana na ishu yangu na kujikalia tuuu.

Wito.
Mke/mume wako anaweza akawa kikwazo cha maisha na mafanikio yako. Najua mtapenda kujua ishu yenyewe, lakini naomba mniwie radhi kwa kutoiweka wazi.

Sasa kwa staili hii tutafikia uchumi mkubwa kweli?
 
Vitu muhimu:

- Mke ana haki ya kuwa na Mawazo tofauti na yako, sio lazima a Support kila kitu.
- Hata sipo Support hakikisha unakiendea kwa utulivu bila kumnyanyasa.
- Hakikisha anapata maitaji yake yote ya Muhimu na ukishaoa ujue hauishi kisela tena huwezi amua tu kuparamia vitu.
 
Bora huyo amekuonesha mapema.. Yakupasa kufanya mambo yako kimyakimya pasipo kumshirikisha..

Wakat mwingne unatakiwa ufanye mambo kama kichwa cha familia haya mambo ya kuwashirikisha baadhi ya wanawake ambao hawajiewi inakuwa ni ujinga.

Fanya mambo kwa faida ya familia yako hawa wanawake wakati mwingne ndio chanzo cha sisi wanaume kuchomoka kwenye reli
 
Tena akiwa goli keeper aisee, ukitaka kumuonya juu ya tabia mbaya uliyoiona kwake kwa nia njema... hujibu kwa hasira "sina shida na hela zako"
 
Vitu muhimu:

- Mke ana haki ya kuwa na Mawazo tofauti na yako, sio lazima a Support kila kitu.
- Hata sipo Support hakikisha unakiendea kwa utulivu bila kumnyanyasa.
- Hakikisha anapata maitaji yake yote ya Muhimu na ukishaoa ujue hauishi kisela tena huwezi amua tu kuparamia vitu.
Amen
 
Bora huyo amekuonesha mapema.. Yakupasa kufanya mambo yako kimyakimya pasipo kumshirikisha..

Wakat mwingne unatakiwa ufanye mambo kama kichwa cha familia haya mambo ya kuwashirikisha baadhi ya wanawake ambao hawajiewi inakuwa ni ujinga.

Fanya mambo kwa faida ya familia yako hawa wanawake wakati mwingne ndio chanzo cha sisi wanaume kuchomoka kwenye reli
Nikweli
 
Wanasema kila penye mafanikio ya mwanaume basi nyuma yake kasimama mwanamke shupavu, sasa kwa kuwa unayemwita mkeo hakusupport basi yumkini si mkeo huyo na alistahili kuwa mke wa mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom