Mke wangu hapendi niwasaidie wazazi wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wangu hapendi niwasaidie wazazi wangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lukunij, Jul 9, 2012.

 1. lukunij

  lukunij Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninaishi katika ndoa sasa mwaka wa tatu nimejaliwa kuwa na mtoto mmoja kinachonishangaza mke wangu amebadilika sana ,kimapato hali yangu si mzuri ukilinganisha na awali ,kila siku kugombana tu ndani ya nyumba na hata heshima imepungua tunajibizana kila kukicha sasa kitu kichonitisha ni pale aliponuna eti kwa sababu nimemsaidia baba yangu pesa na baba aliwahikunisaidia kama laki 5 cku chache zilizopita,sasa na yeye anashida ya pesa nimempa sh laki 6 mkewangu amenuna na kusema ninamsaidia tu baba yangu na wazazi wake siwajali,je munanisaidia vip kiushauri kweli bado ananipenda au?
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  anakupenda sana tu..
  tatizo ana roho mbaya...muombee
   
 3. C

  CAY JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mweleze hao ni wazazi,mnatakiwa kuwatunza.Ila sasa siyo wa upande mmoja tu.Iwe pande zote
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye bold, Inawezekana hamshirikishani vya kutosha kwenye mahusiano yenu. Maana kama baba yako aliwahi kukusaidia wakati wa shida na yeye akapata shida, logically mkeo asingeweza kununa kwa wewe kumsaidia baba yako unless uwe hukumshirikisha mkeo kuhusu huo msaada.

  Ukiwa na familia ni bora kuenenda kwa hekima kwa balance misaada na mawasiliano baina ya hizo koo mbili. Ni vizuri ukae na mkeo na kupanga nini cha kufanya na kuwa na kauli ya pamoja na kufanya mambo kama familia kuliko kila mtu kujifanyia anachojisikia.

  Pia usiwe na inferiority complex kuwa mkeo kabadilika kutokana na kipato, inawezekana ni mambo madogo tu ya kukaa chini na kuongea na kuyamaliza. Hebu jaribu kumuita jioni ya leo uongee naye kuhusiana na mambo ya kifamilia na jaribu kumshirikisha kwenye mipango kadhaa na matumizi ya fedha uone reaction yake. Angalizo: Ongea naye kwa hekima!
   
 5. d

  drlaxx Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angalia hiyo mistari rd. hilo ndo tatizo. wakati unamuoa ulimwonyesha unazo. sasa umefulia unaakuwa na inferiority complex. hata akikuambia ukweli unaona kabadilika.sio yeye tu kilakitu kimebadilika. be a man and face reality.
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Ana roho mbaya huyo! Na usiache kuwasaidia wazazi wako!

  Kama ana kupenda kweli kwa nini ana chukia ukiwasaidia wazazi wako?

  Muombe mungu sana abadilike!
   
Loading...