Mke wangu anawafundisha watoto dini yake kwa siri, kinyume na amri yangu

navin-govind

Member
Apr 10, 2015
72
117
Kuna mgogoro wa kimaslahi kati yangu na mke juu ya mwelekeo wa kiimani wa watoto wetu, hii ni kutokana na sisi wazazi kuwa na dini tofauti

Wakati mwingine watoto hawa huudhuria ibada kwenye dini ya mke wangu na wakati mwingine kwangu na wameanza kuchanganyikiwa kiimani kutokana na hali hii ambapo juzi wameniuliza "baba sisi ni dini gani, mwalimu huwa anauliza shule tunashindwa kujibu.

Huko nyuma nilitoa mwongozo kwa mke kuwa watoto waabudu kwa imani yangu lakini wakati mm sipo amekua akienda kinyume na agizo hilo, akiwaambia kuwa mkiulizwa na baba msiseme huwa nawafundisha imani yangu.Juzi nimegundua siri.hiyo kuwa agizo limekiukwa muda tu, nikamuita mke wangu na kumueleza kwa ukali

Ambapo akageuka mbogo na kuanza kulia kuwa kwa nn nawapangia watoto pa kwenda kuabudu, jambo ambalo si kweli maana wale watoto bado ni wadogo hivyo wanahitaji muongozo hawawezi kujiamulia.

Sasa juzi nimetoa amri mpya kwamba nikisikia tena jambo.hili namtimua kurudi kwao na kuleta mwanamke wa dini yangu tuweze kulea watoto kwa mujibu wa dini yangu

Wadau nitakua nimekosea kwa hili? Au kuna ufumbuzi mwingine hapo?
 
Kuna mgogoro wa kimaslahi kati yangu na wife juu ya mwelekeo wa kiimani wa watoto wetu, hii ni kutokana na sisi wazazi kuwa na dini tofauti

Wakati mwingine watoto hawa huudhuria ibada kwenye dini ya wife na wakati mwingine kwangu, na wameanza kuchanganyikiwa kiimani kutokana na hali hii ambapo juzi wameniuliza ""baba sisi ni dini gani, mwalimu huwa anauliza shule tunashindwa kujibu

Huko nyuma nilitoa mwongozo kwa wife kuwa watoto waabudu kwa imani yangu lakini wakati mm sipo amekua akienda kinyume na agizo hilo, akiwaambia kuwa mkiulizwa na baba msiseme huwa nawafundisha imani yangu
Juzi nimegundua siri.hiyo kuwa agizo limekiukwa muda tu, nikamuita wife na kumueleza kwa ukali

Ambapo akageuka mbogo na kuanza kulia kuwa kwa nn nawapangia watoto pa kwenda kuabudu, jambo ambalo si kweli maana wale watoto bado ni wadogo hivyo wanahitaji muongozo hawawezi kujiamulia

Ulibugu kuanzia uchumba ulishindwa kumshawishi mkeo kuwa dini yako hakika watoto ndio watakao chagua kwenda kwa baba au mama
 
Kuna mgogoro wa kimaslahi kati yangu na wife juu ya mwelekeo wa kiimani wa watoto wetu, hii ni kutokana na sisi wazazi kuwa na dini tofauti

Wakati mwingine watoto hawa huudhuria ibada kwenye dini ya wife na wakati mwingine kwangu, na wameanza kuchanganyikiwa kiimani kutokana na hali hii ambapo juzi wameniuliza ""baba sisi ni dini gani, mwalimu huwa anauliza shule tunashindwa kujibu

Huko nyuma nilitoa mwongozo kwa wife kuwa watoto waabudu kwa imani yangu lakini wakati mm sipo amekua akienda kinyume na agizo hilo, akiwaambia kuwa mkiulizwa na baba msiseme huwa nawafundisha imani yangu
Juzi nimegundua siri.hiyo kuwa agizo limekiukwa muda tu, nikamuita wife na kumueleza kwa ukali

Ambapo akageuka mbogo na kuanza kulia kuwa kwa nn nawapangia watoto pa kwenda kuabudu, jambo ambalo si kweli maana wale watoto bado ni wadogo hivyo wanahitaji muongozo hawawezi kujiamulia

Sasa juzi nimetoa amri mpya kwamba nikisikia tena jambo.hili namtimua kurudi kwao na kuleta mwanamke wa dini yangu tuweze kulea watoto kwa mujibu wa dini yangu

Wadau nitakua nimekosea kwa hili? Au kuna ufumbuzi mwingine hapo?
Kwani wakati unatafuta mchumba, wanawake wa dini zako hawakuwepo? Kama uliamua kuchukua wa iman tofauti, vumiliatu kwani kila muwamba ngoma huvutia kwake.
 
Pole sana mkuu.
Naona mngekaa chini upya mlijadili suala hili, usimtimue. Maana ukioa mwingine utakuwa umesolve temporary problem by creating a permanent problem.
Mtoto kulelewa na mama wa kambo wakati mama yake mzazi yu hai, ina madhara kwa mtoto kisaikolojia.
Vilevile ulipaswa kuliangalia hili kabla ya kuoa.
NAWASILISHA.
 
kwanza kosa ni kuamini kuwa wewe unasauti kuliko mkeo na ndio upuuzi wa Sisi wanaume. Kila mtu ana uhuru wa kumfanya mtoto aamini kipi ni sahihi na kipi si sahihi...kuwakataza watoto wasifuate kile usichokiamini wewe ni Upuuzi na Ujinga... Wewe wafundishe na yeye awafundishe then watakapo kua watu wazima watajua ni wapi waelekee
 
Acha kutumia mabavu huko ni kukosa maarifa na usilazimishe watoto wafuate dini yako.

Kubaliana na ukweli kwamba watoto watafuata dini ya mama yao kwasababu ndie muda mwingi wako nae.
 
Mkuu jinsi nilivyoyaelewa maelezo yako, nimegundua mkeo kuna vitu vingi sana anakuficha au kukuzunguka,hiyo kulia wala usiogope mkuu ni defensive mechanism tu hana/hamna lolote.

Kingine mkuu,trust me ile 49% ya mkemia mkuu wa serikali inakuhusu sana tu.
 
Yan japo hukutaja dini yako wala ya mke wako ila kimtazamo unaonekana wewe ni mkristo na mke ni muislam...
 
Mkuu jinsi nilivyoyaelewa maelezo yako, nimegundua mkeo kuna vitu vingi sana anakuficha au kukuzunguka,hiyo kulia wala usiogope mkuu ni defensive mechanism tu hana/hamna lolote.

Kingine mkuu,trust me ile 49% ya mkemia mkuu wa serikali inakuhusu sana tu.

usitake kuvunja ndoa za watu... Mkemia amesemea waliowahi kwenda kufanya vipimo
 
mnaonaga mkitupigia kelele ndo tunawaelewa eti?
unaweza ukamtimua halafu utashangaa hao watoto watakapokua na kuwa na maamuzi binafsi wanakwenda ulipowakataza.

Mkwe siku si nyingi nakuletea posa ya binti yako
 
kwanza kosa ni kuamini kuwa wewe unasauti kuliko mkeo na ndio upuuzi wa Sisi wanaume. Kila mtu ana uhuru wa kumfanya mtoto aamini kipi ni sahihi na kipi si sahihi...kuwakataza watoto wasifuate kile usichokiamini wewe ni Upuuzi na Ujinga... Wewe wafundishe na yeye awafundishe then watakapo kua watu wazima watajua ni wapi waelekee

Ushauri wa kipuuzi sana
 
Back
Top Bottom