Mke wangu anasumbuliwa na chunusi za uso

Habarini Wana Jf

Mke wangu anasumbuliwa na chunusi za uso zisizoisha ametumia lotion nyingi bila mafanikio naomba mnishauri atumie nini?
Mwambie achanganye udongo na Alovera pori ama kama anaweza kupaka alovera yale majimaji yake itakwisha. Ikishindikanika mwanbie achukue unga wa dengu ajipake nao yaani ajisilipe uso mzima kama ataweza alale nayo mpaka asubuhi.
 
Mimi kuna manzi nlikuwa namfukuzia ile mwanzoni tu akanipiga vizinga kidogo half akaniambia nimnunulie dawa ya vipele usoni inaitwa Eskinol

Akatumia ikamsaidia kabisa
 
Eskinol ni facial cleanser..
Baadhi ya Cleanser zinasaidia kupunguza ama kumaliza tatizo. Ila sii kusema ni dawa, kuna chunusi ni sugu wewe 😀
 
Habari, Alex Milanzi

Tafuta Sulphur Powder, tumia kijiko kimoja cha chai/chakula/kula katika mchanganyo wa mafuta au lotion | 200g isiyokuwa na kemikali wala viambata sumu.

Kutokana na matokeo ya wengi nakushauri tumia Lotion za Body Luxe au Goldy zinazotengenezwa na Tanga Pharmaceutical & Plastics Ltd. Kupitia hii lotion changanya mchanganyo wako wa Sulphur Powder kijiko kimoja, na robo kijiko cha Mdarasini.

Hakikisha wakati wa mchanganyo unatumia kijiko au kitu chenye asili ya urefu (Usitumie Vidole). Matumizi zingatia kupakaa maeneo yenye shida husika au hitilafu, ukikupendeza pakaa mwili mzima.

Je! Upakae muda gani? | Nashauri muda mzuri ni uliokuwa huru kwa mhusika hasa muda unaokuwa nyumbani au familiar places. Sababu Kuu ni harufu au hali ya kukera baada ya mchanganyo huu kuwa katika mwili na kuhusishwa na joto au hali ya jasho. (Sio kwa Wote)

Je! Ufanye nini? | Hakikisha baada ya masaa 8 Hadi 10 unaosha mwili wako au sehemu uliyopakaa dawa hii (Ikipendeza tumia maji ya uvuguvugu).

Je! Faida zake ni zipi? | Faida kuu ya dawa hii ni kupambana vilivyo na chunusi na magonjwa mbalimbali ya ngozi. Utumiapo dawa hii utaondosha chunusi, upele, maonesho ya mabaka yaliyobaki baada ya maradhi ya ngozi. Itakuacha na ASILI yako (Skin Tone), utakuwa nyororo na ngozi yenye muangaza.

Zingatia! Matumizi ya dawa na hakikisha mhusika anakunywa maji ya kutosha na kupata wasaa mzuri wa kupumzika.
-
Nimeshiriki katika tafiti mbalimbali ziliyohusisha tiba ya chunusi na maradhi ya ngozi. Binafsi na katika watu 346 waliotumia dawa hii, 339 wamepona kabisa tatizo la chunusi, ni 7 tu ndio ulionyesha matokeo tofauti.
Vipi kaka... nataka kujua, baada ya kuapply hayo mafuta ma kunawa uso baada ya hayo masaa, je naruhusiwa kupaka mafuta mengine au naacha tu hivyo hivyo bila kupaka mafuta yoyote?
 
Habari, Alex Milanzi

Tafuta Sulphur Powder, tumia kijiko kimoja cha chai/chakula/kula katika mchanganyo wa mafuta au lotion | 200g isiyokuwa na kemikali wala viambata sumu.

Kutokana na matokeo ya wengi nakushauri tumia Lotion za Body Luxe au Goldy zinazotengenezwa na Tanga Pharmaceutical & Plastics Ltd. Kupitia hii lotion changanya mchanganyo wako wa Sulphur Powder kijiko kimoja, na robo kijiko cha Mdarasini.

Hakikisha wakati wa mchanganyo unatumia kijiko au kitu chenye asili ya urefu (Usitumie Vidole). Matumizi zingatia kupakaa maeneo yenye shida husika au hitilafu, ukikupendeza pakaa mwili mzima.

Je! Upakae muda gani? | Nashauri muda mzuri ni uliokuwa huru kwa mhusika hasa muda unaokuwa nyumbani au familiar places. Sababu Kuu ni harufu au hali ya kukera baada ya mchanganyo huu kuwa katika mwili na kuhusishwa na joto au hali ya jasho. (Sio kwa Wote)

Je! Ufanye nini? | Hakikisha baada ya masaa 8 Hadi 10 unaosha mwili wako au sehemu uliyopakaa dawa hii (Ikipendeza tumia maji ya uvuguvugu).

Je! Faida zake ni zipi? | Faida kuu ya dawa hii ni kupambana vilivyo na chunusi na magonjwa mbalimbali ya ngozi. Utumiapo dawa hii utaondosha chunusi, upele, maonesho ya mabaka yaliyobaki baada ya maradhi ya ngozi. Itakuacha na ASILI yako (Skin Tone), utakuwa nyororo na ngozi yenye muangaza.

Zingatia! Matumizi ya dawa na hakikisha mhusika anakunywa maji ya kutosha na kupata wasaa mzuri wa kupumzika.
-
Nimeshiriki katika tafiti mbalimbali ziliyohusisha tiba ya chunusi na maradhi ya ngozi. Binafsi na katika watu 346 waliotumia dawa hii, 339 wamepona kabisa tatizo la chunusi, ni 7 tu ndio ulionyesha matokeo tofauti.
Mkuu asante sana, napata wapi sulphur powder?
 
Mwambie aache kutumia hizo lotion anazotumia na aanze kutumia mafuta ya nazi.

Pili, Sabuni za kuogea anayotumia. Ikiwezekana asiwe anapaka sabuni usoni
 
Aende tu hospitali akakutane na wataalamu. Hizi tiba za kuunga unga huku mitandaoni sio salama kabisa, mkeo anaweza kuharibu sura bure na usiweze kurekebishika.
 
Atumie lotion ya coco pulp...awe anapaka usiku tu, day time awe anapaka mafuta ya nazi
 
Back
Top Bottom