Mke Wangu Anapenda Sana Harusi Hadi Anaboa

JembeNaNyundo

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
532
646
Yaani kila mwezi lazima atumie laki 3 kwa ajili ya michango ya harusi. Nimemvumilia hadi nimemchoka. Ati ni hobby yake. Ukikuta mtu kaachwa ujue kuna mtu yamemfika hapa. Ngoja nitafute dogodogo wa kunipoza aendapo harusini.
 
unashindwaje kumcontrol mkeo ww si ndio baba wa familia au kuna baba mwingine zaidi yako kuwa mkali sio maisha hayo ndio hao wanaotaka kuonesha heshima kwenye maharusi wakifika wanaanza kutunzana hela kesho analialia njaa
 
Umeoa au umeolewa? tuyaache hayo... wewe ndiyo unafikria sasa hivi kutafuta nyumba ndogo aendapo harusini, mwenzio huo mchezo kaanza zamani sana kwenye hiyo mialiko anayokwenda...
 
Dah... Kumbe tatizo lako ni GHARAMA tu..... Je ungapata mwenye hobi na vigodoro?
 
Ukishaona mwanamke anafanya anachotaka unaogopa jitafakari mkuu... Utakuwa umeolewa... Mwanamke inabid afate nin wataka that's how true man act.
 
huyo mkeo umemtoa wapi, vingunguti, tabata matumbi, buguruni, temeke au mbagala? kama ni sehemu hizo usilalamike sana ndo utamaduni wao, so ukipenda boga penda na mbegu zake... cha kukushauri jifanye kama kila mwezi unamuoa upya afu unaalika marafiki na kasherehe nyumbani kwako... hataacha ila atapunguza.
 
Yaani kila mwezi lazima atumie laki 3 kwa ajili ya michango ya harusi. Nimemvumilia hadi nimemchoka. Ati ni hobby yake. Ukikuta mtu kaachwa ujue kuna mtu yamemfika hapa. Ngoja nitafute dogodogo wa kunipoza aendapo harusini.
We unatumia shs ngapi bar???
 
Ana nyota ya sherehe huyo mfungulie catering ili awe anaenda kusupply vyakula nk sio aende km mhudhuriaji tu
 
Back
Top Bottom