Mke wangu anaongea vitu bila mpangilio, itamchukua muda gani?

Mnyanyunda

Member
Aug 2, 2016
82
128
Mada tajwa hapo juu,naomba msaada kwa walio na ujuzi kwa hili..!Mke wangu amepasukiwa na chupa ya uzazi na mtoto kufariki naye hali yake si nzuri kuanzia ijumaa ya 10/8/2018.Jana jumatatu ameanza kutambua watu,jumanne ya leo hali yake kuanzia asubuhi ni kuongea vitu bila mpangilio (kubwabwaja) mpaka inanikatisha tamaa.Msaada wenu kwangu je hii hali ya kubwabwaja maneno itamchukua muda gani ndugu zangu?
 
Ndugu yangu mambo mengine sio ya kuyaandika humu kwa pupa

Hilo jambo ni la kidaktali zaid....

Muone Dk akusaidie by ze way watakuja watu wenye roho ngum watakwambia mkeo karogwa
 
Madaktari wanasemaje?
Isijekuwa kichaa cha mimba?

Nimeeasiliana na dktari usiku huu anasema ni matatizo ya ugonjwa wa uzazi na hii hali itakwenda itakuja mwacha sasa nimeshindwa kumwelewa ndio maana naomba msaada wa mawazo kwani mpaka muda huu bado mke wangu yupo icu
 
Kuchanganyikiwa kaka si lengo langu mkuu
Wasikilize madaktali wenye taaluma zao sisi huku porojo nyingi sana hatopata ufumbuz wa tatizo by ze way utalishwa matango pori tuu

Kuwa mpole najua uchungu wa mtt ndugu yangu

Try kuomba sana kwa sababu hakuna lishindikanalo kwa mungu
 
Nimeeasiliana na dktari usiku huu anasema ni matatizo ya ugonjwa wa uzazi na hii hali itakwenda itakuja mwacha sasa nimeshindwa kumwelewa ndio maana naomba msaada wa mawazo kwani mpaka muda huu bado mke wangu yupo icu
Sasa kumbe yupo ICU hospitali kuna madaktari sasa huku unakuja kutaka msaada gani? Hebu tuliza hizo stress kaka mkeo yupo mahala sahihi.
 
Write your reply...tuliza akili jamaa angu kama yupo ICU muombee has a kwa sala tu ndo dawa yake
 
Mada tajwa hapo juu,naomba msaada kwa walio na ujuzi kwa hili..!Mke wangu amepasukiwa na chupa ya uzazi na mtoto kufariki naye hali yake si nzuri kuanzia ijumaa ya 10/8/2018.Jana jumatatu ameanza kutambua watu,jumanne ya leo hali yake kuanzia asubuhi ni kuongea vitu bila mpangilio (kubwabwaja) mpaka inanikatisha tamaa.Msaada wenu kwangu je hii hali ya kubwabwaja maneno itamchukua muda gani ndugu zangu?
Inakukatisha tamaa? That is yo wife ndugu. Mtunze kwa hali yoyote na muoneshe upendo ktk magumu anayopitià. Wamama huvumilia sana, uzazi ni mgumu na wenye maumivu mno. Anakuhitaji zaidi sasa kuliko kabla.
 
Kuhusu hali ya mkeo, nimeona umesema yupo ICU, je kuna mahali pa kufaa huduma zaidi ya hapo? Jikaze na muombee atoke salama. Sometimes ni hali plus dawa alizopewa zinamlevya. I have experience with those medics!
 
Shukrani kwa ushauri
 
Nimeeasiliana na dktari usiku huu anasema ni matatizo ya ugonjwa wa uzazi na hii hali itakwenda itakuja mwacha sasa nimeshindwa kumwelewa ndio maana naomba msaada wa mawazo kwani mpaka muda huu bado mke wangu yupo icu
Kama yupo ICU wewe tulia tu, maana yuko kwa watalaam. Huku unaweza kuambiwa umchemshia majani ya kunde.
 
Uzazi unachangamoto sana sana,pole jikaze muombee kuwa na subra atarejea kwenye hali unavosema inakukatisha tamaa hapo unakosea sikiliza wataalamu kwa nafasi yako timiza wajibu wako kwan anachopitia ni kigumu sana
 
Back
Top Bottom