Mke wangu ananituma kutoka nje ya ndoa

Baba Loveness

Member
Sep 24, 2014
6
69
Wakuu ni najamaa yangu yupo kwenye wakati mgumu sana .kwani amekuwa akimrekebisha mke wake pale anapo kosea lakini mke wake anamtuma akatafute anae endana nae sasa haelewi afanye uamuzi gani kwani bado anampenda sana mke wake

Ameomba ni mshauri cha kufanya ni memwambia atoke nje ya ndoa ndiyo mkewe atashika adabu kwani dawa ya mwanamke mgomvi ni mwanamke mwenzake ..ati hapo nipo sahihi kwa ushauri nilio mpa
 
Mpe pole kakutana na mwanamke jeuri au mwanamke mashine akomae tu anamengi ya kujifunza ili akomae katika ulingo wa ndoa
 
"Mke ni kama chama cha siasa anahitaji chama cha upinzani ilu aweze kuimarika" Mzee wa Upako
Huyo jamaa aangalie ni wapi hasa anakosea. Pengine kuna vitu ama kero ndogondogo anazidisha mfano kumfatilia sana mke wake, ambavyo vinamchosha bibie.Hiyo ni kama ana jua kwamba mwanzoni alikuwa anapendwa. Unless otherwise jamaa anachapiwa
 
Wakuu ni najamaa yangu yupo kwenye wakati mgumu sana .kwani amekuwa akimrekebisha mke wake pale anapo kosea lakini mke wake anamtuma akatafute anae endana nae sasa haelewi afanye uamuzi gani kwani bado anampenda sana mke wake

Ameomba ni mshauri cha kufanya ni memwambia atoke nje ya ndoa ndiyo mkewe atashika adabu kwani dawa ya mwanamke mgomvi ni mwanamke mwenzake ..ati hapo nipo sahihi kwa ushauri nilio mpa
We unaonaje kwani? upo sahihi au?
 
Ajitafakari matendo na mwenendo wake, then akae chini na mke wake waongee kujua tatizo ni nini. Sidhani kama mwanamke anaweza akaamuka tu na kuanza kuongea hivyo. Lazima kuna tatizo.

Siku zote ni muhimu kutengeneza amani nyumbani kwa nguvu zote. Yaani mwanaume unatakiwa kulinda amani ndani ya nyumba kama rais anavyolinda muungano.

Nilirahisi kuona mke au mume wako ni mbaya, kwa sababu yupo, ila akiondoka ndo utajua umuhimu wake.
 
Mm mwanamke asiniambie habari sijui anataka break au nitafute mwingine....hapohapi ndio tumeachana
 
Kwani wanawake wameisha??
Unapotea nyumbani Kama Wiki hivi na kazini unaenda Kama kawa.
Akikupigia simu unamwambia nimempata sasa.
Atanyooka tu
 
Kwani wanawake wameisha??
Unapotea nyumbani Kama Wiki hivi na kazini unaenda Kama kawa.
Akikupigia simu unamwambia nimempata sasa.
Atanyooka tu
Shangaa mke akapotea mwezi mzima,,,, mpaka kamruhusu jamaa kutoka nje labda na yeye kuna sehemu anajituliza

Ni bora wakayajenga tu
 
Kifupi ni hv aachane kbs na project ya kumbadirisha mkewe hatobadirika labda apende mwenyewe
 
Back
Top Bottom