Mke wangu ananifuatilia FB

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Jamani waungwana naomba msaada wenu huyu mke wangu mie simuelewi kabisa.

mwanzoni mwa mahusiano yetu alikuwa na tabia sana ya kuchunguza simu yangu na hakuwahi kugundua message yoyote mbaya ingawa hata msg isiyo ya kimapenzi ikiingia kwenye simu yangu so long as inatoka kwa mwanamke basi siku hiyo ni vurugu kupita kiasi akidai huyo mwanamke atakuwa bibi yangu ama mpenzi wangu tu. siku mie niliposhika simu yake siku moja, nikagundua msg nyingi za kimapenzi toka kwa wanaume wawili tofauti, anaomba radhi nikamsamehe.

Baada ya muda alikuwa akinisumbua kwa kudai kuwa mimi nina uhusiano na wanawake chungu tele kuanzia wale ninaofanya nao kazi hadi mtaani. Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe yeye ndio ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu. mini ni mvumilivu nilimsamehe ingawa ni baada ua kukana sana na mwisho wa siku akakubali. hayo yakaisha mwaka jana.

Sasa hivi amekuja na mpya. Anasema kila mwanamke ambaye ni rafiki yangu facebook kwamba ni bibi yangu na anakomaa kwelikweli. mie nashindwa hata nimwambie nini ili aamini kuwa mawazo yake sio kweli maana kuna wasichana zaidi ya 1000 kwenye orodha ya marafiki zangu fb na wavulana kama 1000 wengine. kila comment yangu kwa mwanamke yoyote inakuwa ugomvi hauna mfano, kisa eti na comment kwa bibi yangu. kwakweli sina amani kabisa na hali hii inanikosesha raha.

Naomba waungwana mnisaidie nifanye nini maana nahisi kama anaanza tena kuficha uovu wake kwa kunipakazia mie, nahisi tu hilo sijafanya uchunguzi tena.
 
Kuna wimbo uliimbwa unaitwa MUME *****......... Au ndo maana halisi ya mume/mke bora hupewa/hutoka kwa Bwana??????????????????? Huo sio uvumilivu....... sijui niseme nikubaliane na NN kwamba ni degree ya juu ya uolewajwi.... yaani umeolewa...........
 
Sometimes kumbembeleza nako kunaleta shida. Jaribu kuweka msimamo wako, kama ataendelea mueleze wazi wazi bila kuuma uma maneno yale yanayokukera. Onyo: usimwambie siku akiwa amefura (hayuko kwenye mudi) haitakuwa rahisi kukuelewa.

Na kama hawezi kukusikiliza, basi ujue anajamaa lingine linampa kiburi, ndo mapenzi ya siku hizi.
 
umeanza kushauri vizuri,...ila umekuja pinda kidogo uliposema eti asubiri mpaka akiwa kwenye mood fresh_oooooooooooh!...hapana,..jamaa kama ni kuumia kaumia na kujeruhiwa papo_mtu mpaka anakuja jua anamegewa halafu anasamehe,.....kama vip achape mwendo kivyake
 
Sometimes kumbembeleza nako kunaleta shida. Jaribu kuweka msimamo wako, kama ataendelea mueleze wazi wazi bila kuuma uma maneno yale yanayokukera. Onyo: usimwambie siku akiwa amefura (hayuko kwenye mudi) haitakuwa rahisi kukuelewa.

Na kama hawezi kukusikiliza, basi ujue anajamaa lingine linampa kiburi, ndo mapenzi ya siku hizi.

Thanks RD kwa ushauri
 
Inaelekea huyo mkeo hajiamini hata kidogo...Hata kama ana wivu huo wake ni Babu kubwa.
Kwa hiyo anataka uwe na marafiki wanaume tu?
Mweleweshe tu, haina haja ya kumbembeleza, kama hataki kuelewa mwamie adhibitishe hayo mawazo/mamemo yake..

Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu sio ee...
 
Asante and naomba ushauri wako what can I do?

Achana na Facebook.

Facebook imekuwa chanzo cha mitafaruku mingi sana kwenye mahusiano. Mimi kama mimi sipo huko Facebook. Nipo ila nipo ki JF zaidi. Natumia jina la Nyani Ngabu na hata hivyo sijaingia huko tokea sijui lini..hata sikumbuki.

Watu huko huuza sura tu. Kila leo wanabandika mapicha yao halafu wanasubiri kumwagiwa misifa...ooh sijui you are beautiful...sijui I miss you...mara you look gorgeous...sasa kaka hebu fikiria kidogo. Yaani kama una mwenzako yuko huko halafu minjemba inamwagia misifa hivyo utapata amani kweli moyoni na akilini mwako? Vivyo hivyo kwako. Kama wachuchu wanakumwagia misifa kem kem mkeo au mpenzio unadhani atakuwa na amani kweli? Mimi sidhani hata kidogo.

Uamuzi wa mwisho ni wako. Ukiamua kubaki..poa tu...ukiamua kuachana nayo...na yenyewe haina ubaya. Mwisho wa siku pima uone jambo lipi ni la muhimu zaidi na fanya uamuzi kulingana na majibu utakayopata.
 
haya mambo mengine ni kama story tu,...eti unahisi demu wako hajatulia halaf unazidi ku compromise,.......anyway wengine labda tumeathiliwa na malezi

IGWE jua kwamba huyu sio demu wangu, ni MKE wa ndoa na hapo ndipo nashindwa nifanye nini na kuamua kuwaomba ushauri
 
Achana na Facebook.

Facebook imekuwa chanzo cha mitafaruku mingi sana kwenye mahusiano. Mimi kama mimi sipo huko Facebook. Nipo ila nipo ki JF zaidi. Natumia jina la Nyani Ngabu na hata hivyo sijaingia huko tokea sijui lini..hata sikumbuki.

Watu huko huuza sura tu. Kila leo wanabandika mapicha yao halafu wanasubiri kumwagiwa misifa...ooh sijui you are beautiful...sijui I miss you...mara you look gorgeous...sasa kaka hebu fikiria kidogo. Yaani kama una mwenzako yuko huko halafu minjemba inamwagia misifa hivyo utapata amani kweli moyoni na akilini mwako? Vivyo hivyo kwako. Kama wachuchu wanakumwagia misifa kem kem mkeo au mpenzio unadhani atakuwa na amani kweli? Mimi sidhani hata kidogo.

Uamuzi wa mwisho ni wako. Ukiamua kubaki..poa tu...ukiamua kuachana nayo...na yenyewe haina ubaya. Mwisho wa siku pima uone jambo lipi ni la muhimu zaidi na fanya uamuzi kulingana na majibu utakayopata.

Walau sasa umekuja na ushauri. Nashukuru, nitapima NN
 
Na wewe huko FB unafanya nn.MIMI MME WANGU MPENZI hayupo FB yuko biz na drawings zake.Na ww funga hiyo FB mkeo apate amani
 
IGWE jua kwamba huyu sio demu wangu, ni MKE wa ndoa na hapo ndipo nashindwa nifanye nini na kuamua kuwaomba ushauri

Ndio uache kuutesa moyo wako_mkeo wa ndoa kwa nn amegwe tena na rafiki yako,...anyway sijui imani yako-kama muislam mlime talka 3 na kama mkristo kama mm mshit kimya kimya
 
Ndio uache kuutesa moyo wako_mkeo wa ndoa kwa nn amegwe tena na rafiki yako,...anyway sijui imani yako-kama muislam mlime talka 3 na kama mkristo kama mm mshit kimya kimya

Mie Mlutheri, Mke mmoja maisha yote na hapo ndipo pananikosesha amani kila ninapofikiria kumuacha
 
Back
Top Bottom