Mke wangu analeta kiburi, hataki niongeze mtoto wa sita

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,619
21,361
Bila shaka mko poa,

Naleta hii inshu kwenu najua kwenye wengi pana mengi hope nitapata mchango wa kumshawishi mke wangu inshu yenyewe iko hivi, katika kujituma kazini kwangu nimefanikiwa kupata nyongeza ya mshahara, tena ni kubwa kidogo maana ni kama 40% ya mshahara wangu wa zamani, kwa maana nyingine inanipa wigo mpana wa kuwa na familia kubwa zaidi, familia yangu bado changa sana kwa maana ya idadi ya watoto kwani tangu nimuoe huyu mke miaka 7 iliyopita tumefanikiwa kupata watoto watano pekee.

Naona mke wangu analeta tabia ambazo anakutana nazo saluni kwa sababu makubaliano yetu ya mwanzo ilkuwa tuwe na watoto 8 ,ili watoto wanne awaite majina ya ukoo wao na mimi 4 niwaite majina ya ukoo wetu, maana tunatokea jamii ambazo tuna imani ya watoto wengi ndo utajiri wenyewe.

Ombi, lenu kwenu je nitumie njia gani ili huyu mwanamke aweze kunielewa japo na karibia kuoa mke mwingine ili niweze kufikia malengo yangu?
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka mko poa
Naleta hii inshu kwenu najua kwenye wengi pana mengi hope nitapata mchango wa kumshawishi mke wangu.

inshu yenyewe iko hivi,Katika kujituma kazini kwangu nimefanikiwa kupata nyongeza ya mshahara,tena ni kubwa kidogo maana ni kama 40% ya mshahara wangu wa zamani,kwa maana nyingine inanipa wigo mpana wa kuwa na familia kubwa zaidi, familia yangu bado changa sana kwa maana ya idadi ya watoto kwani tangu nimuoe huyu mke miaka 7 iliyopita tumefanikiwa kupata watoto watano pekee.

Naona mke wangu analeta tabia ambazo anakutana nazo saluni kwa sababu makubaliano yetu ya mwanzo ilkuwa tuwe na watoto 8,ili watoto wanne awaite majina ya ukoo wao na mimi 4 niwaite majina ya ukoo wetu ,maana tunatokea jamii ambazo tuna imani ya watoto wengi ndo utajiri wenyewe.

Ombi lenu kwenu je nitumie njia gani ili huyu mwanamke aweze kunielewa japo nanikiria kuoa mke mwingine ili niweze kufikia malengo yangu?
khaa,...kwelii starehe ya maskini ni kale kamchezo ketu,......
 
Duh! Mkuu unatokea pande zipi??? Yaani siku hizi watoto wa 3 tu ni wengi mno, we wa 5 ndani ya miaka 7 na bado unataka wengine wa 3 ili wafike 8??? Hakika hizo zama zishapitwa na wakati, unamzeesha mkeo bure. Babu zetu walifanya hivyo coz maisha ya kipindi chao yalikua na details chache, ilikua either kulima, kuchunga au kuwinda mradi tu chakula kiwepo maisha yanasonga, ila kwa dunia hii ya Leo ya utandawazi mtoto anahitaji mengi zaidi ya chakula na malazi.,so idadi kubwa ya watoto ni mzigo na si fahari tena
 
Dollor inazidi kupanda, life expectancy tz inazidi kushuka, kina mama wamekuwa na ckmplications nyingi wakati wa kuzaa tofauti na zamani sababu ya vyakula na tabia nchi..n.k

Lakini mtu bado anataka awe na watoto nane?!
 
Bila shaka mko poa
Naleta hii inshu kwenu najua kwenye wengi pana mengi hope nitapata mchango wa kumshawishi mke wangu.

inshu yenyewe iko hivi,Katika kujituma kazini kwangu nimefanikiwa kupata nyongeza ya mshahara,tena ni kubwa kidogo maana ni kama 40% ya mshahara wangu wa zamani,kwa maana nyingine inanipa wigo mpana wa kuwa na familia kubwa zaidi, familia yangu bado changa sana kwa maana ya idadi ya watoto kwani tangu nimuoe huyu mke miaka 7 iliyopita tumefanikiwa kupata watoto watano pekee.

Naona mke wangu analeta tabia ambazo anakutana nazo saluni kwa sababu makubaliano yetu ya mwanzo ilkuwa tuwe na watoto 8,ili watoto wanne awaite majina ya ukoo wao na mimi 4 niwaite majina ya ukoo wetu ,maana tunatokea jamii ambazo tuna imani ya watoto wengi ndo utajiri wenyewe.

Ombi lenu kwenu je nitumie njia gani ili huyu mwanamke aweze kunielewa japo nanikiria kuoa mke mwingine ili niweze kufikia malengo yangu?
mwambie aache mambo ya ajabu ajui ada imefutwa nini
 
Sita? Halafu wale nini? We endekeza kuwafyatua tu kama matofali ukidhani jua litayakausha. Watakutafuna hao!
 
Duh aiseee we kidume mi tangu nioe hadi mwaka jana mwezi wa kumi na moja nimetimiza miaka minane nina watoto wawili tu ndo wanapishana miaka minne na nusu huyu wa pili ana miaka mitatu nataka hadi afikishe minne net ndo niatafute wa tatu wewe mwenzangu unawapishanisha mwaka tu au mwaka mimba mwaka mtoto pemba style hiyo kaka ilopitwa na wakatu funguka kama umeongezwa mshahara tafuta la kufanya kuongeza kipato zaid ya hapo fungua miradi mshirikishe mkeo mueke busy asimamie miradi mshirikiane kulea hao ulonao kwanza watafutie cha kurith nyumba kama unayo ongeza si mbaya
 
Go on man!!! If you are able to feed them and you are depositing enough fund to run your family in the future. Convince her she will agree as women are easily to be convinced
 
Back
Top Bottom