Mke wangu anakuwa busy na sim ifika jioni. Ni nini?

Hii si kawaida sana kwa mke!!! ukiona hivyo na kama hayuko tayari kukushirikisha anachowasiliana jua kuwa huna mke. Kwa upande wa pili ni wanaume wangapi ambao huwa wana tabia kama ya mke wako hata wengine wana password na kuzima simu usiku na line nyingi za mashaka!!! Ndoa zimegeuka smaku na mobile phones are the catalysts!!
 
vunja ukimya.........jarbuni kuliweka hili mezan,penzi linakuzwa na mawasiliano ati!hata hivyo ci vibaya kuwa wivu ni vyema mkazungumzia kero za muungano wenu
 
Sasa kama wewe uko home yeye anakuwa busy na simu anachat na nani??
:pray::pray:
Hebu mwambie vile unavyojisikia kuhusu hiyo tabia yake
 
Hivi shosti, mume hana mawasiliano mchana kutwa, akirudi home kavuta mdomo kama bata anaangalia mipira! Unafanyaje na unacheka na nani? Hao unaowasiliana nao kutwa unaishia kucheka nao usiku! Siku hizi mwanaume akiwa na small house ati ananunia mkewe! Jando inabidi irudi tu aisee!
Hili nalo neno......
Mleta mada natumaini umesikia hili....
 
Saa zingine anachat umbea tu na wanawake wenzie wanasimuliana misery zao za maisha! Sasa utaangua kicheko kumbe mnawaponda waume zenu ili kupunguza maumivu, mume akidaka simu si atazimia? Kama ni mabwana zake atachat nao mchana kutwa na kuwapigia, wala hahitaji ku-risk hivyo!
King'ast hapo kwenye Red nimepapenda, hapo kwenye bluu naamini tayari ameshawapa kwa nini akajificha chumbani kama hakuna kitu kati yao?! mjomba mlete mada, huyu angekuwa ni girlfriend au mchumba ningekushauri TAFAKARI, CHUKUA HATUA. Lakini kwa kuwa ni mke sithubutu kukwambia hivyo nachoweza kusema ni angalia hapo kwenye red ya King'ast naamini amemaliza kila kitu ambacho ningeweza kusema kwa maneno machache!
 
Wanajamii habari za jioni. Mke wangu ikifika jioni mpaka usiku anakuwa busy sana na sim hata mda wa kuongea na mimi hana, wakati mwingine tukiwa sebureni hujifanyifa anaumwa na kwenda chumbani, ukienda gafla unakuta vidole vinacheza kwenye sim. Mimi kiukweli sio kwamba wivu umekuwa juu, lakini je ni sahihi kwenye ndoa? Na wala sio mfanyabiashara. Naombeni ushauri nisije nikawa mimi nakosea.

Pole sana ndugu! Facebook hiyo!
 
kaka usijiumize kichwa na kujipa mawazo yasiyo na lazima, hapo muhimu ni kumuuliza tena tumia hekima sana na kwa mapenzi na akiwa katika mood nzuri, kuwa mbona anakuwa bize sana na sim huwa anakuwa anawasiliana na nani au ni internet?mwambie kuwa unamiiliza hivyo kwa kuwa unampenda sana na unahitaji muda wake, hivyo anapokuwa bize na simu wewe unakuwa unamkosa, hivyo umuombe ajitahidi kujirekebisha....muoneshe kuwa unahitajio sana muda wake sio kila wakati simu peke yake. Naamini kama anakupenda kwa dhati atakusikiliza na kujirekebisha, na utafurahi (BILA MABAVU PLIZ)....KILA LA KHERI NSHAALLAH!
Wanajamii habari za jioni. Mke wangu ikifika jioni mpaka usiku anakuwa busy sana na sim hata mda wa kuongea na mimi hana, wakati mwingine tukiwa sebureni hujifanyifa anaumwa na kwenda chumbani, ukienda gafla unakuta vidole vinacheza kwenye sim. Mimi kiukweli sio kwamba wivu umekuwa juu, lakini je ni sahihi kwenye ndoa? Na wala sio mfanyabiashara. Naombeni ushauri nisije nikawa mimi nakosea.
 
Mjini shule kiongozi..ukiona manyoya ujue kachoropoka..anza kumfatilia kuanzia sasa.,unaweza ukawa usaliti ndio unaanza ivyo
 
Ni vizuri sana ukaongea naye, yaweza ikawa yuko na mahusiano ya nje au sio kabisa.Ni vizuri ukaongea naye na umweleze kuwa hupendezwi na hiyo tabia. Kama ana-cheat iko siku utajua ukweli.
 
Wanajamii habari za jioni. Mke wangu ikifika jioni mpaka usiku anakuwa busy sana na sim hata mda wa kuongea na mimi hana, wakati mwingine tukiwa sebureni hujifanyifa anaumwa na kwenda chumbani, ukienda gafla unakuta vidole vinacheza kwenye sim. Mimi kiukweli sio kwamba wivu umekuwa juu, lakini je ni sahihi kwenye ndoa? Na wala sio mfanyabiashara. Naombeni ushauri nisije nikawa mimi nakosea.

Labda anacheza kamri ya AIRTEL ili apate shs 3,000,000
 
Muda wa jion tumia kupga stor na mpnz wako,pia msaidie kuandaa vitu vidogo kama juice,kachumbari nk kwa ajil ya mlo wa usiku.Baada ya mlo mkiwa kitandani hold her tight,kiss her then mpe haki yake inayostahil mpk aridhike.
Cjui atapata wapi muda wa kuchat.,mfanye aone ww wa muhimu aogope kukupoteza,huwa anachat kwasababu hana cha kufanya.
 
piga marufuku mobile phone ikishafika jioni, akutakae atapiga landline

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Du! Hapa jf kweli unaweza ua ndoa, kuna ushauri mwingine sio mzuri. Nimekueleweni wajameni, ila kusema kuwa kuna watu wanangata kweli yawezekana but it pains.
Chukua yanawezekana, mengine yaache hapa kwa ajili ya kumbukumbu zetu za baadae. All the best, jitahidi kumuweka karibu. Toka naye weekend, try new staffs kama kwenda sehemu siku mbili tatu huku ukiangalia muelekeo.
 
Umemnunulia simu lini..............wengine ni ushamba wa technolojia, anaweza akawa anacheza gemu la nyoka kwenye Nokia Tochi!!:bump:
 
Mkuu hata kabla hujasema anatumia simu ya aina gani labda niseme anatumia Blackberry haha kama ndio then atakuwa BBM huyo na sio vingine maana hiyo kitu inamfanya mtu awe busy sana, na kuwa nae makini maana ni hatari BBM
 
Back
Top Bottom