Mke wangu ana mimba ya miezi mitatu na wiki mbili ila mtoto anacheza tumboni!

Mtanzatozo

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
972
1,163
Habari wakuu

Mke wangu ana mimba ya miezi mitatu na wiki mbili ila mtoto anacheza! Je, hili sio tatizo?
 
Habari wakuu

Mke wangu ana mimba ya miezi mitatu na wiki mbili ila mtoto anacheza! Je, hili sio tatizo?
Kwa mimba ya kwanza Quickening/Mtoto kucheza uanza kwenye week ya kumi na sita au zaidi.
Na Kwa Mimba ya pili nakuendelea Mama anaweza kuhisi Quickening hata ndani ya week 13.

Mkeo kwa sasa ana almost week 15.
Je, hii ni mimba yake ya kwanza?
 
Kwa mimba ya kwanza Quickening/Mtoto kucheza uanza kwenye week ya kumi na sita au zaidi.
Na Kwa Mimba ya pili nakuendelea Mama anaweza kuhisi Quickening hata ndani ya week 13.

Mkeo kwa sasa ana almost week 15.
Je hii ni mimba yake ya kwanza?
Alhamdulillhah mkuu! hii mimba yke ya pili..! hesabu yake anasema ni miezi 3 na wiki mbili na leo kliniki yake
 
Habari wakuu

Mke wangu ana mimba ya miezi mitatu na wiki mbili ila mtoto anacheza! Je, hili sio tatizo?

Hapa kunaweza kuwa na vitu viwili.

Kawaida hali hii huweza kumtokea mama mjamzito wiki ya 17-20 kwa aliyekwisha kupata mtoto hapo kabla. Na wiki ya 21-22 kwa yule ambaye hajawahi kupata mtoto.

Moja, inawezekana anachokipata mama mtoto ni hisia za kisaikolojia zaidi kuliko hali halisi.

Mbili, inawezekana pia ujauzito ukawa na mkubwa kuliko makadilio aliyonayo. Hii hutokea kama mama pamoja na ujauzito alipopata aliendelea kupata damu kama ya hedhi, lakini inakuwa siyo nyingi na kwa muda mrefu kama ya hedhi. Hii huwachanganya na kuona amepata hedhi. Kutatua hili ni kama mmefaya altrasound kuona umri huu ni halisi.
 
anaweza kuwa na mimba ya wiki 17 na aka blidi mkuu..?

Ndiyo, lakini siyo hedhi kabisa, kunakuwa na utofauti kwenye kiasi cha damu na urefu wa muda wa kupata hiyo damu.
Inakuwa vagina bleeding in pregnancy. Sababu zake zipo na hutokea , haipaswi kuchukuliwa kama kitu cha kawaida.

LAKINI:
Nilichokieleza hapo kabla ni kitendo cha mama kushika ujauzito ile wiki nne za mwanzo kwa bahati mbaya mama akaona damu ambayo hutoka karibu kabisa na muda wa hedhi. Na yeye huihesabu kama hedhi, wakati ni mjamzito. Atakapokuja kugundua kuwa ni mjamzito anaweza kuhesabu kwa kutokujua akawa na wiki chache za kuhesabu za ujauzito kuliko umri halisi wa mimba.

Na kilichoelezewa hapo juu pia kwenye wiki ya 17-21 ni quickening, yaani mama kuanza kuhisi mtoto wake akiwa anajongea/kutembea. Hali ya kumgusa kwa ndani.
 
Back
Top Bottom