Mke wangu ana kawaida ya kukagua simu yangu kila siku, nini dawa yake?

Sep 5, 2019
89
73
Aisee nimeamini kuwa 'Samaki mkunje angali mbichi'

Tabia hii niliichukulia kawaida hapo awali Ila sasa nimeichoka. Nikirudi tu toka kazini atakimbilia simu na:

1. Kuangalia sms (kisha atazifuta)
2. Kuangalia calls (na kuzifuta)
3. Akikuta namba ngeni lazima aulize
4. Simu ikipigwa akiwepo huikimbilia na kuiangalia.

Nimechoshwa haka ka tabia. Hebu nipeni muarobaini nimkomeshe na aache upuuzi huu.

NAPOKEA UPONYAJI.
 
Ya finger print haifai hata kidogo asjaribu mana akikutana na mwanamke mjanja anategeshewa siku aliyochoka sana akilala mwanamke anachukua sim anaenda kuigusisha kwenye kidole af ndo anaskilzia mziki wake Hahahaaaaa & this is proved
Dawa ni kutoweka dole gumba . Mimi fingerprint nimeweka kidole kidogo cha kushoto sasa mpaka aje apatie ni lini? Na 5 attempts tu simu inajiloki
 
Hata wangu alikuwa na tabia hiyo.Nilichofanya nikamwambia nakupa 3 trials,ukishindwa kujibehave naweka password,mtihani ukamshinda nikatimiza ahadi.Sasa ni mwaka na nusu sipati makelele yake.Majuzi kanishukuru sana kwa trick niliyoifanya kwani nilimuepusha na mengi.Sasa bado katabia kengine nako nimemwambia ukiendelea nakupa dawa fulani mpaka utakapokoma mwenyewe.Vimaswali vya ulikuwa wapi,hivi ulikuwa kwa malaya zako,mara utapata magonjwa na umalaya wako basi nimemuahidi tena kwa mara nyingine kuwa kwakuwa vimaswali hivyo havikomi,basi naanza kukupa majibu ya kukuchoma moyo.Akiniuliza ulikuwa wapi,na mjibu nilikuwa kwa mke mdogo na anakusalimia sana.
 
Tarehe ya kuzaliwa, Mwache tu akikua ataacha. We usifute msg yoyote hata ya mcheps iache aje aione. Akiuliza kaa kimya...atalia weeee mwisho wa siku simu yako ataoina kituo cha polisi.
Njia ya pili na wewe anza kukagua yake..muulize kila msg hata Kama ya kawaida we muulize tu akufafanulie utaona na yeye anakereka. Ataacha kushika simu yako.
Dawa ya moto ni maji!
 
Back
Top Bottom