Mke wangu amezaa nje ya ndoa nimeamua tuachane .nisaidieni juu ya hili.

MZEE SERENGETI

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
214
10
Wana,JF Naomba ushauri wenu.
Nilikuwa nimeoa na huyo mke nilikuwa nimezaa nae watoto wawili,nikapata nafasi ya kwenda kusoma hapahapa Tanzania,Mke wangu ni mwalimu wa shule ya Msingi,nilipokuwa chuo tulikuwa tunawasiliana vizuri,nilikuwa naendalikizo,lakini mara nyingi nilikuwa siendi likizo zote kwa sababu ya hali ya uchumi,na nilikuwa namwambia kwamba siendi likizo kwa sababu ya hali ya kiuchumi ambayo hata yeye alikuwa anaijua,nili kuwa namwambia ntabakia kwenye mkoa huu na kwa ndugu yetu ambaye na yeye anamfahamu,hadi namaliza chuo nikapata Temple ambayo ingeweza kutusaidia,kupata chakula,nikamwambia fanya utaratibu wa uhamisho,akasema sawa,badae siku hiyo hiyo usiku akanipigia simu akaniambia mimi ni sasa hivi ni MJAMZITO SI WEZI KUJA HUKO,Nikamuuliza umeolewa?akasema hapana,Tangu pale nikaona kuwa hatanifaa,watoto wako shule nina wahudumia mwenyewe nikimwambia changia shilingi elfu kumi,anakuwa mkali sana,tangu pale sikuwahi kumwambia chochote kuhusu watoto.
HADI HVI SASA HATUKO PAMOJA LAKINI YEYE ANATAKA TUSAMEHEANE NA TUISHI PAMOJA NIMEKATAA.
(NIMEONA NILILETE KWENU WADAU MNISAIDIE)
 
Maskini.... Wanawake wengine wanapata waume wazuri wao wanageuka magodoro. Wanaume wanaopata wake wazuri waaminifu ni vise versa. Sijui Mungu ametuunganisha hasi na chanya ili tusaidianeje? Shukuruni kwa kila jambo. Ni msumari, lakini jipe muda wa kuumeza pengine utayeyuka. Duuuhhhhh!!!!
 
Duuh mkuu ulioa kihalali, yaani mkeo wa ndoa anakuwa na ujasiri wakukwambia kuwa mjamzito,
 
Aise pole sana mkubwa najua upo kwenye wakati mgumu sana? naomba nikuulize swali mlifunga ndoa?
 
nyie hamjaoana kihalali mechukuna tuu kwani amepata wapi ujasiri wa kukuambia ushenzi huo? Huyo piga chini
 
Duh, Yaani anakuambia mjamzito wakati wa safari.toka alipohisi kitu kwa nini hajakuambia?Hebu jaribu nionane akupe details.
 
pole mkuu...
kuna ya kusamehewa sio hilo, watu wanapiga chini mke aliyetembea nje ya ndoa sembuse huyo alieamua kukuletea kid kabisa...
nakushauri achana nae mkuu!!
 
daaaaah pole sana, labda nikuulize swali wewe waweza kuendelea kuishi na huyo mkeo ilhali unajua kakusaliti mpaka kapata ujauzito? ukipata jibu then pigia mstari
 
Maisha haya,wanaume wakizaa nje wanasameheka wengiwao.ila wanawake ni ngumu ndo nature.MSAMEHE.
 
HADI HVI SASA HATUKO PAMOJA LAKINI YEYE ANATAKA TUSAMEHEANE NA TUISHI PAMOJA NIMEKATAA.
(NIMEONA NILILETE KWENU WADAU MNISAIDIE)

Mkuu hakuna mtu anaejua hii case kuliko wewe na sababu umeshaamua hapo mwanzo kukataa basi huo ni uamuzi wako.., sababu things will never be the same na kukaa kwenu pamoja kunaweza kuleta athari hata kwa watoto..

Cha muhimu wewe hakikisha hao watoto wanapata malezi bora na mahitaji yao ya kila siku hakuna sababu ya kumlazimisha achangie... (kuhusu huyo mwenza wako wewe ndio unamjua vizuri na uamuzi utakaochukua utakuwa ni sahihi...)
 
pole sana mkuu .... je huo ujauzito alikuambiwa ni wa muda gani na mhusika ni nani ??? katika taarifa yake unaona kuna majuto yoyote??
 
Na hao watoto wawili siyo wa kwako - To be very very Honest - wewe haujawahi kuoa!

BE umemsoma vizuri enhee...huyu jamaa kuna mengi yamejificha. Hapa tumepata story ya upande mmoja kama chapati iliyo kaangwa upande mmoja. Ukimsoma vizuri utagundua something is very wrong somewhere....wewe utamwachaje mwanamke mpaka apate mimba...afu wewe huko chuoni ulikuwa unaishije????? Huyo mama angekuja hapa akatoa story yake probably Mkuu Serengeti ungepigwa na mawe!
 
Wana,JF Naomba ushauri wenu.
Nilikuwa nimeoa na huyo mke nilikuwa nimezaa nae watoto wawili,nikapata nafasi ya kwenda kusoma hapahapa Tanzania,Mke wangu ni mwalimu wa shule ya Msingi,nilipokuwa chuo tulikuwa tunawasiliana vizuri,nilikuwa naendalikizo,lakini mara nyingi nilikuwa siendi likizo zote kwa sababu ya hali ya uchumi,na nilikuwa namwambia kwamba siendi likizo kwa sababu ya hali ya kiuchumi ambayo hata yeye alikuwa anaijua,nili kuwa namwambia ntabakia kwenye mkoa huu na kwa ndugu yetu ambaye na yeye anamfahamu,hadi namaliza chuo nikapata Temple ambayo ingeweza kutusaidia,kupata chakula,nikamwambia fanya utaratibu wa uhamisho,akasema sawa,badae siku hiyo hiyo usiku akanipigia simu akaniambia mimi ni sasa hivi ni MJAMZITO SI WEZI KUJA HUKO,Nikamuuliza umeolewa?akasema hapana,Tangu pale nikaona kuwa hatanifaa,watoto wako shule nina wahudumia mwenyewe nikimwambia changia shilingi elfu kumi,anakuwa mkali sana,tangu pale sikuwahi kumwambia chochote kuhusu watoto.
HADI HVI SASA HATUKO PAMOJA LAKINI YEYE ANATAKA TUSAMEHEANE NA TUISHI PAMOJA NIMEKATAA.
(NIMEONA NILILETE KWENU WADAU MNISAIDIE)
Sasa ndugu yangu wee umekwisha fanya maamuzi na umekwisha kataa, sasa sisi tukusaidie nini au bado unampenda unatafuta sababu za kurudiana naye? Hilo li mwanamke halikufai linachiti sana mpaka limeamua kutotumia kinga!!! angalia litaja kukuua
 
Back
Top Bottom