Mke wangu amepewa taarifa zangu na mtandao wa simu. Kisheria imekaaje?

TAI DUME

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
8,840
23,066
Wakuu!

Wiki 2 zilizopita nilisafiri kikazi kwenda mkoani kwa kazi ya siku 5. Siku moja kabla ya kurudi nyumbani nikaongezewa kazi ya wiki moja nyingine.

Kimbembe kikawa kwa wife nyumbani hakunielewa. Kukatokea kupishana ila mm sikujali sana coz sikuichukulia serious sana na kweli nilikuwa mkoani kikazi. Yeye akawa anadai nipo hapahapa Dar kwa michepuko yangu.

Sasa jana nimerudi home toka mkoa nimekuta ana printout ya mawasiliano yangu yote ya kwenye simu. Kwa maana ya kwamba niliifuma karatasi inayoonyesha nimewasiliana nani, wakati gani, yupo wapi na mm nikiwa wapi. Na nilimpombana zaidi akadai ana uwezo wa kupata mpaka voice clip zangu kwa ninaowasiiliana nao.

Japo ilimthibitishia ni kweli nilikuwa nimesafiri lakini imeniogopesha sana. Kwa stage hii aliyofikia huyu anaweza kunidukua chochote kile kwenye simu yangu.

Wataalam wa sheria naomba mnisaidie hii kisheria imekaaje, Je kwa kuwa yeye ni mke halali wa ndoa, ni haki yake kupewa hizo taarifa? Vp kama nikiamua kuishtaki hiyo kampuni mimi kama mteja wao je sheria itanibeba?

Sina nia ya kuprocess kesi yoyote lkn nataka tu kufahamu.

Majibu yenu tafadhali.
 
Mkianza kutumia sheria za mahakamani...na kuendeleea kudokoa dokoa simu
Dah hiyo combination hapo inazaa uadui wa kutosha.
Msifikie mbali sana kuchunguzana na kuhukumiana.
Usitumie sheria.
Kaa nae ndoa ikishaingiza zaidi ya mtu mmoja
Sio ndoa tena ni kikundi.
Ongea nae.
Utatia doa ndoa yako.yeye kashakosea ila wewe ukienda kisheria atakua kasawazisha...means itakua ndo mwanzo wa kupelekana mahakamani mpaka uzikwe wap itaamuliwa mahakamani.
Speaking from experience....ongea nae kwa urafiki zaidi usitumie sheria.
Ila kama hakuamini kwa kiwango hicho mzee
Mpo kipindi kigumu sana.
Muombe Mungu...usizid kufungua zaidi milango ya kuingiza shetani katika familia yako.
Ila muonye kwa maneno
 
inawezekana kabisa kama una mtu ndani ya mtandao husika
kuna namba yangu ilifungwa, na ilikua site mbali na nilipo

nikamtaarif rafiki, yeye akawasiliana na rafiki yake
nikapewa PDF ya bounds zote zilizoingia na kutoka, mpaka waliosajili ile namba kabla yangu
nikashangaa
 
Back
Top Bottom