Gobret
JF-Expert Member
- Jun 11, 2010
- 320
- 88
Hiyo ndoa ni ya Kiislam, sina kimwana
Pole sana mkuu, inauma sana hasa pale unapokuwa mwaminifu kwa mwenzako lkn mwenzako hawi mwaminifu kwako. Nadhani mimi nipo upande wako zaidi kwa jinsi nitakapohisi au kusikia au kuona kuwa mwenzangu ananisaliti. Hakika nitaumia sana na ninaweza kuchukua uamuzi mbaya sana. Sijui ninaweza kuchukua uamuzi gani maana naomba yasinikute maana sijielewielewi vizuri ktk jambo kama hili.
Ninachoweza kusema ni wewe kuyatazama maisha yako upya kabisa, jinsi ulivyosimama na pia fikiria kama wewe ndio uko kwenye hilo anguko. Je, hali ingekuweje. Mshirikishe Mungu zaidi kwa jinsi ninavyokuona ni kijana uliyeshika vizuri imani yako ya kiislamu. Hata kama kuna utaratibu wa kuachana ambapo imani husika inauruhusu lkn bado wewe unanafasi pekee ya kuridhia jambo hilo. Usifanye uamuzi kwa hasira, tulia na ikibidi ufunge kwa ajili ya hilo na uwashirikishe wakuu wako wa kiimani. Naamini watakushauri vizuri.
Kumbuka maisha atakayoishi mwanao pindi utakapotengana na mama yake kwa kufanya uamuzi wakati una hasira. Utaoa mwanamke mwingine na hali usidhani itakuwa tofauti pengine ni zaidi ya hayo au pengine ukabahatika kumpata mwaminifu lkn ukweli ni kuwa huwezi kujua.
Pengine mwenzako alighaflika kidogo lkn sivyo alivyo. Kumbuka kati ya kiumbe kilichozaliwa na m/ke hakuna kilichokosa udhaifu, wote tuko sawa ndio maana kwa Mungu kuna msamaha.
Mwisho, kukubali kuishi maisha ya ndoa kuna changamoto zake, haijalishi imuishi miaka mingapi. Je, hayo yangekutokea mkiwa mmeishi mfano miaka 25 ya ndoa yenu ungefikiria uamuzi gani? Au kwa sababu leo una nguvu ya kuoaa mwingine na bado watakupenda; ktk umri huo huoni ni tofauti? Sipingi talaka ktk imani zetu bali nasema tusitumia hasira au jazba ktk kutoa talaka tafakari sana.
Mimi ni mkristo, sipingi mafundisho wa Mtume maana ni mtume wa Mwenyezi Mungu hata kama mafundisho ninayopewa hayanitumii huko lkn nina imani kuwa wote wanaofuata mafundisho yake ni wengi na ni watu wazima wenye akili zao nzuri tu kama Wakristo. Kwa maana hiyo kama kijana wa kiislamu una imani thabiti: tulia, tafakari sana na mpe Mungu nafasi ktk kufunga kwa ajili ya matatizo yako. Nina imani kuwa Mungu atakupa jibu na utalitatua jambo hili vizuri sana.
Pole sana kijana mwenzangu na poleni wanawake ambao pia haya yanawakuta kwenye maisha yenu.