Mke wangu amenisaliti kwa ushahidi wa mazingira, nifanye nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wangu amenisaliti kwa ushahidi wa mazingira, nifanye nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kipusy, Sep 5, 2011.

 1. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Jamani naitaji msaada mkubwa sana, wa mawazo na saikolojia. Mimi nina mke nimezaa nae. Tangu tufunge ndoa ni miaka 4 sasa.
  yeye yuko Mkoani mimi niko chuoni Dar es Salaam kimasomo elimu ya juu. Wiki za nyuma kabla ya sikukuu ya Idd mawasiliano na mke wangu yaliyumba sana, yalitawaliwa na kiburi sana.

  Nimeenda kwenye sikukuu ya Idd ndio nikagundua usaliti. Mke wangu alikua bize sana na simu, pia alikua anaificha sana tofauti na mwanzo, haitoki mkononi kila mara anaandika msg. Nikaiwinda nikashindwa.

  Siku moja alitoka kazini akanisalimia akakaa kidogo sitting rum kisha akaenda chumbani mida ya saa 1 usiku. akazima taa kajifunika blanket. Mi nikaingia chumbani nikawasha taa. Nikamuuliza mbona umelala saa hizi, sio kawaida? akajibu' nilipokua natoka job nimejigonga mguu unauma...., nikamjibu poa. Nikamwambia ' naomba simu yako" akakataa katakata na sikujua iko wapi. akasema wewe ya nini si unayo yako? nikamwambia ninashida nayo, akasema nenda ntakuletea zima na taa...

  nikatoka chumbani sikuzima taa, nikarudi nikakuta kazima tena na kajifunika kama mwanzo. Nikatumia nguvu nikampekua nikamnyang'anya simu. Baada ya kumnyang'anya nikawa nayo mimi, baada ya muda kidogo ikaingia msg inasema "Thanks hny"

  Nikaandika msg kumuuliza ' nitakuona kesho dia?' akajibu hivi " tutapanga mpz". Nikawasha moto nyumbani hapo, amekili kua ni mpenzi wake ila hawaja sex..... Naombeni ushauri maana sijaamua kitu mpaka sasa, ingawa nimeshatembeza kichapo sana... kuendelea kuishi nae naona sitakua na amani maana hapa nilipo niko dar yeye yuko mkoani.... sina imani nae tena.....
   
 2. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mmh pole sana mkuu Kipusy, hizo ndo ndoa ndoano. Picha yote ushaiona lililopo ni wewe kuangalia zaidi mustakabali wako. Inaonesha kwa asilimia nyingi jamaa kishampitia mkeo na siku hiyo ndo alitoka huko. Angalia mustakabali mzima, kama ni kusamehe usamehe mazima.

  Kumbuka kucheki ngoma, maana upweke ulimshinda mama.
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  aaisee Kipusi una hasira za maamuzi ya haraka saaana.... Yaani na kichapo tayari!! Dah! Enways...

  Miaka mne ni mingi saana kukaa mbali na mwenza, ni hatari kwa afya ya ndoa. Kikubwa ilitakiwa usimtreat kama mtoto mdogo - Maamuzi ya kufanya inategemea saana wewe maamuzi yako kama bado unapenda awe katika maisha yako ama lah! Ukijua nini unataka inatakiwa nae pia ukae nae na kumuuliza na kumwambia kua Ok - Unaelewa kua ana mtu, sasa nini msimamo wake...

  Siku nyingine hata kama una wasi wasi na mtu, akikuambia naumwa.... Toa walau hata pole jamani.. yaani unajibu 'pouwa' kweli... Alafu bana mkeo kisha lala na jamaa ni aibu tu anaona ku admit kwako; hivo chagua kusuka ama kunyoa...
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Pole sana, kwahiyo umeamuaje?
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu, swala la mke na mume ni swala nyeti sana na linataka umakini wa hali ya juu sana kuhamua kesi kama hizo...!

  Kama amekiri kuwa ni mpenzi wake, ila anasema kuwa hajatembea naye, kidogo mashaka... Na jinsi inavyo onesha huyo mke hana heshima na wewe. Kwa sababu angekuwa anakuheshimu hasingekuwa ana cahti na huyo hawara wake na wewe upo ndani ya nyumba.

  Fanya utaratibu uwasilishe mashata kwa wazee wenu au viongozi wa dini...! Au kama una kifua basi fanya utaratibu wa kuwasiliana na huyo mwizi wako na umwambie kile kilichoko moyoni mwako.
   
 6. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #6
  Sep 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu...usiamini anaposema kuwa hawaja sex...kuna mengi atakuwa hajakuambia.
  Mwisho wa siku maamuzi ni yako kama utaendelea nae au unabwaga manyanga na kuanza upya...kila uamuzi una gharama zake.
  Binafsi siwezi kuishi na mwanamke wa hivyo tena.
  Ubarikiwe.
   
 7. l

  luckman JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mtupe pembeni huyo si mwaminifu hata kidogo! Kwa mtu mwenye upendo sioni kama anweza kushindwa kuvumilia ingawa sina uhakika kama hamjado kuw miaka 4 mfululizo, hiyo ni tabia yake sema ulikuwa hujajua!unasoma ili badae uwe na mwelekeo mzuri wa maisha sasa ka mwenzako anajichanganya kitaa na masela mmhhh! Sioni ka kuna mke hapo!
   
 8. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mambo mengine yanatia hasira sana. Haiwezekani unajua nipo unaendelea na jamaa yako ambaye ananyang'anya kabisa nafasi ya mumewe katika ndoa. Hata hajali kuwa mwenzie karudi, yeye anamjali hawara wake. Unaweza mvunja mguu ukaanza kutibia baadaye.
  Inaboa sana, ibiwa sawa, jitahidi basi nisijue, maana ndo staili ya maisha ya sasa hivi wizi wizi tuu.
   
 9. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Raha ya mapenzi ni kuwa na peace of mind na kuwa na imani na mwenzio. sasa pima mwenyewe hapo. moyo wako utakacho amua ndio sahihi kukifanya na sio uambiwe na mwingine kwani wakati unapanga kufunga ndoa hukuwambia watu wakutafutie mchumba. Ni hayo tu..Pole
   
 10. H

  HolySinner Member

  #10
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, pole sana. I feel ur pain. Ingekuwa mimi ningeshamdedisha. Hawa wanawake wa hovyo sana. Lazima atakuwa keshaliwa na huyo jamaa. Hebu tafuta namba ya hilo jizi lako kisha ulipeleleze. Ukilipata lifundishe adabu. Huyo mama mtafutie adhabu zaidi. Kichapo tu hakitoshi
   
 11. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Sio kama miaka 4 yote niko nae mbali ila hua naenda ikizidi sana miezi mi2
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  SIDHANI KAMA ANAMAANISHA HAJAKUTANA NAE MIAKA MINNE,...KWANI DAR NA MIKOANI KUNA UMBALI WA KUSHINDWA KUKUTANA NA MPNZIO,...MM NAFIKIRI MWANANMKE AMEAMUA KUCHEAT TU,...SASA JAMAA AAMUE KUSUKA AMA KUNYOA,...ANYWAY KWANGU MM AMBAYE NI MUUMINI WA MFUMO DUME HAPO NDIO INGEKUA MWISHO WA SALAM

  nb:mfumo dume ninaomaanisha sio sawa na unyanyasaji wa kijinsia_ni ile baba ni kichwa cha nyumba,...wanaharakati plz msinipige mawe
   
 13. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  bado sijaamua ndugu, naumiza kichwa sana, yaani naumia sana, ndio maana nimeweka hapa mnishuri
   
 14. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wanawake bana hatakama ukikuta kajamaa kanamhemea lazima atajitetea eti alikuwa ananilazimisha na wala hajaingiza
  ila cjajua wewe ni dini gani, kama ni mkristo vumilia mkuu kwani alichounganisha mungu mwanadamu hawezi kutengua
  na kama ni muisilam mpe talaka rejea aende akajifunze huko kwa wazazi wake.
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Huyo dada anatia huruma aisee... Hili suala la kutoka nje ya ndoa na kumdharau the hubby kweli kabisa kachemka... Tena sidhani hata kama huyo mwanamume wa nje anampango wa kuishi nae zaidi tu ya kulala nae.... Kashindwa vumilia kwa hizo siku chache attention iwe kwa mumewe... Hata hivo hatuwezi sema saaana maana Mapenzi bana...
   
 16. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Hadhabu gani ndugu, nikiua ntafungwa
   
 17. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Lawama hizi zisingekuwepo kama ungekuwa unaishi na mkeo sehemu moja. Jamani wengine huwa mnawazoesha kutwa mara 3, sasa ikiwa moja baada ya mwaka si unataka lawama tu.
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Haya mambo hayataki maamuzi ya haraka... hasa ukute mhusika anaonekana kujuta! Ila in this case naona mwenzetu ana ma confidence saana.. Na tayari Kipusy kanithibitishia kua wanaonana mara kwa mara... as much as wako mbali...
   
 19. kipusy

  kipusy JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  mimi ni muislam
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Msamehe!
   
Loading...