goriath son
Member
- Jan 20, 2016
- 32
- 32
Wadau nawasalim,
Ninahitaji ushauri wenu ama nimsamehe wife au la kutokana na kitendo chake cha kuikimbia nyumba na kwenda kuishi kanisani
Ipo hivi;
Mwaka 2012 mke wangu alianza kuhudhuria kanisa moja la kilokole baada ya kukaribishwa na rafiki, sisi wote ni walutheri, sikumzuia maana si vibaya mtu kumtafuta mungu ukizingatia kuwa haya makanisa yetu ya main stream (non Pentecostal churches) hayapo deep spiritually zaidi ya kusali kwa mazoea.
Hata hivyo kinyume na matarajio, wife alijiingiza katika kanisa hilo mazima mazima na kujitoa Lutheran kabisa, alishikana urafiki na mama mchungaji, akawa anashinda kwenye kanisa hilo muda wote, ilifika pahala majirani walidhan wife kasafiri kumbe yupo church, mimi ni mfanyabiashara, ni agent mkubwa wa cement, bia, na bidhaa mbali mbali, pia namiliki gesti na bar.
Katika hizo biashara zote yeye wife ndie alikua msimamizi, mimi nikabaki nasimamia biashara moja ambayo huwa inahitaji usimamizi wa karibu sana, cha ajabu baada ya kunogewa na kanisa, akaacha kusimamia biashara za familia na kushinda kwenye maombi na kundi lao la akina mama liliongozwa na mama mchungaji, hivyo biashara zikaanza kwenda mrama, nilipomuuliza kulikoni ulizuka ugomvi mkubwa sana, kwamba natumiwa na ibilisi ndio maana sitaki asali.
Nikaita wazee tulizungumze jambo hilo, bado ikashindikana, baadae akanipa taarifa kwamba kuna ratiba ya mikesha kanisani kila alhamisi, nikamwambia over my dead body, nikamwambia achague moja kati ya ndoa na kanisa, akasema hawezi kufungiwa nira na mtu asieamini, hivyo amechagua kanisa, akabeba vitu vyake vyote na kuamia kanisani, akapewa chumba yeye na wenzie hapo kwa mchungaji na nasikia siku hiyo alipokelewa kama shujaa siku ya sunday kwenye ibada kuu, ambapo walimsifu kuwa ameachana na shetani rasmi, asijali Mungu atampa mume mwingine
Kwa ufupi nikaanza maisha peke yangu na watoto wawili alioowaacha since 2012, tunaendelea vizuri na Mungu ametubariki mara dufu, nikawa nimemfuta kabisa moyoni na kichwani, mwaka jana September nikaanza kuona dalili za ex wife kuanzisha mawasiliano na mimi, mara salam, mara vipi watoto, mara waambie nawapenda sana, etc, birthday yangu akatuma boxer na vest imefungwa vizuri, na kadi na ujumbe, juzi ameniandikia sms ya whatsaap ndefu sana, akafunguka kila kitu.
Kwamba nimsamehe arudi home, alikosea sana, hakujua kuwa wale sio watu wazuri, kuwa tangu tukutane kimwili 2012 hajakuta na mtu mwingine, kuwa ikiwezekana nimruhusu aje home tuyaongee, kwanza hivi sasa yuko kwao ameachana na hilo kanisa.
Taarifa nilizozipata ni kuwa wale wachungaji walimpenda sana mwanzo kutokana na pesa alizokua akiwapa kama zaka na sadaka, ambazo alikua anachukua kwenye biashara zangu, laki tano hadi milion moja anapeleka church kila sunday, na nyingine anachukua ndani na kumpa mama mchungaji, baada ya kuondoka kwangu akawa hana pesa tena, with time yeye ndio akawa anahitaji msaada, ikafika pahala wakamwambia akapange chumba chake nje ya kanisa na afanye hata mama ntilie, ndipo akajiona amesalitiwa na kujitoa lakini tayari damage ni kubwa.
Sasa nimekuja kwenu ili mnipe mawazo maana, siwezi kusema uongo, nilianzisha uhusiano na msichana mmoja hivi anafanya kazi kwenye hii mifuko ya jamii, tuna mwaka sasa, watoto wangu wanampenda na ndugu pia, nilipanga awe ndio replacement, amemaliza masters yake mwaka jana, hiki ndio kikwazo kikubwa, tangu 2012 sikutaka kujiingiza kwenye serious relationship nilikua na buy time huenda kuna siku wife akajirudi, hata hivyo nikachoka kusubiri, amejirudi while its too late.
Your help pls