Mke wangu alibadilika baada ya kumfungulia biashara. Nifanye nini kuokoa ndoa yangu?

Mrudishe kwao hata kwa miezi mitatu, alafu kula mikausho mikali. Alafu yeye mwenyewe atajifunza kama mama yake,hao ndugu zake na hao jamaa zake wanaomtumia meseji wataweza kumhudumia na kumtunza kama ufanyavyo....akirudi atakuwa na funzo la maisha.
Huu ndio ushauri wa kufuata. Mnawachekea sana hawa wanawake. Mie hata nikirudi nyumbani hamna kuongea ongea na simu ukiconcentrate na simu unakula makofi na kurudi kwenu uje na wazazi na maelezo yaliyonyooka

Nikulishe ,nikuvishe nikufungulie biashara nikununulie magari, nitunze ukoo wenu halafu unizingue akili. Silei ujinga hata wanangu wanajua hilo
 
Pole Sana mkuu, Kaaa muongee na mkeo kwanza, muwekane Sawa kuhusu Hilo, ongeza upendo kwa mke wako. Mjali na kuweka ratiba ya kutoka naye out, ukiweza mpitie mrudi naye nyumabn baada ya kaz, pata muda wa kupumzika ili umgonge vizuri. unavyohangaika na hela na ndoa lazima uihangaikie ili kuilinda. Ukiwa makini na ndoa yako hata huyo rafiki yako hawez kupata nafas kwa mkeo.
 
Mada za mapenzi siku hizi zimekuwa nyingi mno alafu wanaume ndio wengi tunaolalamika sana siku hizi hii inasikitisha sana, hawa wanawake siku hizi wamekuwa ni wakuwaumiza wanaume tu sijui tunafeli wapi???
 
Mkuu pole kwa hili, ila halitakiwi kukupa shida sana. Ukweli ni kwamba wake zetu wanatongozwa kila mahali iwe kwenye usafiri, kanisani/msikitini, makazini na mahali pengine popote wanapoweza kukutana na mwanaume. La muhimu ni mke kujua nini maana ya kuwa mke wa mtu na ajielewe. Akitongozwa na kukubali basi ajue anajinajisi yeye, mme wake na familia kwa ujumla.
Kwa mazingira hayo, wacha mke aendelee na biashara, awe makini zaidi na muaminifu pale anapokuwa na changamoto ya namna hii, inayomshinda akushirikishe muitatue pamoja.
Jenga uaminifu na imani kwake na yeye hivyo afanye hivyo kwako pia. Maisha yataendelea kuwa swafi kabisa.
Matatizo mengi ya ndoa yanamalizwa kwa kuzungumza, hivyo hata ninyi zungumzeni. Kukiwa na nia njema kwa kila mmoja wenu, kila kitu kitakaa sawa.
Habari za Jumapili wanajamvi.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.

Mimi na mke wangu tangu tufunge ndoa huu ni mwaka wa tisa. Hatukuwahi kuwa na migogoro mikubwa ingawa mikwaruzano ile midogo ilikuwepo.

Sasa katika kipindi cha miaka sita ya ndoa yetu nilimuweka tu nyumbani sikutaka ajishughulishe na biashara yoyote. Mwaka wa sita wa ndoa yetu nilipata ajali ya pikipiki iliyopelekea mimi kuvunjika baadhi ya viungo vya mwili. Hivyo nilikuwa admitted Muhimbili hospital kwa muda wa kama miezi 3 kabla ya kuruhusiwa.

Kutokana na uwekezeji wangu kwa kipindi chote hiki wakati naugua hatukuwahi kupata Shida ya mahitaji ya nyumbani. Baada ya lile tukio nikajiuliza hivi ikitokea nimefariki Huyu mama ataishije na watoto wangu. Nikamshirikisha nimfungulie biashara ili aanze kujifunza mbinu za utafutaji. Nilipopona tukafungua biashara ya kufanya miamala ya simu na kuuza soft drinks jumla na rejareja.

TATIZO:
Miaka mitatu ya hii biashara imeanza kuniletea matatizo Kwenye ndoa. Wanaume wamekuwa wanapiga simu mpaka Jumapili Siku ambayo wanajua hafanyi biashara na mbaya zaidi kuna mmoja nilikuta SMS za mitongozo na wife alikuwa ameshaingia king. Sasa nilimtafuta yule kijana na kuongea naye ingawa alisema alikuwa hajui kama yule mke wa mtu tangu sasa hatomsumbua tena. Mke wangu yeye alijitetea kuwa alimwambia yule kijana kuwa yeye ameolewa lakini aliendelea kumsumbua tu.

Hivyo nilifunga biashara for a while nikitafakari nini cha kufanya.

NDUGU WA WIFE:

Hawa watu walianza kuongea maneno ya hivyo sana kuwa mimi sitaki maendeleo ya ndugu yao baada ya kuona sasa hivi ameanza kufanikiwa ndio nataka kumrudisha nyuma bila kuangalia kiini cha tatizo.

Wengine mpaka wakadiri kwenda mbali na kusema wao ndio walimpa mtaji niliwauliza ni kiasi gani cha mtaji mlimpa wanasema laki saba. Niliishia kucheka tu kwa sababu hiyo lakini saba haitoshi hata kulipia kodi ya hilo eneo kwa mwaka.

NINACHOOMBA:
Wadau ninachoomba kutoka kwenu ni mawazo jinsi gani niweze kuliweka hili jambo sawa iwe kwa kufunga kabisa biashara yenyewe au vyovyote vile ili mradi ndoa yangu irudi Kwenye amani kama Mwanzo. Mama mkwe amenikasirikia hivyo yeye sioni kama ni mshauri mzuri kwa mke wangu.

Mniwie radhi kwa maelezo marefu ila nitasoma kila comment ili niweze kupata suluhisho.

Ahsante.
 
Huu ndio ushauri wa kufuata. Mnawachekea sana hawa wanawake. Mie hata nikirudi nyumbani hamna kuongea ongea na simu ukiconcentrate na simu unakula makofi na kurudi kwenu uje na wazazi na maelezo yaliyonyooka

Nikulishe ,nikuvishe nikufungulie biashara nikununulie magari, nitunze ukoo wenu halafu unizingue akili. Silei ujinga hata wanangu wanajua hilo
Yes, kumbe wanaume halisi wenye miiko na maadili yetu ya asili ya kiafrika bado wapo? Sikujua hili, hongera kaka umetuwakilisha. Mungu abariki kazi za mikono yako.
 
Kuna amani na utulivu. Inawezekana ndoa yako haikuwa na amani ila ilikiwa na utulivu sababu hukujua tabia ya mkeo. Tabia haina uhusiano na kumfungulia biashara au kushinda nyumbani. Ifahamu tabia ya mkeo, fanya maamuzi kulingana na tabia yake. Kufuga mke ndani hakubadili tabia.
Wanawake wakianza kushika hela huwa wanaanza dharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wanaume wengi tukishaoa tunakua busy Sana na maisha. Mke anahitahi ukaribu, kumjali na tendo la ndoa. Ukijisahau akatokea boya akamfanyia hayo atachukua nafas yako. Lazma tutenge muda kwa ajili ya ndoa. Asilimia kubwa ya ndoa zenye migogoro wanaume hatuzip nafas ndoa. Ila ni muhimu hata Kama mke wako ana tabia gan. Ukimiweka karibu na ukaongeza utundu na ubunifu kwenye tendo anatulia. Ila Kama utaachukulia Hilo Kama Jambo la ziada kikubwa kutafuta maisha, vijana wa mtaani watachukua nafas yako. Na wakigonga wanagonga kweli. Jaman tufanye maisha Ila tutenge muda wa ndoa.
 
Habari za Jumapili wanajamvi.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.

Mimi na mke wangu tangu tufunge ndoa huu ni mwaka wa tisa. Hatukuwahi kuwa na migogoro mikubwa ingawa mikwaruzano ile midogo ilikuwepo.

Sasa katika kipindi cha miaka sita ya ndoa yetu nilimuweka tu nyumbani sikutaka ajishughulishe na biashara yoyote. Mwaka wa sita wa ndoa yetu nilipata ajali ya pikipiki iliyopelekea mimi kuvunjika baadhi ya viungo vya mwili. Hivyo nilikuwa admitted Muhimbili hospital kwa muda wa kama miezi 3 kabla ya kuruhusiwa.

Kutokana na uwekezeji wangu kwa kipindi chote hiki wakati naugua hatukuwahi kupata Shida ya mahitaji ya nyumbani. Baada ya lile tukio nikajiuliza hivi ikitokea nimefariki Huyu mama ataishije na watoto wangu. Nikamshirikisha nimfungulie biashara ili aanze kujifunza mbinu za utafutaji. Nilipopona tukafungua biashara ya kufanya miamala ya simu na kuuza soft drinks jumla na rejareja.

TATIZO:
Miaka mitatu ya hii biashara imeanza kuniletea matatizo Kwenye ndoa. Wanaume wamekuwa wanapiga simu mpaka Jumapili Siku ambayo wanajua hafanyi biashara na mbaya zaidi kuna mmoja nilikuta SMS za mitongozo na wife alikuwa ameshaingia king. Sasa nilimtafuta yule kijana na kuongea naye ingawa alisema alikuwa hajui kama yule mke wa mtu tangu sasa hatomsumbua tena. Mke wangu yeye alijitetea kuwa alimwambia yule kijana kuwa yeye ameolewa lakini aliendelea kumsumbua tu.

Hivyo nilifunga biashara for a while nikitafakari nini cha kufanya.

NDUGU WA WIFE:

Hawa watu walianza kuongea maneno ya hivyo sana kuwa mimi sitaki maendeleo ya ndugu yao baada ya kuona sasa hivi ameanza kufanikiwa ndio nataka kumrudisha nyuma bila kuangalia kiini cha tatizo.

Wengine mpaka wakadiri kwenda mbali na kusema wao ndio walimpa mtaji niliwauliza ni kiasi gani cha mtaji mlimpa wanasema laki saba. Niliishia kucheka tu kwa sababu hiyo lakini saba haitoshi hata kulipia kodi ya hilo eneo kwa mwaka.

NINACHOOMBA:
Wadau ninachoomba kutoka kwenu ni mawazo jinsi gani niweze kuliweka hili jambo sawa iwe kwa kufunga kabisa biashara yenyewe au vyovyote vile ili mradi ndoa yangu irudi Kwenye amani kama Mwanzo. Mama mkwe amenikasirikia hivyo yeye sioni kama ni mshauri mzuri kwa mke wangu.

Mniwie radhi kwa maelezo marefu ila nitasoma kila comment ili niweze kupata suluhisho.

Ahsante.
Kusanya mtaji taratibu na mwisho mwambie umetapeliwa
 
Tatizo wanaume wengi tukishaoa tunakua busy Sana na maisha. Mke anahitahi ukaribu, kumjali na tendo la ndoa. Ukijisahau akatokea boya akamfanyia hayo atachukua nafas yako. Lazma tutenge muda kwa ajili ya ndoa. Asilimia kubwa ya ndoa zenye migogoro wanaume hatuzip nafas ndoa. Ila ni muhimu hata Kama mke wako ana tabia gan. Ukimiweka karibu na ukaongeza utundu na ubunifu kwenye tendo anatulia. Ila Kama utaachukulia Hilo Kama Jambo la ziada kikubwa kutafuta maisha, vijana wa mtaani watachukua nafas yako. Na wakigonga wanagonga kweli. Jaman tufanye maisha Ila tutenge muda wa ndoa.
mtu uangaike juani kulisha na kuitunza familia na kitandani napo ukomae tena duh!
Kweli no body can stop reggae.
 
Mwanamke hatakiwi kuwa na cofidence yoyote ile na akiwa nayo atakusumbua akiwa mzuri atakudharau akiwa na hela atakutishia mpaka ngumi ndo maana wazee wetu walikuwa wanawaweka nyumbani tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom