Mke wa waziri mkuu ni kiongozi wa kitaifa?

Utamu ni hizo POSHO, lazima wajitokeze Nje kuonyesha kuwa walipigwa na JUA na POSHO inahitajika

Mliona picha Mke wa Rais akiwa Comoro na Ndege ya Rais wakibadilishana Saa za Ukutani?
 
Sina tatizo kwa Mama Pinda kuzindua chochote huko Korea maana yuko na mumewe Waziri mkuu na hivyo atakuwa apewa heshma kama Mke wa Waziri Mkuu. Nimeona picha kwenye blogu ya Michuzi na shida yangu ni vaa ya huyu mama hasa hicho kijitambaa alichozungusha kichwani. Anaonekana kama RAPA wa muziki! I think kuna 'National Emblem' kama ukikiangalia vizuri and that makes it look tacky. Hizi posho za mavazi wakubwa wakisafiri nje hapati huyu mama maana kwa jinsi alivyo kwenye picha ni dhahiri anahitaji msaada. Terrible!
 
Viongozi wa CCM wanapo sema wanamuenzi Baba wa Taifa siwaelewi kabisa, Mke wa Kambarage hakuwa na kiherehere kama wake za magamba. Wala mwenyewe Kambarage hakuruhusu mkewe ajifanye kiongozi wa kitaifa. Leo hii magamba na watoto wao wanajifanya ni viongozi wa kitaifa na kutumia rasilimali za Taifa kwa faida zao.

Wake za magamba wana-anzisha NGO pindi magamba yanapochukua madaraka, wanatumia influence hiyo kujipatia misaada mbalimbali kwa kivuli cha NGO hizo. Iko siku watakuja toa majibu ya wanachokifanya sasa.
 
Una lako na mzee Mwinyi, kwani neno "First Lady" kalianzisha yeye? na kama dunia nzima inatambua kuwa mke wa rais ni first lady kwa nini wewe ushangae. nini maana ya first lady, si ndio mwanamke bora kuliko wote katika nchi hiyo, hapo maana yake hakuna hawa ghasia wala makinda hao wote wapo mbali huko. huenda wakawa10th lady huko.mke wa waziri mkuu ni 2nd lady, yaani ni bora kuliko mawaziri wote wanawake na wengine wenye vyeo mbalimbali ukimtoa 1st lady. sasa kama makinda tu ambae si first wala second ana sauti serikalini je first na second si wanaweza hata kumfukuza kazi.
Hata wake wa akina Nyerere, Msuya, Hayati Sokoine, Salim Ahmed Salim, nk wapo lakini hawakuwa na vimbelembele kama tuliwachagua wao kwa kura kutuongoza! Siku hizi mtoto wa Rais, Riz1, licha ya mali za kumwaga alizonazo, anatumia influence ya baba yake kushinikiza masuala mbalimbali ndani ya nchi/chama! Afadhali kule Iringa walikatimua mbio!
 
watu wa iringa walinifurahisha sana kumtimua RIZ1, ni dhahiri washajitambua. kuhusu hili la mke wa Pinda na viongozi wengine nadhani ni ulimbukeni tu na upofu wa viongozi wa leo, s'thing must be done to stop this mapema kabisa
 
Nijiavyo mimi, mkewa kiongozi anayetambuliwa kitaifa ni mke wa rais, japokuwa utambulisho wake ni wa kikatiba. Huyu ndiye ambaye angalau akisafiri na mumuwe anatakiwa kulipwa posho ya safari kama anayolipwa mumewe. Wengine wote hawatambuliki.

Lakini hapa nchini kumezuka ugonjwa wa wake wa viongozi kujifanya nao ni viongozi. Mara utasikia mke wa waziri Mkuu Mizengo Pinda, mara mke wa makamu wa rais na kesho tutasikia mume wa spika. Jamani mke wa waziri mkuu ana nafasi gani katika nchi, hadi asafiri nje ya nchi kwa fedha za umma na kupata fursa ya kuhutubia mikutano kwa niaba ya yetu sisi?


Taifa letu linahiji kuombewa kwa kweli,Mtoto wa mkulima naona hiyo nick name haimfai,Safari zote za kikazi anayetumwa na madaraka tu,na madaraka hayo hayana watu wawili,hivyo si sahii kwa Pinda na mkewe kupewa status moja haikubaliki nchi hii ni ufisadi mtupu,wakihojiwa katika bunge wenzao wanaomba miongozo ya spika juu ya mambo yaliyowazi kabisa.Pinda unatumia vibaya fedha za walipakodi wa TZ,acheni hayo mambo jamani tukisema huku wao wanakimbilia huku utafikiri kambale.hata posho zitaendelea kwa staili hii !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tunahitaji mjadala mpana zaidi kuhusu nafasi za wake wa viongozi wa kitaifa katika ustawi wa taifa letu, tangu nafasi hizo zilipoanza kutumiwa vibaya tumeshuhudia ziara, kauli, maagizo na matamko yasiyo na manufaa kwa Watanzania zaidi ya kutugawa kwa misingi ya vyama vya siasa. Hivi kuna ubaya gani kwa Serikali kutueleza nafasi ya wake wa viongozi wa kitaifa katika uendeshaji wa nchi yetu? Protocol ikoje pale mke wa kiongozi wa kitaifa anapofanya ziara mikoani bila kuandamana na mumewe? hivi anapaswa kupokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa? Hizo ahadi anazotoa anatoa kama nani? Nchi ni yetu sote hii tusinyanyasane jamani....!!!!!
 
Ndio maana ya kuwa shamba la bibi! Nani anamlipia hiyo safari? Kama ni serikali, watuambie kwa nini wanalipa maana yeye sio kiongozi wa serikali.
 
Nijiavyo mimi, mkewa kiongozi anayetambuliwa kitaifa ni mke wa rais, japokuwa utambulisho wake ni wa kikatiba. Huyu ndiye ambaye angalau akisafiri na mumuwe anatakiwa kulipwa posho ya safari kama anayolipwa mumewe. Wengine wote hawatambuliki.

Lakini hapa nchini kumezuka ugonjwa wa wake wa viongozi kujifanya nao ni viongozi. Mara utasikia mke wa waziri Mkuu Mizengo Pinda, mara mke wa makamu wa rais na kesho tutasikia mume wa spika. Jamani mke wa waziri mkuu ana nafasi gani katika nchi, hadi asafiri nje ya nchi kwa fedha za umma na kupata fursa ya kuhutubia mikutano kwa niaba ya yetu sisi?

Naomba hiyo ibara inayomtambua mke wa rais kikatiba tafadhali....
 
nijiavyo mimi, mkewa kiongozi anayetambuliwa kitaifa ni mke wa rais, japokuwa utambulisho wake ni wa kikatiba. Huyu ndiye ambaye angalau akisafiri na mumuwe anatakiwa kulipwa posho ya safari kama anayolipwa mumewe. Wengine wote hawatambuliki.

lakini hapa nchini kumezuka ugonjwa wa wake wa viongozi kujifanya nao ni viongozi. Mara utasikia mke wa waziri mkuu mizengo pinda, mara mke wa makamu wa rais na kesho tutasikia mume wa spika. Jamani mke wa waziri mkuu ana nafasi gani katika nchi, hadi asafiri nje ya nchi kwa fedha za umma na kupata fursa ya kuhutubia mikutano kwa niaba ya yetu sisi?

spanner katiba yetu haiwatambui wake wa viongozi katika mfumo wa uongozi nchini mwetu. Kusafiri nao hilo ni kawaida kiprotocali. Viongozi wetu wanatambulika kama ifuatavyo
1. Rais (ibara ya 33)
2. Makamu wa rais (ibara ya 47)
3. Waziri mkuu (ibara ya 51)
4. Rais wa zanzibar (ibara ya 103)
5. Waziri kiongozi (?)

hiyo ni kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa
 
Nijiavyo mimi, mkewa kiongozi anayetambuliwa kitaifa ni mke wa rais, japokuwa utambulisho wake ni wa kikatiba. Huyu ndiye ambaye angalau akisafiri na mumuwe anatakiwa kulipwa posho ya safari kama anayolipwa mumewe. Wengine wote hawatambuliki.

Lakini hapa nchini kumezuka ugonjwa wa wake wa viongozi kujifanya nao ni viongozi. Mara utasikia mke wa waziri Mkuu Mizengo Pinda, mara mke wa makamu wa rais na kesho tutasikia mume wa spika. Jamani mke wa waziri mkuu ana nafasi gani katika nchi, hadi asafiri nje ya nchi kwa fedha za umma na kupata fursa ya kuhutubia mikutano kwa niaba ya yetu sisi?

Japokuwa sina katiba naamini mke wa Rais hajatajwa hata katika ibara yoyote ya katiba! Mwenye data amwage jamvini hapa! Na kama katiba inatambua uwepo wa mke wa Rais kama kiongozi ni sharti ibadilishwe haraka sana bila kuchelewa.

Kama mke wa Rais si kiongozi wa kitaifa itakuwaje kwa mke wa Waziri Mkuu? Tukiruhusu haya mambo ambayo ni unconstitutional tutajikuta Taifa linatumia gharama kubwa kwa anasa zisizohitajika. Hali hii ikiendelea watoto, vijukuu, vitukuu na hata mbwa wa viongozi nao watakuwa viongozi wa kitaifa.
 
Tuache uzembe wa kufikiri, tujadili mambo ya maana, mara kitambaa kichwani, mara posho za mke wa waziri mkuu, mara Faizafoxy kakosea... hivi mnataka muda wote , watu woote tusifie chadema na mimba ya Josephine!!!! Mnaboa saaaaana
 
Wewe Josephine unaota au umetoka hospital? hivi nani amekupa mandate ya kufokea watu ktk forum hii? who you are by the way? wewe unatofauti gani na hao unawaita wajinga? si uliapa wewe na ukasaliti kiapo. nini tofauti yako na walioapa kuitetea katiba na wanachukua 10% tena kwa maisha baada ya kufa wewe ni hatari zaidi
 
Give me a break man.Kama umeishiwa hoja kaa kimya usinifananishe na wajinga unaowajua na kuwafikiria.Nilitembea na unaemuita Boyfriend wangu kwa pesa yetu tuliyoifanyia kazi wenyewe na si kodi ya mtanzania yeyote.

Yale yalikuwa mapato halali niliyoyafanyia kazi na ilikuwa ni kwa faida yako na ukoo wako wananchi wa kijiji chako wanalia na umasikini,maradhi na umasikini.Watu mmekuwa masikini wa akili kupita maelezo yanavyoelezea, mnatetea upuuzi usiokuwa na kikomo wakati ndugu zenu wanalia na kusaga meno.

Linalozungumzwa ni matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi.Tafuta wapi nimetumia fedha ya chama mimi kama mimi.lete ushahidi hapa ndiyo uondelee kuongea upuuzi.

kuwa na akili yenye miguu miwili inayoweza kutembea na kuonyesha muelekeo,mmekuwa ni watu wa kutetea na kuandika mambo yasiyo na macho kwasababu tu mmpewe kazi acheni kuwa vibaraka,muogopeni Mungu.

Not only that nenda kajifunze suala la mahusiano urudi hapa uandike upuuzi wako.
Mmmmh, bora tujadili hoja iliyopo na si habari ya kumuogopa MUNGU.
With all due respect wewe ni mtarajiwa first lady lakini majibu yako yamekaa kimipasho mipasho, jenga hoja
 
..meli hiyo si mali ya serikali ya Tanzania.

..Waziri Mkuu angeisubiri tu ifike Tanzania na kwenda kuzindua shughuli zake.
 
Naamini wabunge wa CDM wanapitia humu sana tu wanaweza kumuuliza PM ktk maswali ya papo kwa hapo.
Sina hakika lakini si kilakitu lazima kitamkwe kwenye katiba pengine kuna miongozo mingine inamtambua kufanya hivyo
 
Tuache uzembe wa kufikiri, tujadili mambo ya maana, mara kitambaa kichwani, mara posho za mke wa waziri mkuu, mara Faizafoxy kakosea... hivi mnataka muda wote , watu woote tusifie chadema na mimba ya Josephine!!!! Mnaboa saaaaana
Wewe ndo unabore, nani amesema chadema au ccm? Watu anajadili kama ni halali wake wa viongozi wetu kutumia rasimali za nchi kana kwamba na wao ni viongozi.Chadema inakuhangaisha sana mzee? Pole maana ndiyo hali halisi huwezi kuzui maji ya mto yatakuzoa tu.Jadili mada acha kubwatuka! Ukiona watu wanafatilia issue ndogo kama hizi mkuu ujue wamechoka na viongozi hawa. Wangekuwa ni viongozi wanaotimiza wajibu wao hamna mtu angefatilia vitu kama hivi maana vingekuwa vimefunikwa na mazuri mengi! Sasa hivi mkuu mabaya ya viongozi ndo yanayoangaliwa zaidi kuliko mazuri yao maana mabaya ni mengi zaidi.Poleni maana hamna pa kutokea mnatoa macho tukama mjusi aliyebanwa na mlango! Mtachemka sana kwa sababu wenzenu wamewazidi welevu wa kila kitu. Nendeni mkakope akili la sivyo safari yenu ni ngumu sana.
 
Back
Top Bottom