Mke wa waziri mkuu ni kiongozi wa kitaifa?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Nijiavyo mimi, mkewa kiongozi anayetambuliwa kitaifa ni mke wa rais, japokuwa utambulisho wake ni wa kikatiba. Huyu ndiye ambaye angalau akisafiri na mumuwe anatakiwa kulipwa posho ya safari kama anayolipwa mumewe. Wengine wote hawatambuliki.

Lakini hapa nchini kumezuka ugonjwa wa wake wa viongozi kujifanya nao ni viongozi. Mara utasikia mke wa waziri Mkuu Mizengo Pinda, mara mke wa makamu wa rais na kesho tutasikia mume wa spika. Jamani mke wa waziri mkuu ana nafasi gani katika nchi, hadi asafiri nje ya nchi kwa fedha za umma na kupata fursa ya kuhutubia mikutano kwa niaba ya yetu sisi?
 
Inakasirisha wakati mwingine pale bwana mdogo km Ridhwan anapoweza kutumia influence ya kua mtoto wa mkubwa na kubwatukia wazee hovyo pasi kujua kwamba nafasi ya baba ni dhamana tu aliyopewa kwa muda!
 
Acha mke hata watoto wa viongozi ni viongozi siku hizi,ni kawaida siku hizi katika ugomvi wa kawaida kwenye kumbi za starehe kusikia 'unajua mimi ni nani utaumia wewe raia'.
 
Yaani kazi kweli! Yet wansafiri kwa kodi zetu sisi watu walala hoi!

Eti unasikia 1st Lady and ziara Shinyanga na wala hayuko na mumewe.. halafu anapelekwa na ndege ya serikali..na kupokewa na Mkuu wa Mkoa!

Yaani pesa za Wtz zinaliwa kweli!
 
Tunapopiga kura kunakuwa hakuna picha za wake zao,
kama vipi wanataka watambulike basi wakati wa uchaguzi waweke picha za wake zao na tunapompigia kura mume/mke nae anakuwa kiongozi kama ilivyo kwa makamu wa rais,
la sivyo ni ulimbukeni ya kutaka kuiga mambo ya wazungu, First Lady.
Kwanza katiba yetu haimtambui mke/mme wa rais au kiongozi, mimi sijaona kama kuna mtu kaona anihabarishe!
Ni matumizi mabaya ya hela za waTZ
 
Inakasirisha wakati mwingine pale bwana mdogo km Ridhwan anapoweza kutumia influence ya kua mtoto wa mkubwa na kubwatukia wazee hovyo pasi kujua kwamba nafasi ya baba ni dhamana tu aliyopewa kwa muda!

Leta ushahidi, wacha pumba na majungu.
 
Ni mazoea tu, wake za marais walianza kuwa "wasemaji wa Ikulu" tangu enzi za Mzee "Ruksa!" Wakubwa wengine, kama PM, nao wameshaanza kuiga!


Una lako na mzee Mwinyi, kwani neno "First Lady" kalianzisha yeye? na kama dunia nzima inatambua kuwa mke wa rais ni first lady kwa nini wewe ushangae. nini maana ya first lady, si ndio mwanamke bora kuliko wote katika nchi hiyo, hapo maana yake hakuna hawa ghasia wala makinda hao wote wapo mbali huko. huenda wakawa10th lady huko.mke wa waziri mkuu ni 2nd lady, yaani ni bora kuliko mawaziri wote wanawake na wengine wenye vyeo mbalimbali ukimtoa 1st lady. sasa kama makinda tu ambae si first wala second ana sauti serikalini je first na second si wanaweza hata kumfukuza kazi.
 
Nijiavyo mimi, mkewa kiongozi anayetambuliwa kitaifa ni mke wa rais, japokuwa utambulisho wake ni wa kikatiba. Huyu ndiye ambaye angalau akisafiri na mumuwe anatakiwa kulipwa posho ya safari kama anayolipwa mumewe. Wengine wote hawatambuliki.

Lakini hapa nchini kumezuka ugonjwa wa wake wa viongozi kujifanya nao ni viongozi. Mara utasikia mke wa waziri Mkuu Mizengo Pinda, mara mke wa makamu wa rais na kesho tutasikia mume wa spika. Jamani mke wa waziri mkuu ana nafasi gani katika nchi, hadi asafiri nje ya nchi kwa fedha za umma na kupata fursa ya kuhutubia mikutano kwa niaba ya yetu sisi?

anaendaga kufanyaga shoping
 
Hapa tuache mzaha ,inashangaza mke wa waziri mkuu anasafiri nje ya nchi na kuiwakilisha serikali kwa itifaki ipi,great thinkers tunaomba mfafanue kwa faida ya wana jamvini,ili watu wasipotoshe
 
Give me a break man.Kama umeishiwa hoja kaa kimya usinifananishe na wajinga unaowajua na kuwafikiria.Nilitembea na unaemuita Boyfriend wangu kwa pesa yetu tuliyoifanyia kazi wenyewe na si kodi ya mtanzania yeyote.

Yale yalikuwa mapato halali niliyoyafanyia kazi na ilikuwa ni kwa faida yako na ukoo wako wananchi wa kijiji chako wanalia na umasikini,maradhi na umasikini.Watu mmekuwa masikini wa akili kupita maelezo yanavyoelezea, mnatetea upuuzi usiokuwa na kikomo wakati ndugu zenu wanalia na kusaga meno.

Linalozungumzwa ni matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi.Tafuta wapi nimetumia fedha ya chama mimi kama mimi.lete ushahidi hapa ndiyo uondelee kuongea upuuzi.

kuwa na akili yenye miguu miwili inayoweza kutembea na kuonyesha muelekeo,mmekuwa ni watu wa kutetea na kuandika mambo yasiyo na macho kwasababu tu mmpewe kazi acheni kuwa vibaraka,muogopeni Mungu.

Not only that nenda kajifunze suala la mahusiano urudi hapa uandike upuuzi wako.
 
Hata mkeo ni kiongozi wa kitaifa, bila wewe na mkeo na mimi na mume wangu na wengine wote waliopo kutakuwa na Taifa?
.suala hapa ni katiba inasemaje kuhusu mke wa waziri mkuu kuiwakilisha serikali,usitoe majawabu rahisi namna hii. kale chakula ulale
 
Sina tatizo kwa Mama Pinda kuzindua chochote huko Korea maana yuko na mumewe Waziri mkuu na hivyo atakuwa apewa heshma kama Mke wa Waziri Mkuu. Nimeona picha kwenye blogu ya Michuzi na shida yangu ni vaa ya huyu mama hasa hicho kijitambaa alichozungusha kichwani. Anaonekana kama RAPA wa muziki! I think kuna 'National Emblem' kama ukikiangalia vizuri and that makes it look tacky. Hizi posho za mavazi wakubwa wakisafiri nje hapati huyu mama maana kwa jinsi alivyo kwenye picha ni dhahiri anahitaji msaada. Terrible!
 
Kwa ukweli, na kusema lwa kweli FaizaFoxy 'anaboa'.
Pili, kikatiba Spika wa Bunge ni mkubwa wa nne kiudarajia kutoka rais,makamu wa raisi, waziri mkuu, spika wa bunge.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom