Mke wa tajiri yangu ananitaka kimapenzi

RMD

New Member
Aug 24, 2011
3
1
Jamani wadau nisaidieni kwa hili mimi ni house boy nimetolewa kijijini kuja kulisha mifugo ya bosi wangu hapa dar lakini huyu shemeji yangu yaani mke wa bosi wangu ameshanionyesha dalili zote za kunitaka kimapenzi na ameniahidi kuwa ataniamisha na kunitafutia mahali pa kukaa kuliko kusubirli mshahara wa sh 60,000 kwa mwez, na huyu shemeji yangu ameniahidi kunipeleka shule na ameniambia nikithubutu kusema kwa bosi ndio nitajiweka katika hali ngumu zaidi na nitafukuzwa kama mbwa hapa nilipo hii kozi ya computer kanipeleka yeye na kaniahidi nikikubaliana naye atanifanyia mengi mazuri na kinachoniumiza zaidi bosi wangu alishaniambia mwisho wa kazi yangu ni mwezi wa kumi na mbili mwaka huu alinieleza tangu ananichukua nyumbani sasa wadau nipeni ushauli kuhusu huyu shemeji yangu nifanyeje
 
mmmmh! chalii unazali kama la YUSUPH mwana wa yakob! anyway, labda kakanyaga miwaya huyo anatafuta wa kuondoka naye au vinginevyo .........
(houseboy??? 60,000/= per month??? amekupeleka course ya computer? ulikuwa unaijua JF kabla au uliijua baada??)
 
Jamani wadau nisaidieni kwa hili mimi ni house boy nimetolewa kijijini kuja kulisha mifugo ya bosi wangu hapa dar lakini huyu shemeji yangu yaani mke wa bosi wangu ameshanionyesha dalili zote za kunitaka kimapenzi na ameniahidi kuwa ataniamisha na kunitafutia mahali pa kukaa kuliko kusubirli mshahara wa sh 60,000 kwa mwez, na huyu shemeji yangu ameniahidi kunipeleka shule na ameniambia nikithubutu kusema kwa bosi ndio nitajiweka katika hali ngumu zaidi na nitafukuzwa kama mbwa hapa nilipo hii kozi ya computer kanipeleka yeye na kaniahidi nikikubaliana naye atanifanyia mengi mazuri na kinachoniumiza zaidi bosi wangu alishaniambia mwisho wa kazi yangu ni mwezi wa kumi na mbili mwaka huu alinieleza tangu ananichukua nyumbani sasa wadau nipeni ushauli kuhusu huyu shemeji yangu nifanyeje
Hii story ina uwalakini
 
Wewe kaka kama ni hous boy mwezi kuijua jamii forums na una access ya mtandao basi ongera sana.
Tumia akili yako kuchagua baya na zuri ukilinganisha na ulikotoka na unakokwenda.
 
kimbia.
kuwa km yusufu kwa mke wa farao.
pole.

Rose1980_acha kunfundisha uoga kijana,..kwanza ndio kafika mjini sasa anataka aonje mazuri ya town_hapa ni kumwambia tu kwamba yana shubiri zake,..ila athinki tanki_kama itamlipa achukue na kama ni how come basi apotezee mazee.....kumbuka anatafuta mtaji wa maisha huyo na hii ni golden chance kwake
 
Hii story ina uwalakini

Je alipolekwa kwenye course mume hajauliza ni kwa nini aache kazi za kulisha ng'ombe akasome na ni nani aliyempa ruhusa ya kwenda kusoma wakati aliletwa kwa kazi nyingine
House boy mjanja sana na mpaka katoka kijijini muda mfupi sana ila ashaijua JF na anajua kutumia mtandao kwa kwenda mbele
 
haswaaa! mke wa bosi ni bosi wako pia, jina shemeji ni mazingira ya kazi tu! ila hii story haijakaa uzuri. au labda mleta mada anajua kisa cha houseboy akaamua kujivika uhusika, vinginevyo mazingira ya TZ houseboy na JF ni maji na mafuta.

sawa sawa...ila kastory kazuri mkuu
 
Heheheh houseboy umekuja kuchunga mifugo mpaka unaingia kwenye internet na kupost jamiiforums?! Ama kweli dunia ni kijiji!
 
Duuh huyo houseboy ni noumer, yaani mwezi na JF keshaijua? Mie nimeanza kutumia mtandao miaka 6 iliopita na nimekuja kujua kuwa kunakitu kinaitwa JF mwaka huu, yeye mwezi tu....

Nahisi hapa naibiwa kiingilio.
 
Najua kwenye ndoa kuna matatizo kibao, lakini kuchukulia hiyo gea ulale na mke wa mtu ni hatari, unaweza kujiona unafaida lakini athari zake kwako ni kubwa pengine kuliko hata huyo unayemchulia mke. Unaweza kujikuta maisha yako usipende tena kutafuta mwanamke wako ukawa mzee wa wake za watu. Kuwa makini kijana.

Ukishindwa kuchambua pumba na mchele hapa basi usisahau kuvaa kinga. Hakikisha unakuwa nazo kuanzia sasa, uwe unajaribu kuzivaa isijefika siku ya siku hujui.
 
"Mimi ni house.." .... "Mke wa bosi wangu"..... "shemeji yangu.."

Ama kweli "Upumbavu ni KIPAJI"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom