Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Tumeona taarifa juu ya ma-kontaina ya pembe za ndovu kupitishwa bandarini Dar es Salaam na kukamatiwa nje ambako hakuna ufisadi kama wetu. Wengi wanajiuliza, inawezekana vipi maofisa wa TRA na Bandari kufumbia macho kitu kama hicho? Je, wanapaswa kulaumiwa?
Nitawaambia juu ya kisa cha kweli kilichotokea katika mojawapo ya awamu za maraisi wetu (sio Nyerere, hilo nawahakikishieni). Makonteina kadhaa toka nje yalifika bandari Dar es Salaam. Bandari na TRA wakaamuru yasitoke hadi yamekaguliwa ipasavyo na ushuru kutozwa, sio tu kwa kusoma Bill of Lading.
Ofisa wa Bandari akaitwa Ikulu. Akaambiwa na mke wa raisi, wewe una jeuri sana. Kwani hujaona Bill of Lading, unataka kukagua nini? Siku hiyo ilikuwa Jumamosi. Akaambiwa ikifika Jumatatu makontaina hayajatoka nitakushughulikia ili ujue mimi ni nani katika nchi hii.
Ofisa wa bandari akawataarifu wakuu wenzake na kuomba ushauri. Wakamwambia bwana, kayatoe makonteina. Usijali nyaraka au taratibu za kuyatoa, wewe chukua watu, pakia konteina hizo kwenye magari zitoe nje ya bandari na muulize mama anataka zikashushiwe wapi. Itabidi usimamie zoezi hili mwenyewe, na walinzi wote waeleze yanatoka kwa ruhusa yako.
Ungekuwa wewe ndiye kiongozi wa bandari, ungefanya nini?