Mke wa Raisi anapoamrisha kiongozi wa serikali kuvunja sheria; wewe ungefanyaje?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,566
Tumeona taarifa juu ya ma-kontaina ya pembe za ndovu kupitishwa bandarini Dar es Salaam na kukamatiwa nje ambako hakuna ufisadi kama wetu. Wengi wanajiuliza, inawezekana vipi maofisa wa TRA na Bandari kufumbia macho kitu kama hicho? Je, wanapaswa kulaumiwa?

Nitawaambia juu ya kisa cha kweli kilichotokea katika mojawapo ya awamu za maraisi wetu (sio Nyerere, hilo nawahakikishieni). Makonteina kadhaa toka nje yalifika bandari Dar es Salaam. Bandari na TRA wakaamuru yasitoke hadi yamekaguliwa ipasavyo na ushuru kutozwa, sio tu kwa kusoma Bill of Lading.

Ofisa wa Bandari akaitwa Ikulu. Akaambiwa na mke wa raisi, wewe una jeuri sana. Kwani hujaona Bill of Lading, unataka kukagua nini? Siku hiyo ilikuwa Jumamosi. Akaambiwa ikifika Jumatatu makontaina hayajatoka nitakushughulikia ili ujue mimi ni nani katika nchi hii.

Ofisa wa bandari akawataarifu wakuu wenzake na kuomba ushauri. Wakamwambia bwana, kayatoe makonteina. Usijali nyaraka au taratibu za kuyatoa, wewe chukua watu, pakia konteina hizo kwenye magari zitoe nje ya bandari na muulize mama anataka zikashushiwe wapi. Itabidi usimamie zoezi hili mwenyewe, na walinzi wote waeleze yanatoka kwa ruhusa yako.

Ungekuwa wewe ndiye kiongozi wa bandari, ungefanya nini?
 
Kwa sababu system zetu hazifanyi kazi ipasavyo (ndio maana mama ikulu nae ana mamlaka, tena yaliyo negative), kama hataki kuhamishiwa bandari ya Mtwara, basi kiongozi wa bandari ataweza kushiriki hata 'kusembua' yanapotakiwa kwenda kupumzika hayo makontena.

Siamini kama kuna ujasiri uliosalia wa viongozi wetu kusema siruhusu makontena kutoka, na kama aking'ang'anizwa basi aache kazi!
 
Ndio maana ya separation of power...nchi zetu hizi bado watu hawajui wajibu wao. Wanafikiri utumishi wa umma ni kuhakikisha maboss wanafurahi hata kama wanavunja sheria.
 
tumeona taarifa juu ya ma-kontaina ya pembe za ndovu kupitishwa bandarini dar es salaam na kukamatiwa nje ambako hakuna ufisadi kama wetu. Wengi wanajiuliza, inawezekana vipi maofisa wa tra na bandari kufumbia macho kitu kama hicho? Je, wanapaswa kulaumiwa?

Nitawaambia juu ya kisa cha kweli kilichotokea katika mojawapo ya awamu za maraisi wetu (sio nyerere, hilo nawahakikishieni). Makonteina kadhaa toka nje yalifika bandari dar es salaam. Bandari na tra wakaamuru yasitoke hadi yamekaguliwa ipasavyo na ushuru kutozwa, sio tu kwa kusoma bill of lading.

Ofisa wa bandari akaitwa ikulu. Akaambiwa na mke wa raisi, wewe una jeuri sana. Kwani hujaona bill of lading, unataka kukagua nini? Siku hiyo ilikuwa jumamosi. Akaambiwa ikifika jumatatu makontaina hayajatoka nitakushughulikia ili ujue mimi ni nani katika nchi hii.

Ofisa wa bandari akawataarifu wakuu wenzake na kuomba ushauri. Wakamwambia bwana, kayatoe makonteina. Usijali nyaraka au taratibu za kuyatoa, wewe chukua watu, pakia konteina hizo kwenye magari zitoe nje ya bandari na muulize mama anataka zikashushiwe wapi. Itabidi usimamie zoezi hili mwenyewe, na walinzi wote waeleze yanatoka kwa ruhusa yako.

Ungekuwa wewe ndiye kiongozi wa bandari, ungefanya nini?
nachungulia makontena yana nini ndani kisha nayaachia.inabakia kuwa siri yangu kichwani kwamba mke wa rais ni hatari.
 
jamani afrika tuna wake wa marais kwa ajili ya heshima tu ya rais yaani utamaduni tu. hawana lolote hawawezi hata kushauri vitu vidogo vyenye manufaa kwa nchi. ukitaka kujua hilo angalia mama mugabe,museven,kibaki endeleza.
 
inaelekea ni wewe na sasa Mwakyembe kakuweka katika list ya aibaji humo ndo unatafuta cha kujitetea. ulikuwa wapi miaka yote kuuliza. unaogopa nini si useme ilikuwa lini tutapiga mahesabu wenyewe. unaogopa nini na kazi ndio inataka kukukimbia.

nasema hivi maana sioni umuhimu wa wewe kuja sasa kuomba ushauri as nilidhani unatupa story tu tumjue etc
 
Mkuu kwanza tuwekee jina lake hapa, vinginevyo wewe ni mnafiki na mpiga majungu. Unaficha nini kama awamu yake ilishapita, na unaogopa nini ilihali umeshasema kwamba suala lilijadiliwa na maofisa wengine, yeye atajuaje kama aliyeleta taarifa hizi si mmoja wa maofisa walisimuliwa. Tupe jina la huyo mke wa Rais mwizi!

Na pili ningekuwa mimi ningezuia hayo makonteina yasitoke, halafu ningeandika barua ya kujiuzuru wadhifa wangu ndani ya masaa 24 na kueleza kwa ufasaha kila kitu kilichojiri hadi kupelekea kujiuzuru. Kopi ya barua ningeipeleka kwenye vyombo vyote vya habari vya ndani na nje ya nchi. Halafu siku inayofuata ningekuwa Kenya au Uganda kwa mapumziko.

Kwa level ya ofisa wa bandari lazima alikuwa na vihela vya kutosha kumuweka kwenye hotel pale Kenya au Uganda kwa angalau wiki mbili akisikilizia hali ya mambo inavyoendelea.

Katika hilo, naamini ningekuwa na jeuri zaidi yake, nisingekubali kabisa kuburuzwa. Hayupo aliye mkuu kuwashinda watanzania. Kama watanzania wangejua ukweli huo, naamini wangenilinda, na yeye u-mke wa rais wake ungekuwa kwenye wakati mgumu.
 
Tumeona taarifa juu ya ma-kontaina ya pembe za ndovu kupitishwa bandarini Dar es Salaam na kukamatiwa nje ambako hakuna ufisadi kama wetu. Wengi wanajiuliza, inawezekana vipi maofisa wa TRA na Bandari kufumbia macho kitu kama hicho? Je, wanapaswa kulaumiwa?

Nitawaambia juu ya kisa cha kweli kilichotokea katika mojawapo ya awamu za maraisi wetu (sio Nyerere, hilo nawahakikishieni). Makonteina kadhaa toka nje yalifika bandari Dar es Salaam. Bandari na TRA wakaamuru yasitoke hadi yamekaguliwa ipasavyo na ushuru kutozwa, sio tu kwa kusoma Bill of Lading.

Ofisa wa Bandari akaitwa Ikulu. Akaambiwa na mke wa raisi, wewe una jeuri sana. Kwani hujaona Bill of Lading, unataka kukagua nini? Siku hiyo ilikuwa Jumamosi. Akaambiwa ikifika Jumatatu makontaina hayajatoka nitakushughulikia ili ujue mimi ni nani katika nchi hii.

Ofisa wa bandari akawataarifu wakuu wenzake na kuomba ushauri. Wakamwambia bwana, kayatoe makonteina. Usijali nyaraka au taratibu za kuyatoa, wewe chukua watu, pakia konteina hizo kwenye magari zitoe nje ya bandari na muulize mama anataka zikashushiwe wapi. Itabidi usimamie zoezi hili mwenyewe, na walinzi wote waeleze yanatoka kwa ruhusa yako.

Ungekuwa wewe ndiye kiongozi wa bandari, ungefanya nini?
sidhani kama hili jambo lina ukweli ndani yake
kwa uzoefu nilionao ref income tax act second schedule president ana tax exemption
ina wezekana watu wa custom waliona mzigo unajina la mheshimiwa wakauacha tena wantakiwa wapewe taarifa kwa maandishi!
lakini mpaka uwe na jina la mtu ambaye anatakiwa kua exempeted,hayo mengine aliyoeleza jamaa ya kutishwa mm sielewi wa sidhani yapo kwa zama hizi labda zamani zama za ujinga
 
Unarekodi mazungumzo ya huyo mke wa rais na unamwambia ukweli kuwa haiwezekani kwa namna yoyote ile makontena yakatoka kwa namna anayotaka yeye.
Kwa lolote litakalotokea unaliweka kwenye vyombo vya habari na inakuwa kashfa kubwa tu kwake.
 
Anatakiwa asimamie utaratibu wa kazi asisimamie tumbo lake. Kama huwa anapiga deal zake/kama ni mchafu/si msafi pia basi na hilo itabidi aliachie. Kama anaamini yupo safi basi asimamie sheria.
 
Tumeona taarifa juu ya ma-kontaina ya pembe za ndovu kupitishwa bandarini Dar es Salaam na kukamatiwa nje ambako hakuna ufisadi kama wetu. Wengi wanajiuliza, inawezekana vipi maofisa wa TRA na Bandari kufumbia macho kitu kama hicho? Je, wanapaswa kulaumiwa?

Nitawaambia juu ya kisa cha kweli kilichotokea katika mojawapo ya awamu za maraisi wetu (sio Nyerere, hilo nawahakikishieni). Makonteina kadhaa toka nje yalifika bandari Dar es Salaam. Bandari na TRA wakaamuru yasitoke hadi yamekaguliwa ipasavyo na ushuru kutozwa, sio tu kwa kusoma Bill of Lading.

Ofisa wa Bandari akaitwa Ikulu. Akaambiwa na mke wa raisi, wewe una jeuri sana. Kwani hujaona Bill of Lading, unataka kukagua nini? Siku hiyo ilikuwa Jumamosi. Akaambiwa ikifika Jumatatu makontaina hayajatoka nitakushughulikia ili ujue mimi ni nani katika nchi hii.

Ofisa wa bandari akawataarifu wakuu wenzake na kuomba ushauri. Wakamwambia bwana, kayatoe makonteina. Usijali nyaraka au taratibu za kuyatoa, wewe chukua watu, pakia konteina hizo kwenye magari zitoe nje ya bandari na muulize mama anataka zikashushiwe wapi. Itabidi usimamie zoezi hili mwenyewe, na walinzi wote waeleze yanatoka kwa ruhusa yako.

Ungekuwa wewe ndiye kiongozi wa bandari, ungefanya nini?

Ningemwita mtu jasiri kama A. L. Mrema.
 
jamani afrika tuna wake wa marais kwa ajili ya heshima tu ya rais yaani utamaduni tu. hawana lolote hawawezi hata kushauri vitu vidogo vyenye manufaa kwa nchi. ukitaka kujua hilo angalia mama mugabe,museven,kibaki endeleza.

Mkuu Ligendayika, unayosema na uhalisi ni mambo mawili tofauti. Katika awamu fulani ya uongozi, mke wa raisi alipewa nafasi ya kupendekeza majina katika baraza la mawaziri! Katika awamu nyingine, mke aliamrisha mtu ateuliwe kuwa mkurugenzi katika wizara, japo ndio kwanza alikuwa ametoka kumaliza shule na kupata Masters degree, akawapiku wengi tu waliostahili hiyo nafasi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom