Mke wa Rais wa zamani wa Ivory Coast aasisi harakati ya kisiasa

jollyman91

Member
Sep 21, 2021
69
29
Mke wa Rais wa zamani wa Ivory Coast Bi Simone Gbagbo leo ameshiriki katika uzinduzi wa harakati ya kisiasa, ikiwa ni hatua moja kuelekea kuasisi chama chake cha siasa kwa ajili ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2025.

Simone Gbagbo ametilia mkazo mwelekeo wake wa kuwa na "Kodivaa yenye nguvu, iliyo huru, yenye mapatana, ya kisasa na yenye mafanikio" chini ya kauli mbiu ya "umoja, nidhamu na kazi." Akizungumza wakati wa kuzindua harakati yake ya kisiasa Simeone Ggagbo amewatolea wito wananchi wa Ivory Coast kuwa watendaji wenye bidii na wanaoweza kusamehe na kupatana.

4bseff5995f96b1cs2u_800C450.jpg
Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo

Itakumbukwa kuwa, Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo alirejea Abidjan mji mkuu wa nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu akiwa na mwanamke mwingine alitetajwa kwa jina la Nady Bamba ambaye amekuwa mwenza wake tangu mwanzoni mwaka mwaka 2000; na kisha akawasilisha ombi la kumtaliki aliyekuwa mkewe Bi Simone Gbagbo.

Kwa upande wake Laurent Gbagbo amesema kuwa ana mpango wa kuanzisha chama chake kipya mwezi Oktoba mwaka huu. Hata hivyo wafuasi wa Bi Simone wanasema kuwa ni vigumu sana kuwatenganisha wawili hao kisiasa. Wamesema kuwa Bi Simone Gbagbo anajua vyema siasa na ameshiriki pakubwa pamoja na muwewe katika harakati za kisiasa nchini Ivory Coast.

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo alirejea nchini humo mwezi Juni mwaka huu baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kumfutia kesi iliyokuwa ikimkabili ya kutenda jinai za kivita na dhidi ya binadamu.
 
Back
Top Bottom