Mke wa Rais wa Syria kufunguliwa mashtaka nchini Uingereza

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Miaka 10 tangu kuanza kwa mapigano nchini Syria, Mke wa dikteta na rais wa Syria, Bashar al-Assad, Asma al-Assad anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu na kushawishi uhalifu dhidi ya wananchi wa Syria, mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake nchini Uingereza.

Asma ambaye ana uraia pacha wa Syria na Uingereza anatakiwa kujibu mashtaka hayo mbele ya mahakama ya Uingereza, ambapo mashtaka dhidi yake yameandaliwa na mawakili wa Kampuni binafsi inayotoa huduma za kisheria ya nchini Uingereza.

"Ni muhimu kuwawajibisha si wale tu waliohusika kutenda matendo maovu ya ukatili dhidi ya binadamu, lakini pia wale waliohusika kuchochea, kutukuza na kushawishi matendo hayo. Tunahakikisha kuwa wa haki na kweli inafikiwa kwa wote waliohusika bila kujali hadhi zao," taarifa ya kampuni hiyo ya sheria ilieleza.

Kampuni hiyo inasema haitakuwa vyema kumyang'anya uraia wa Uingereza Asma bila kumchukulia hatua zingine za kisheria, ikisisitiza kuwa anatakiwa kujibu mashtaka yanayomkabili "kupitia mchakato huru wa kisheria."

Syria inatuhumiwa kwa mauaji na utesaji wa wananchi. Kampuni hiyo inasema, ikiwa na ushahidi wa watu wengi, kuwa mamlaka za Syria zimetumia nguvu kubwa dhidi ya waandamanaji, ikiwamo matumizi ya silaha za sumu za kemikali, ukamataji holela wa watu wengi na kuwafyatulia risasi za moto waandamanaji.

Mwezi Machi mwaka 2011, wakishawishiwa na mwenendo wa matukio nchini Misri na Tunisia, wananchi wa Syria waliinuka kupinga utawala wa rais Bashar al-Assad, wakitaka mageuzi na uhuru. Maandamano yaliyoanza kwa amani yaligeuka mapigano ya kumwaga damu pale utawala wa Assad ulipowalazimisha wananchi kuchukua silaha kutetea uhai wao.

Miaka 10 baadaye, hali ya amani haijarejea nchini humo huku kukikosekana suluhu ya moja kwa moja ya vurugu nchini Syria. Mapigano hayo yamesababisha nusu milioni ya Wasyria kupoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni 12 wakiyakimbia makazi yao kutafuta hifadhi katika makambi ya wakimbizi ndani ya nchi na nje ya nchi hiyo.

Chanzo: Anadolu Agency
 
Back
Top Bottom