Mke wa Rais ana madaraka gani hapa nchini?

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Wakuu, leo (7/10/2011) mchana nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa marafiki zangu ambaye ana taasisi ndogo ambayo wiki chache kutoka sasa itakayosherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa. Akanijulisha kuwa kwa sababu inashughulika na masuala ya wanawake aliona vyema kumwalika Salma Kikwete kama mgeni rasmi.

Kilichonistaajabisha ni kwamba alipowasiliana na ofisi yake moja ya masharti aliyopewa ya mama huyu kuhudhuria ni kwamba lazima DC aalikwe pamoja na watu wengine wawili watatu wa kiserikali.

Swali ni je, katiba, sheria na itifaki zinasemaje kuhusu jambo la namna hii? Isitoshe huyu mama anaendeshwa kwenye msafara na gari yake ina ngao ya nchi wakati hana mamlaka yoyote yanayompa haki ya kutumia ngao.

Naomba kuwasilisha.
 
its a million dollar question....

siyo kila kitu kiandikwe kisheria....kwenye nchi kuna tamaduni na mazoea ambayo wenye nchi hujiwekea...
 
Ni mwenyekiti wa WAMA! Cha ajabu hapo ni nini? Huenda huo ni utaratibu wake aliojiwekea. Mbona Reginald Mengi amejiwekea utaratibu kwamba kama anakupa msaaada lazima uende na waandishi wa habari ili hali Bhakhresa hata akitoa msaada wa mamilioni haonekani kwenye vyombo vya habati. Nadhani ni kautaratibu tu na jamaa yako angekatimiza tu hako kautaratibu tu basi apate hudhurio la First Lady!
 
its a million dollar question....

siyo kila kitu kiandikwe kisheria....kwenye nchi kuna tamaduni na mazoea ambayo wenye nchi hujiwekea...
ni kweli mkuu ila mazoea kama haya hayana budi kukomeshwa mara moja
 
We haujui mbwa wa boss wako naye ni boss wako? Vivyo hivyo mke wa raisi ni raisi.
 
Kweli haya ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi.Kimsingi hana mamlaka yoyote ni hulka na ulimbukeni wa hawa wake za maraisi kudhani kuwa wanauwezo wa kufanya jua liwake usikukisa wanaishi ikulu.
 
Ni mwenyekiti wa WAMA! Cha ajabu hapo ni nini? Huenda huo ni utaratibu wake aliojiwekea. Mbona Reginald Mengi amejiwekea utaratibu kwamba kama anakupa msaaada lazima uende na waandishi wa habari ili hali Bhakhresa hata akitoa msaada wa mamilioni haonekani kwenye vyombo vya habati. Nadhani ni kautaratibu tu na jamaa yako angekatimiza tu hako kautaratibu tu basi apate hudhurio la First Lady!

post yako ina chembe chembe za udini
 
Wakuu, leo (7/10/2011) mchana nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa marafiki zangu ambaye ana taasisi ndogo ambayo wiki chache kutoka sasa itakayosherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa.
Akanijulisha kuwa kwa sababu inashughulika na masuala ya wanawake aliona vyema kumwalika Salma Kikwete kama mgeni rasmi.
Kilichonistaajabisha ni kwamba alipowasiliana na ofisi yake moja ya masharti aliyopewa ya mama huyu kuhudhuria ni kwamba lazima DC aalikwe pamoja na watu wengine wawili watatu wa kiserikali.
Swali ni je, katiba, sheria na itifaki zinasemaje kuhusu jambo la namna hii? Isitoshe huyu mama anaendeshwa kwenye msafara na gari yake ina ngao ya nchi wakati hana mamlaka yoyote yanayompa haki ya kutumia ngao.
Naomba kuwasilisha.

nafasi ya mwanamke wa ikulu ni kubwa, licha ya kwamba haijatajwa kwenye katiba.
 
Kile ni kiburudisho cha kikwete tu basi...... Kwanza hata huyo kikwete mwenyewe hana mamlaka yeyote mana hamna mwananch aliyemchagua!!!

kikwete ni rais wa nchi kiutaratibu mke wake nae ana kiasi fulani cha mamlaka so lazima wamuenzi kama mke wa rais na huu utaratibu upo dunia nzima
 
Back
Top Bottom