LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 14,937
- 26,644
AMA kweli haki hakuna. Katika hali ya kusikitisha, kijana mmoja Elias John, mkazi wa Kigamboni jijini Dar ( 28 ) amejikuta katika wakati mgumu wa kupofuka baada ya kuchomwa sindano inayo daiwa kuwa na sumu kufuatia kujihusisha kimapenzi na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mke wa askari Polisi.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar Es salaam, Elias alidai alikumbwa na mkasa huo mwaka 2011 wakati akiwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo aliyemtaja kwa jina moja la Amina, ambaye pia alikuwa ni mke wa polisi aliyemtaja kwa jina moja la James, aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Polisi Kilwa Road, Jijini Dar es salaam.
" Polisi huyo alikuwa akinifuata mara kwa mara na kuniambia kuwa niachane na mwanamke huyo, lakini kwangi ilikuwa ngumu kwa sababu tulipendana sana " alisema kijana huyo.
Alisema siku ya tukio, akiwa kijiweni, polisi huyo akiambatana na wenzake walifika na kumkamata bila kosa lolote na kumpeleka katika kituo kidogo cha polisi Mianzini, Temeke.
Wakiwa kituoni hapo, kijana huyo alisema kwa pamoja walimshika mikono na miguu wakai James alichukua sindano na kumchoma.
Akiwa hajui hatma yake, Elias alisema mara tu baada ya kuchomwa sindano hiyo alisikia maumivu makali yaliyopanda hadi kichwani na ghafla akapoteza uwezo wake wa kuona.
" Siwezi kuelezea zaidi maumivu niliyoyapata baada ya kuchomwa sindano ile na hapo hapo macho yangu hayakuweza kuona tena licha ya kujitaidi sana '
Alisema baada ya kuchomwa sindano hiyo, askari hao walimtaka aondoke na akajitaidi kuwapa taarifa ndugu
zake, ambao walimchukua na kumpeleka Muhimbili ambako hata hivyo walishindwa kumsaidia na hata alipopelekwa CCBRT, pia ilishindikana.
Katika hali ya kusikitisha zaidi, ndugu z ake walijaribu kufuatilia suala hilo polisi, lakini walipofika waliambiwa kirahisi kwamba askari wote hao walishafukuzwa kazi.
Alisema juhudi za ndugu zake kuhakikisha haki inatendeka zimegonga mwamba licha ya suala lake kufikishwa kwa taasisi za haki za binadamu, ambako bado linashughulikiwa, ingawa hakuna matumaini ya kupatikana kwa ufumbuzi.
" Maisha yangu yamekuwa magumu sana na sijui hatma ya kesi yangu, nitaendelea kuishi hivi mpaka lini ? kwa vile kwa sasa naomba omba tu " alisema. Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuliangalia suala lake kwa undani ili lipatiwe ufumbuzi .
CHANZO : GAZETI LA AMANI,, DESEMBA 12, 2013.
MY TAKE : THE DEVIL SHOULD NOT BE TREATED GENTLY! A MAN WHO SLEEP WITH ANOTHER MAN'S WIFE, IS THE DEVIL AND THEREFORE SHOULD BE TREATED ACCORDINGLY!