SI KWELI Mke wa Ngolo Kanté aliomba talaka ili apate mali lakini aambulia patupu

SI KWELI Mke wa Ngolo Kanté aliomba talaka ili apate mali lakini aambulia patupu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu hii taarfa inasambaa sana kupitita mitandao ya kijamii uhalisia wake ni upi?

Just 6 days before the World Cup kickoff, N’Golo Kanté’s French wife announced she was filing for divorce, believing that under French law their assets would be split 50/50 regardless of the circumstances.

However, during the court proceedings, it was later revealed that Kanté had no assets in France, while his properties and wealth in his home country were registered in the names of his twin children.

As it stands, Kanté is now the one entitled to receive a share of her assets. After hearing the outcome, she immediately wanted to call off the divorce, but the verdict had already been passed
1780899521545.png

1780827066672.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo X, Facebook na Instagram kumekuwapo taarifa inayosambaa ikieleza:

"Siku sita tu kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, mke Mfaransa wa N’Golo Kanté alitangaza kuwa anataka talaka, akiamini kwamba chini ya sheria za Ufaransa mali za wanandoa zingegawanywa kwa usawa wa asilimia 50 kwa 50 bila kujali mazingira.

Hata hivyo, wakati kesi ya talaka ikiendelea mahakamani, ilibainika kuwa Kanté hakuwa na mali yoyote iliyosajiliwa nchini Ufaransa. Badala yake, mali na utajiri wake katika nchi yake ya asili vilikuwa vimesajiliwa kwa majina ya watoto wake mapacha.

Kutokana na hali hiyo, Kanté ndiye aliyekuwa na haki ya kupata sehemu ya mali za mke wake. Baada ya kusikia uamuzi huo, mke wake alitaka kufuta mchakato wa talaka, lakini ilikuwa ameshachelewa kwa sababu hukumu ilikuwa imeshatolewa."


Uhalisa wa madai

JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kupitia zana za kidigitali na kubaini kuwa madai hayo yamezuka angalau kuanzia Juni 5, 2026.

Lakini, madai hayo yamechapishwa katika kurasa binafsi za watumiaji wa mitandao ya kijamii tena wote wakiwa wameandika katika mtindo mmoja bila kuhariri chochote. Ufuatiliaji umebaini kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.

Maisha ya Ngolo yamekuwa ya siri sana na hivyo kupelekea mambo yake mengi kutokuwa hadharani, hivyo haipo wazi pia kuhusu mwanamke aliye naye kwenye mahusiano ama kuwa na watoto mapacha kama taarifa zilizozuka zinavyoeleza.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa Ngolo amewaandikisha majina watoto wake mapacha ni madai yanayorejelea picha ya siku nyingi ambayo Ngolo alipiga alipokuwa Mali na kudaiwa kuwa ni wanawe lakini uhalisia ni kuwa hawakuwa watoto wake bali ni wa ndugu yake.

Hivyo JamiiCheck imehitimisha kuwa madai haya ni ya kubuni kufuatia baadhi ya madai halisi yaliyowahi kuwepo, mathalani madai maarufu yaliyoeandana na haya ni yale ya mchezaji Achraf Hakimi mwaka 2023. Soma zaidi hapa.
Back
Top Bottom