Mke wa Mzee Majuto afukuzwa aomba msaada kwa watanzania

Basi Nenda

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
20,151
45,817
Mke wa marehemu Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto amesema kuwa amefukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mume wake jijini Tanga maeneo la Donge.

Amesema kuwa watoto wa marehemu pamoja na Ndugu wa Mzee Majuto ‘wamemfukuza’ wakidai kuwa hawana pesa za kumsaidia hivyo ajisaidie mwenyewe kupitia pesa za pole anazopata toka kwa watu.

”Toka amekufa marehemu mume wangu hakuna mtu yeyote amenisaidia zaidi ya Watanzania na marafiki wa marehemu” amesema mke wa Majuto.

Yapata siku 12 tangu mwigizaji Mzee Majuto afariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mke wake ambae walizaa watoto wanne ameongea na chombo cha habari cha Ayo TV nakuomba msaada toka kwa watanzania wamsaidie kwani sasa yupo eda na hana msaada wowote

Source : Dar 24

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio huyo
kingpic.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi habari za Misaada ifikie hatua watanzania waone aibu wasipende miteremko.

Sheria ziko wapi si aende kwenye vyombo vya Sheria apeleke malalamiko yake.

Kero sana hii.
Huwa najiuliza kwa watanzania wenye shida na hawajui wap pakupeleka shida zao inakuwaje....

Hapo inaonekana kuna mgogoro wa kifamilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom