Mke wa mwenye shule atapeliwa 600M kwa uroho

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,277
15,522
Mwanamke huyo ambaye ni mke ya mkuu wa chuo kimoja kilichopo Dodoma anayemiliki shule ya sekondari wilayani Same ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 600 ambazo walipewa mkopo toka bank kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo.

Mwanamke huyo anaesemekana kupenda sana mambo ya kishirikina alitapeliwa na watu waliojifanya waganga wa kienyeji ambao walimwambia wana uwezo wa kufanya makeke shule ikafurika wanafunzi vibaya mno kitendo kilichomchanganya mmama huyo mroho na akakubali.

Wachawi hao wa ndumba walifika maeneo ya shule na kumwambia bi mkora huyo sharti wamuue mwanafunzi mmoja shuleni hapo kwa kichawi halafu mambo mengine yafuate lakini bi mkora aliingiwa na roho ya utu na kukataa kumtoa mwanafunzi Kafara na hapo ndio wakaanza kupiga hela baada ya kumwambia mbadala wake ni kumwaga mavumba. Akatoa kwanza milioni 10, 20, 30, 40 ,50 ,70 ,70......................................................................................600 kudadadeki jamaa wakalala mbele.

Bi mkora akaanza kuona 'no changes' na badala yake shule inaendelea kudorora wakati mkopo wa 900 waliochukua bank 600 nzima ishaliwa ikabidi ajisalimishe kwa pilato kwa msaada zaidi.

Hata hivyo 'it was too little too late' kwani maprofesa hao tayari walishalala mbele kuuwahi mwaka 2016 huku wakiacha vumbi tu.

Wife of school owner conned Sh600 million
 
Last edited by a moderator:
Ila kias nampongeza apo kwa kukataa kutoa kafala mtu apo kwakweli nampongeza
 
Mwanamke huyo ambaye ni muke ya mkuu wa chuo kimoja kilichopo Dodoma anayemiliki shule ya sekondari wilayani Same ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 600 ambazo walipewa mkopo toka bank kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo. Mwanamke huyo anaesemekana kupenda sana mambo ya kishirikina alitapeliwa na watu waliojifanya waganga wa kienyeji ambao walimwambia wanauwezo wa kufanya makeke shule ikafurika wanafunzi vibaya mno kitendo kilichomchanganya mmama huyo mroho na akakubali. Wachawi hao wa ndumba walifika maeneo ya shule na kumwambia bi mkora huyo sharti wamuue mwanafunzi mmoja shuleni hapo kwa kichawi halafu mambo mengine yafuate lakini bi mkora aliingiwa na roho ya utu na kukataa kumtoa mwanafunzi Kafara na hapo ndio wakaanza kupiga hela baada ya kumwambia mbadala wake ni kumwaga mavumba. Akatoa kwanza milioni 10, 20, 30, 40 ,50 ,70 ,70......................................................................................600 kudadadeki jamaa wakalala mbele. Bi mkora akaanza kuona 'no changes' na badala yake shule inaendelea kudorora wakati mkopo wa 900 waliochukua bank 600 nzima ishaliwa ikabidi ajisalimishe kwa pilato kwa msaada zaidi. Hata hivyo 'it was too little too late' kwani maprofesa hao tayari walishalala mbele kuuwahi mwaka 2016 huku wakiacha vumbi tu.

Wife of school owner conned Sh600 million
loh itakuwa ni ile shule ya ali kachenje ipo pale makanya wilaya ya same,ambaye mumewe ni mkuu wa chuo cha UDOM,daaaaah pole sana
 
Watu hawana huruma mil.600....na angeendelea kuwa mjinga wangempiga 900 yote
 
Al Kachenje Secondary School. Unalipa waalimu laki tatu wanatoa elimu mbovu wanafunzi wanafeli wanakimbia shule then unalipa waganga wa kienyeji milioni 600?????? Verry stupid.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kama sinema vile, Yaani anatoa 10, 20, mpaka 600 alikuwa hashtuki tuu. Hatausahau huu Mwaka 2015 kama hajapata shinikizo la damu
 
Watu hawana huruma mil.600....na angeendelea kuwa mjinga wangempiga 900 yote

Nimecheka sana, maana mleta mada anajua kupamba story! Eti "maprofesa hao walilala mbele kuwahi mwaka 2016"! Hahahhaha


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Sitaki kuamini mke wa professa alafu tahira mpaka unawapa watu ml600..huyo mama kilaza elimu yake ni level gani???
 
Huyu mama ni mmoja wa wanaofurahia huduma ya asili kupigwa biti na serikali.
 
Back
Top Bottom