Mke wa Mwandishi wa Habari Azory Gwanda Kutembelewa na Kaimu balozi wa Marekani

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Apr 3, 2018
336
559
Capture.JPG
Nimeinasa kwenye Mitandao ya Kijamii ya usembassytz kuhusu Kaimu balozi wa Marekani kwenda Kumtembelea na kumtakia heri ya Sikukuu Mke wa Muandishi wa Habari za Uchunguzi Azory Gwanda ambaye Alitoweka miaka kadhaa hadi sasa kwa kuchukuliwa nyumbani kwake usiku na Watu wasiojulikana (Siwezi kusema ameuawa sababu hakuna mwenye uhakika na hilo).
Kwa kweli Hii imenifikirisha kidogo na kujiuliza maswali kadhaa.

1. Kuna kiongozi yeyote hata DC tu ambaye ameshawahi kwenda kumsabahi au vinginevyo?
2. Hivi viongozi wetu wanapoona picha hizi wanajisikiaje?...
3. Kwani uchunguzi wa suala lake umefikia wapi?
4. Huyu Mama balozi amefikia/ameona nini hadi atoke Msasani hadi Kibiti kumuona, au kumsabahi tu mke wa Muandishi huyu?

kwa mwenye majibu ya Maswali, maoni afunguke kwa ustaarabu tafadhali.
 
Amerika itatufanyia kitu mbaya soon,
Moja wapo ni vikwazo na misaada
hiyo inaweza kuwa njia moja ya kutufanya tunyooke na kupunguza utegemezi wa nje, lakini pia kuturudisha kwenye mstari kidogo.
 
Ameenda kumu intaviyuu ili aweze kwenda kuishi amerika? Kama mkimbizi baada ya kuishi kipindi kirefu bila mzazi mwenzie...?
 
Ugeni kama huo kisiasa ni jambo hatari sana. Wenye akili watakua wameelewa vizuri. Tusubiri "WAZIRI WA MAMBO YA NDANI" atoe waraka wa kuzuia mabalozi kutembelea wahanga wa kisiasa, kama alivyotoa Waziri wa mambo ya nje waraka wa kukemea nchi za magharibi kufuatilia mwenendo wa kisiasa Tanzania (Waraka wa USA, U.K na CANADA kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa).
 
Ameenda kumu intaviyuu ili aweze kwenda kuishi amerika? Kama mkimbizi baada ya kuishi kipindi kirefu bila mzazi mwenzie...?
Unakosea...ccm na hii serikali haikukuzaa,sio mjomba Wala mtu Baki kwamba atakuzika siku moja.utakufa peke yako Kama azory siku moja.usifanye kejeli kwa mjane huyu.
 
...Namkumbuka yule binti Wa shule aliyefiwa na wazazi na ndugu zake akiwa kwenye mtihani.
Ninakumbuka rundo la wanasiasa ambalo lilishuka kwake kumpa Pole na kumuahidi misaada mbali mbali.
Ninajiuliza kwa mini hakuna haya kiongozi mmoja Wa Serikali ama Chama Babalao amejitokeza kwenda kumpa Pole mama Azory na kumuahidi msaada hats Wa kumsomeshea tu watoto wake! Kulikoni? Wanajua cha kujua,?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom