Mke wa mtu ni sumu!! Kijana akatwa mkono nusura kuuliwa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa mtu ni sumu!! Kijana akatwa mkono nusura kuuliwa!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by stineriga, Jun 26, 2012.

 1. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  [​IMG]


  MWANAUME AKATWA MKONO
  Naye Victor Bariety wa Geita anaripoti kuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Nyakamwaga wilayani hapa, amenusurika kifo baada ya kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu japokuwa mwenyewe amekanusha.
  Kijana huyo alijeruhiwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto na mwanaume mmoja aliyedai kuwa anatembea na mke wake na siku ya tukio alionekana akiwa na mke wa mwanaume huyo.
  Akisimulia mkasa huo akiwa wodini kwenye Hospitali ya Mkoa wa Geita alikolazwa akitibu majeraha, mwanafunzi huyo Fikiri Mtasimwa (20), mkazi wa Kijiji cha Gengetano, Kata ya Nyakamwaga mkoani hapa alidai kuwa alikutwa na balaa hilo usiku wa Juni 17, mwaka huu wakati akinywa uji kwenye kijiwe chao.
  Alidai mwanaume huyo anayemfahamu kwa jina la baba Neema alimvamia kwenye kijiwe hicho kinachomilikiwa na binti aliyemtaja kwa jina moja la Mektirida na kuanza kumshambulia kwa mapanga sehemu za kichwani, mgongoni na begani kabla ya kumkata mapanga katika mkono wake wa kushoto na kusababisha kiganja cha mkono huo kunyofoka akimtuhumu kutembea na mkewe aliyemtaja kwa jina la mama Neema.
  “Wakati nakunywa uji nilimuona baba Neema akichomoa panga kiunoni mwake na kuanza kunikata kwa kunilenga shingoni, nilikwepa lakini bahati mbaya lilitua kisogoni na kunijeruhi ndipo nilipoamua kukimbia lakini sikufika mbali kwani nilidondoka, akanifuata na kunikata panga jingine la pili kichwani.
  “Nilinyanyuka tena na kukimbia huku damu zikivuja...nikadondoka tena, akanikata begani.
  “Inavyoonekana alikuwa na lengo la kuniua kwani alianza kunikata mkono wangu wa kushoto mara kadhaa na kiganja changu kikadondoka ndipo rafiki yangu aitwaye Fikiri William ninayesoma naye kidato cha tatu, alipofika kunisaidia na njemba hilo likatoweka na kwenda kusikojulikana nami nikapoteza fahamu,” alisema Mtasimwa.
  Alisema alijikuta yupo hospitali akiwa hana kiganja na kufafanua:
  “Siku moja kabla ya tukio nilikutana na baba Neema na kumsalimia lakini akaniambia kuwa mimi nina dharau sana wala hahitaji salamu yangu na akanitishia kuwa maisha yangu yapo hatarini, aliondoka bila kunieleza sababu.”
  MGANGA MKUU
  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Ndallo Ndallo alithibitisha kuwepo kwa majeruhi huyo katika hospitali hiyo na kuongeza kuwa hali yake ni mbaya kutokana na majeraha aliyoyapata sehemu mbalimbali za mwili.
  KAMANDA WA POLISI
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi, Leonard Paulo alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa juhudi za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hii story inakaribia kufanana na ya uncle Jei Jei aka Josephat Joseph
   
 3. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hivi ni kwa sababu ya uke tu au kuna kingine?
   
 4. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  toba!! duh kweli uchungu wa mke aujua mume mh
   
 5. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 280
  Zinduna! Unaudharau kwa sababu unaumiliki. Wengi wetu tukiuwaza basi akili huhamia katika kichwa cha mb** toka.

  Ni hatari tupu.

  Bazazi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Zinduna, acha tu, sema wewe unacho ndio maana unaona cha kawaida,:A S 11:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kumbe ku__ ni tamu kiasi hicho,sikujua.

  20 y/o @form3 mbona kachelewa shule
   
 8. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  aren't you a man?
   
Loading...